Hiyo haya ya mwisho ndio majibu ya kwanini Tanganyika sio Tanzania haiwezekani kufanyika yaliyofanyika Kenya leo au yaliyofanyika mara ya mwisho Kibaki alipotangazwa kuwa raisi awamu ya pili.
Huku Tanganyika hakuna sana siasa za ukabila isipokuwa kuna kabila fulani chache zimeanza kuhamasisha siasa za kikabila na kikanda, na bahati mbaya hata ndani ya hizo kabila kuna busara ya Mungu miongoni mwao ambao hawashabikii sana siasa za namna hiyo. Maana napo wanajikuta wanabaguana sisi wakatoliki na wale walutheri n.k.
Bahati mbaya zaidi bado hizo kabila zilizojiunga zina watu wachache kwa ujumla wao hivyo kura hazitoshi.
Na huku Tanzania bado madaraja ya watu kutokana na kipato bado sio makubwa sana kama Kenya kwenye ubepari.
Huku hata masikini anamiliki aridhi na hakuna anae kosa mahali pa kulima sababu yeye masikini. Huku kama haulimi ni uvivu wako tu.
Huku tatizo la ukosefu wa ajira sio kubwa kama Kenya.
Huku ukifanya vurugu ukafungwa au kuumizwa au kuuwawa una cha kupoteza zaidi, lakini kule wengi wa vijana ambao ndio wafanya fujo na wanaojitoa muhanga hawana cha kupoteza wengi wamekata tamaa.
Babu Odinga hana cha kupoteza(umri haumruhusu kugombea uchaguzi ujao) kuliko mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka na ndio maana hakutokea kuapishwa kama Odinga.