Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Ushabiki, ujinga na uchawa umejaa miongoni mwa watanzania wengi huku tukidhani dunia inakwenda kwa style hiyo.
Kelele za watu kuanza kupendekeza majina ya watanzania wanaofaa kwenda kugombea tena huko WHO baada ya kifo cha Dr. Faustine Ndugulile zimeshika kasi, na serikali nayo ikaja na kauli za kudai watapeleka jina lingine likagombee huko WHO!
Wengi wanadhani, Dr. Ndugulile alipelekwa na serikali ya Tz kwenda kugombea huko WHO, na wengine wanadhani Dr. Ndugulile aliibuka tu, akagombea na akashinda.
Kwa uchache sana, watu wanapaswa kufahamu kuwa Dr. Ndugulile alitumia gharama kubwa sana (ikiwemo muda, akili, kupoteza baadhi ya vitu) kwa kipindi kirefu mnoo ikijipanga kuupata ukuu wa WHO kanda ya Africa, na huenda wakati wa harakati zake hizo alipopoteza unaibu waziri wa Afya baada ya Magufuli kumshtukia kuwa ni 'kupe' wa WHO kwenye harakati za kukabiliana na Covid.
Kwa watu msiofahamu, mnapaswa kufahamu haya kuhusu nafasi mbali mbali za ajira na ukuu katika mashirika ya kimataifa.
1. Nafasi yoyote inagombewa kwa sifa binafsi, utaifa wa mhusika sio sifa ya kuchaguliwa au kutokuchaguliwa.
2. Kushinda nafasi yoyote katika ukuu wa umoja wa kimataifa inahitaji maandalizi binafsi ya mhusika kwa kipindi kisichopungua miaka minne. (Kama Tz tunataka tena hiyo nafasi, basi watu wetu waanze sasa kuwaza labda 2028 na kuendelea)
3. Ushawishi wa kimataifa wa mgombea husika katika nyanja mahususi unaweza kumfanya mhusika kupata hizo nafasi. (Sio rahisi kwa mtu ambaye sio msomi na mtafiti mzuri wa mambo ya afya kidunia akapewa nafasi ya ukuu wa kitengo cha WHO, haiwezekani)
4. Kushinda au kushindwa kunategemea sana aina ya wagombea waliopo katika huo mchuano, kanda wanazotokea na falsafa ya uchaguzi inayotawala.
(Mara nyingi hawataki kanda moja au nchi moja kupata nafasi husika mfululizo au kujirudia rudia, mara nyingi huwa ni mara moja basi!)