Baada ya kifo cha Dr. Ndugulile, kwa sasa Tanzania tusahau kabisa kuupata tena ukuu wa WHO ukanda wa Afrika, haiwezekani!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Ushabiki, ujinga na uchawa umejaa miongoni mwa watanzania wengi huku tukidhani dunia inakwenda kwa style hiyo.

Kelele za watu kuanza kupendekeza majina ya watanzania wanaofaa kwenda kugombea tena huko WHO baada ya kifo cha Dr. Faustine Ndugulile zimeshika kasi, na serikali nayo ikaja na kauli za kudai watapeleka jina lingine likagombee huko WHO!

Wengi wanadhani, Dr. Ndugulile alipelekwa na serikali ya Tz kwenda kugombea huko WHO, na wengine wanadhani Dr. Ndugulile aliibuka tu, akagombea na akashinda.

Kwa uchache sana, watu wanapaswa kufahamu kuwa Dr. Ndugulile alitumia gharama kubwa sana (ikiwemo muda, akili, kupoteza baadhi ya vitu) kwa kipindi kirefu mnoo ikijipanga kuupata ukuu wa WHO kanda ya Africa, na huenda wakati wa harakati zake hizo alipopoteza unaibu waziri wa Afya baada ya Magufuli kumshtukia kuwa ni 'kupe' wa WHO kwenye harakati za kukabiliana na Covid.

Kwa watu msiofahamu, mnapaswa kufahamu haya kuhusu nafasi mbali mbali za ajira na ukuu katika mashirika ya kimataifa.

1. Nafasi yoyote inagombewa kwa sifa binafsi, utaifa wa mhusika sio sifa ya kuchaguliwa au kutokuchaguliwa.

2. Kushinda nafasi yoyote katika ukuu wa umoja wa kimataifa inahitaji maandalizi binafsi ya mhusika kwa kipindi kisichopungua miaka minne. (Kama Tz tunataka tena hiyo nafasi, basi watu wetu waanze sasa kuwaza labda 2028 na kuendelea)

3. Ushawishi wa kimataifa wa mgombea husika katika nyanja mahususi unaweza kumfanya mhusika kupata hizo nafasi. (Sio rahisi kwa mtu ambaye sio msomi na mtafiti mzuri wa mambo ya afya kidunia akapewa nafasi ya ukuu wa kitengo cha WHO, haiwezekani)

4. Kushinda au kushindwa kunategemea sana aina ya wagombea waliopo katika huo mchuano, kanda wanazotokea na falsafa ya uchaguzi inayotawala.

(Mara nyingi hawataki kanda moja au nchi moja kupata nafasi husika mfululizo au kujirudia rudia, mara nyingi huwa ni mara moja basi!)
 
Ukiona mzungu kaachia uongozi taasisi kubwa kama WHO kwa nchi ambazo hata viongozi wake wakiumwa wanakimbia bara kimatibabu basi ujue maamuzi ya afya za ulimwengu yako katika taasisi nyingine kabisa
 
Ukiona mzungu kaachia uongozi taasisi kubwa kama WHO kwa nchi ambazo hata viongozi wake wakiumwa wanakimbia bara kimatibabu basi ujue maamuzi ya afya za ulimwengu yako katika taasisi nyingine kabisa
Watu wa aina yako nawachukia sana kwenye maisha yangu, kwa Nini ujiweke kwenye kundi la wasiofaa, kwa Nini usiamini Kuna wanaoweza kuliko wewe? Hii dhana uliyonayo ni ngumu hata kuondoa umaskini kwenye familia yako.
 
Hata hivyo haukuwa na msaada wowote kwa watanzania walio wengi.

Asha-rose Migoro amewahi kuwa Undersecretary wa UN, prof. Tibaijuka alikuwa UN Habitat lkn bado hali ya maisha ya watanzania haikubadilika na ccm iliendelea kuiba uchaguzi.
 
Watu wa aina yako nawachukia sana kwenye maisha yangu, kwa Nini ujiweke kwenye kundi la wasiofaa, kwa Nini usiamini Kuna wanaoweza kuliko wewe? Hii dhana uliyonayo ni ngumu hata kuondoa umaskini kwenye familia yako.
Usimchukuie mtoa maoni, ana haki ya kusema kile anachowaza.

Kwa mfano unaposema kuwa aamini kuna wanaoweza kuliko yeye, ni kweli wapo lakini wamefanya nini cha maana?

Binafsi naunga naye kwa pointi kuwa "kama wapo wanaoweza, hao hao mbona wakiumwa wanakimbilia nchi za nje?

Kama kuna watafiti wazuri kwenye sekta ya afya, ni dawa ipi ya ugonjwa gani imeingizwa sokoni kutokea kwenye mazingira yetu?

Je, ni kweli kuwa kila ugonjwa dawa yake lazima itoke ulaya? Igunduliwe na wazengu?

Magonjwa mengi tuliyonayo ni matokeo ya mazingira tunayoishi. Jamii za kale ziliishi miaka mingi na zilijitibu kwa dawa zake za ndani walizofanyia tafiti wenyewe kwa njia wanayoijua. Kwanini hawa wasomi wameifubaza taaluma asilia?

