Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Gentleman,Hapa karibuni kumekuwa na kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari ya jirani, jambo ambalo bila CCTV kungekuwa na tuhuma za kuteka, uchawi na hata kuletea mtuu kuuwawa au kuungwa.
Lakini wakati tukitafakari hili tukumbeke kwamba hivi karibuni serikali imepiga marufuku CCTV kuelekezwa zaidi ya mipaka ya nyumba ya mtu mwenye hizo kamera.
Hakuna siri juu ya jambo hili, kwamba serikali imekurupuka kusisitiza juu ya sheria hii baada ya tukio la October 29, ambapo wenye CCTV wengi walisambaza video za CCTV zilizowanasa polisi wakiwapiga risasi watu wasio na hatia na kuwaua. Serikali iliumbuliwa sana na hizi video ambazo inasemekana ndizo zinaimaliza serikali kiushahidi, kiasi kwamba wamaeamua kubana matumizi ya CCTV kwa kisingizio cha "kulinda taarifa binafsi" za watu.
Soma Pia: Roho Mbaya na Wivu wa Majirani: Kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari Arusha kitufundishe umuhimu wa CCTV
Katika nchi nyingi zilizoendelea, tukio la kihalifu linapotokea mitaani, polisi huwafikia majirani wenye CCTV kuona kama camera zao ziliweza kunasa tukio hilo ili camera hizo ziwasaidie katika upepelelezi wao. Kwa hapa kwetu polisi wanapiga marufuku CCTV ili kulinda uovu unaoweza kufanywa na polisi mitaani. Hili halikubaliki na serikali inapaswa itafakari upya juu ya jambo hili badala ya maslahi ya kibinafsi ya kutotaka kuwe na ushahidi pale uhalifu wa kiserikali unapofanyika.
Una akili timamu kweli? Mambo gani ya kumchafua mtu atayafanya mitaani kwenye public space? Kubusiana na michepuko?Gentleman,
kulinda taarifa binafsi za mwananchi sio kipaumbele cha serikali sikivu ya CCM pekeyake tu, bali ni kipaumbele cha serikali zote za wanadamu dunia kote.
Na hivyo,
basi serikali sikivu ya CCM kamwe haiwezi kuruhusu jambo ambalo wengi hulifanya kwa makusudi tena kwa nia mbaya ili kudhalilisha utu wa mtu ambe wanawalenga kuwachafua.
Ulizi wa watoto wetu ni jukumu la wazazi na sio CCTV cameraz
Yaani fikiria serikali inaweka kipao mbele kuficha uovu wa polisi badala ya kuwa na usalama mitaani! Hii serikali inahitaji kuondolewa kwa namna moja au nyingine, hasa hiyo namna nyingine.Tulikuwa nazo mbona? Ila baada ya mauaji ya October 29 ziling'olewa karibia zote
wewe ndio unadhani ni public spaces kwasababu ya ufinyu wa uelewa na ufahamu wa jambo hili muhimu na nyeti sana na athari zake kwa utu wa mtu na faragha zake.Una akili timamu kweli? Mambo gani ya kumchafua mtu atayafanya mitaani kwenye public space? Kubusiana na michepuko?
Siku baba yako akikabwa kabali na panya road kwenye barabara mlizong'oa CCTV za watu ndio utaujua umuhimu wakewewe ndio unadhani ni public spaces kwasababu ya ufinyu wa uelewa na ufahamu wa jambo hili muhimu na nyeti sana na athari zake kwa utu wa mtu na faragha zake.
hata hivyo,
kwa kibali maalumu unaweza kufunga vifaa hivyo ili hatimae ukitokea ukiukwaji wa haki na utu wa mwananchi, uwajibike kwa mujibu wa sheria,
Lakini bado kuna mashaka makubwa dhini ya nia dhabiti ya vifaa hivyo kua kila mahali.
kwani nyinyi panyaroad siku izi mnakaba usiku na mkiona cctv camera mnaacha kukaba?Siku baba yako akikabwa kabali na panya road kwenye barabara mlizong'oa CCTV za watu ndio utaujua umuhimu wake
Tafuta dictionary uangalie maana ya neno deterrent halafu litumie kwenye CCTVkwani nyinyi panyaroad siku izi mnakaba usiku na mkiona cctv camera mnaacha kukaba?
Sawa ndugu mjumbe,Tafuta dictionary uangalie maana ya neno deterrent halafu litumie kwenye CCTV
Huyo ni kibaka, sio jambaziSawa ndugu mjumbe,
ni muhimu sana pia kutafuta kamusi ya kiswahili na kupata tafsiri na maana halisi ya CCTV na itapendeza zaidi gentleman,
ama niaje?
jambazi ni jambazi na muovu ni muovu tu gentleman, huwezi kumdiscourage kufanya uovu wake na kutimiza malengo yake kwa cctv cameras 🐒