Tetesi: Baada ya kivuko Busisi kuzingua, wananchi waruhusiwa kupitia katika Daraja la Magufuli na kuvuka kwa mguu hadi ng’ambo

Tetesi: Baada ya kivuko Busisi kuzingua, wananchi waruhusiwa kupitia katika Daraja la Magufuli na kuvuka kwa mguu hadi ng’ambo

Wakuu

Baada ya kivuko eneo la Busisi kuzingua na kushindwa kutoa huduma, watu wamevunja geti la Daraja la Magufuli, kisha kuvuka kwa mguu hadi ng’ambo kama video inavyoonesha.

Soma, Pia: Vivuko vya Kigongo-Busisi havifanyi kazi leo. Daraja lifunguliwe kwa dharura kuruhusu magari

DC ASEMA HAWAJAVUNJA GETI WAMERUHUSIWA KUPITA
Alipoulizwa na JamiiForums kuhusu kilichotokea, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga anasema “Hawajavunja geti, ilikuwa jana (Januari 26, 2025) baada ya vivuko kusimama kutoa huduma kutokana na changamoto ya uwepo wa magugumaji.

"Majani hayo yalikuwa mengi kiasi kwamba ingeweza kuathiri utendaji kazi wa vivuko, hivyo kilichofanyika ulifanyika utaratibu Wananchi wakafunguliwa geti na kupitia kwenye njia ile nyingine ya Daraja.

“Sio kweli kuwa wamevunja geti, nadhani ni ile furaha tu ya kuruhusiwa kupita ndio wakajikuta wengine wanasema hivyo, geti lipo vizuri na halina changamoto yoyote.”
Mitano tena
 
Point ni kwamba, wahusika wa daraja wakifunga geti, si salama kulazimisha kutumia daraja.

Labda wamefunga kwa sababu kuna matengenezo fulani yamefanyika na kuna sehemu watu wakipita itatokea ajali.

Sasa hapo ukilazimisha kupita ikatokea ajali utamlaumu nani?

Suala si kupitisha magari mazito, suala ni kwamba hujapewa ruhusa kupita hujui daraja lina mapungufu gani bado.
Mbona ufafanuzi wa mkuu wa wilaya unaonesha wamefungua makusudi ili kuwahudumia raia?
 
Back
Top Bottom