Binafsi nachojua, haya mashirika ya kimataifa kama WHO hayawezi kukubali kuongozwa na mtu ambaye hatasaidia kusukuma agenda zao. Wakikukubali lazima mtambue kuwa tayati ulikuwa na vinasaba nao
 
sisiemu hakuna wanaloshindwa wachague hata stivu nyerere wapeleke na ile timu ya ushindi ya kwenye uchaguzi serekare za mitaa mbona wanashinda fasta. MAJIZI WAKUBWA HAO.
 
Watu wa aina yako nawachukia sana kwenye maisha yangu, kwa Nini ujiweke kwenye kundi la wasiofaa, kwa Nini usiamini Kuna wanaoweza kuliko wewe? Hii dhana uliyonayo ni ngumu hata kuondoa umaskini kwenye familia yako.
Nimeongea uongo mkuu? Ulitaka niwe mnafiki mbele ya uhalisia unaoonekana? Mtapewaje uongozi nyeti wakati hizo nchi ambazo zinachangia bajeti ya WHO kwa asilimia zaidi ya 90% zina wabobezi bora zaidi yenu
Bajeti ya WHO kwa mwaka 2024 ilikua takribani dola bilioni 10 ila nchi za Afrika zilichangia hata dola milioni 100 hazikufika; Leo mnasema mnapewa uongozi , ili iweje kwa mfano?
 
Ukiona mzungu kaachia uongozi taasisi kubwa kama WHO kwa nchi ambazo hata viongozi wake wakiumwa wanakimbia bara kimatibabu basi ujue maamuzi ya afya za ulimwengu yako katika taasisi nyingine kabisa

Ulitaka wazungu wagombee nafasi ya DG-WHO Africa? Unajua hata unachokiongea?
 

Unajua nafasi aliyogombea na kushinda the late Ndugulile?
 
Hakuwa kupe alikuwa Chawa Yeye na Marehemu yule mtoto wa Malecela.

Wakati yupo katibu kabla ya kutumbuliwa August 17 2020 na JPM , baada ya vipenyo wa Wizara ya Afya kudaka info jamaa akilikisha prohibited info kwa mabeberu Sambamba na yule Mwera .

Hiyo nafasi ndio basi, tusiendelee kuota
Nimeshangaa Samia akisema tutapeleka motu mwenye Sifa tena lol , seems Samia is not informed kabisa how Fau got there .
Kama ingekuwa simple hivo tungepeleka miaka mingi sana, kila baada ya 4 years hizo post zinakuwa on air

Fau alikuwa na connection na hao watu wa UN na WHO, na alipata connection nao wakati yupo SA akisoma kama sikosei kisha alipopata chance pale MoH ikawa ni booster kwake ndio maana alikuwa Loyal kwa hao watu , jamaa alikuwa akiomba report as if zinahitajika state kumbe zilikuwa zinaenda kwa masponsor…..maafisa wa ngosha wakawa wanazitrack…… zinapoelekea. Wakagundua haziombwi na waziri wala Rais….. ndipo ngosha akala kichwa chap
Mtoto Wa Malecela nae akawa ni walewale tena akaenda kuleta taharuki ya zika, nae akaliwa kichwa chap…. Mabeberu wakamchukua


hao WHO ndio waliomshawishi agombee , alianza kushawishiwa na WHO team since alipotumbuliwa mwaka 2020 na jamaa wakamwambia jitahidi kupublish scientifique papers, angalieni papers zake nyingi kapublish miaka gani….. then akawa analink na academician wengi ili atokee kwenye publish tofauti tofauti.

So he saw the post 4 years Back na WHO ukienda kinyume na serikali yako kwa maslahi yao wanakupa shavu. Yes , push za Samia zilisaidia somehow…. But not that important and that was not all it took….. part kubwq alisha play na uchawa with internat lobying way back

It is not kuwa Fau alikuwa na uwezo snaa, au alikuwa na Usmaet , no
, he was average brained…..hata Kigamboni ukiicheki…. Over 5 years wala haina cha maana.

Ukiniuliza Katibu ambae ni SMART kwangu ni huyu Mpoki, jamaa ni muadilifu na ana akili…..na hana ishu na mabeberu…. Alitumbuliwaga kwa sababu ya ile ishu ya Lissu pale Dodama…..Mpoki ni Dr wa kuua na Kufufua ndio aliyesimamia ishu ya Lissu na ndie aliyeshauri asiende MNH maana technology ipo chini or else Lissu anakufa….ndipo kina mbowe wakafanya mishe chap kumpaisha Tundu Nairobi

Ngosha alivokamata hizo, akala kichwa chap , jamaa akawa anaenda kusoma magazeti pale wizara ya mambo ya nje na ole wake asifike…. Akaja kumpa ubalozi wa mchongo
 
Tanzania imeweza kueleza sababu za kifo cha mteule wa WHO?
kupewa nafasi nyingine ni ndoto
 
Uko.sahihi kabisa lakini usisahau alipata.support kubwa ya.serikali wakati ulipokuwa muafaka.

Lazima alikuwa akifanya kazi za.consultancy either who kwa muda mrefu au.hata.cdc yaani kwenye platform za afya.za dunia anajulikana kitaalamu.zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…