Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Hapa karibuni kumekuwa na kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari ya jirani, jambo ambalo bila CCTV kungekuwa na tuhuma za kuteka, uchawi na hata kuletea mtuu kuuwawa au kuungwa.
Lakini wakati tukitafakari hili tukumbeke kwamba hivi karibuni serikali imepiga marufuku CCTV kuelekezwa zaidi ya mipaka ya nyumba ya mtu mwenye hizo kamera.
Hakuna siri juu ya jambo hili, kwamba serikali imekurupuka kusisitiza juu ya sheria hii baada ya tukio la October 29, ambapo wenye CCTV wengi walisambaza video za CCTV zilizowanasa polisi wakiwapiga risasi watu wasio na hatia na kuwaua. Serikali iliumbuliwa sana na hizi video ambazo inasemekana ndizo zinaimaliza serikali kiushahidi, kiasi kwamba wamaeamua kubana matumizi ya CCTV kwa kisingizio cha "kulinda taarifa binafsi" za watu.
Soma Pia: Roho Mbaya na Wivu wa Majirani: Kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari Arusha kitufundishe umuhimu wa CCTV
Katika nchi nyingi zilizoendelea, tukio la kihalifu linapotokea mitaani, polisi huwafikia majirani wenye CCTV kuona kama camera zao ziliweza kunasa tukio hilo ili camera hizo ziwasaidie katika upepelelezi wao. Kwa hapa kwetu polisi wanapiga marufuku CCTV ili kulinda uovu unaoweza kufanywa na polisi mitaani. Hili halikubaliki na serikali inapaswa itafakari upya juu ya jambo hili badala ya maslahi ya kibinafsi ya kutotaka kuwe na ushahidi pale uhalifu wa kiserikali unapofanyika.