Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Baada ya kivuko eneo la Busisi kuzingua na kushindwa kutoa huduma, watu wamevunja geti la Daraja la Magufuli, kisha kuvuka kwa mguu hadi ng’ambo kama video inavyoonesha.
Soma, Pia: Vivuko vya Kigongo-Busisi havifanyi kazi leo. Daraja lifunguliwe kwa dharura kuruhusu magari
DC ASEMA HAWAJAVUNJA GETI WAMERUHUSIWA KUPITA
Alipoulizwa na JamiiForums kuhusu kilichotokea, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga anasema “Hawajavunja geti, ilikuwa jana (Januari 26, 2025) baada ya vivuko kusimama kutoa huduma kutokana na changamoto ya uwepo wa magugumaji.
"Majani hayo yalikuwa mengi kiasi kwamba ingeweza kuathiri utendaji kazi wa vivuko, hivyo kilichofanyika ulifanyika utaratibu Wananchi wakafunguliwa geti na kupitia kwenye njia ile nyingine ya Daraja.
“Sio kweli kuwa wamevunja geti, nadhani ni ile furaha tu ya kuruhusiwa kupita ndio wakajikuta wengine wanasema hivyo, geti lipo vizuri na halina changamoto yoyote.”