King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Aisee mitiki panda mbali na mazao ya chakula ,inashauriwa hivyo. Inataka maji mengi pia inatengeneza sumu inayoua mimea mingine karibu yake, ivyo usiweke karibu na mazao ya chakula wala miti mingine.
Sio majina tu, hata koo zao ni tofauti. Ngoja nikabukue tena, nikupe tofauti ya kimaumbile ili hata kama unataka kununua basi kigezo cha kwanza kiwe umbile. Kuna masikio na idadi ya chuchu. Kuna urefu holizontally. Wajuba wasije wakakuuzia viguruwe dwarf.
AINA ZA NGURUWE (baadhi)
LARGE WHITE
-Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya nguruwe wa kufugwa nyumbani
-Kama jina lake lilivyo ana rangi nyeupe mwili mzima
-masikio yake yamesimama wima
-Ana sura iliyobonyea kwa ndani (dish faced)
LANDRACE
-Weupe mwili mzima
-masikio yamelala kabisa
-Wana ukubwa wa wastani
SADDLEBACK
-Ni wakubwa
-Wana rangi nyeusi na mstari mweupe kuzunguka shingo na miguu ya mblele
-Masikio yamelala kiasi
Mkuu hongera sana mwanzo mzuri
nami nataka kuwa na wazo kama lako unanishaurije nianzeje
maana nimechoka na kuajiriwa
Tafuta eneo zuri, kubwa na linalofikika nje ya mji bila kusahau suala la usalama.Angalia maji kama yanapatikana. Kwa nini eneo kubwa, sababu, baada ya muda mfupi utagundua kwamba huna sehemu ya kuweka wastes/mbolea za mifugo, huna jinsi ya kupanua mradi, huna jinsi ya kuongeza mradi uliozaliwa baada ya kuwepo raw material kutoka mradi wa kwanza, mfano, unazalisha mbolea nyingi sana ambayo ungetumia kulima bustani, unazalisha maziwa mengi,unahitaji kisehemu kujenga kakiwanda ka kusindika maziwa, etc.
Mkuu kuhusu hali ya hewa ambayo mitiki inakubali hilo siwezi nikakupa jibu sahihi sana. Ila nifaamuvyo mimi ni kuwa mitiki inakubali sana sehemu za baridi. Hata sehemu za joto Kama Morogoro inakubali pia. Dar na pwani mitiki inaweza kukubari vizuri sana.Ukame ule Kama wa singida, Dodoma na shinyanga siyo mzuri Kwa maendeleo ya mitiki kwani itakufa Kwa kukosa maji. Haipendi sana sehemu yenye unyevu wa kupitiliza. Hapa morogoro Miti ya mitiki hulimwa sana mahenge , kilombero mvomero- hasa turiani na Iringa wameanza kulima Kwa kasi.
Soko la mitiki like wazi kabisa. Heka moja unaweza kutengeneza hadi 120 millions Tsh. Pia ukiwa na heka mbili za mitiki zenye umri wa miaka miwili unaweza ukaenda bank na kuvuta mkopo hadi sh 50 milioni. Ni akiba nzuri uzeeni( pension yako). Mimi ,nimejipangia kila mwaka kupanda si chini ya hekari tano za mitiki.
Naomba wanaofahamu zaidi mazingira na faida ya mitiki wanisaidie Katika kumwelimisha huyu ndugu.
Mimi naweza nikakuuzia miche ya mitiki Kwa sh 300 Kwa mche.
Mkuu, ni umbali gani unatakiwa kupanda mtiki hadi mtiki? Namaanisha intavo... Mimi nipo Pwani na viheka vyangu kama 20 hivi nataka kama Mungu akipenda nivipige mitiki afu mambo mengene yaendelee mbele. Jaman shamba halitupi...
Kwa mujibu wa watalaam wa misitu, ili upate mavuno mazuri ya mbao, tumia 3m x 3m na kama unataka kupata boriti ( mlingoti) nzuri, basi tumia 2m x 2m.
Umri wowote kuanzia miaka mitatu.Malila asante sana kwa kunihakikishia vpmo. Hapo juu kuna mtu kauliza swali ambalo nadhan halikujibiwa kwa ufasaha. Kuhusu kupata mkopo bank miti inatakiwa iwe na umri gani na unahitaji vitu gani?
Kuhusu vitu vinavyohitajika malila atatueleza.Malila asante sana kwa kunihakikishia vpmo. Hapo juu kuna mtu kauliza swali ambalo nadhan halikujibiwa kwa ufasaha. Kuhusu kupata mkopo bank miti inatakiwa iwe na umri gani na unahitaji vitu gani?
Kuhusu vitu vinavyohitajika malila atatueleza.
Kuhusu vitu vinavyohitajika malila atatueleza.
J2 Nitakuwepo. Karibu.Mkuu J2 ntakuwa MORO naweza kukuona?
Bahati mbaya sana nchi yetu hakuna bima ya misitu,na misitu ya makampuni makubwa bima ziko nje ya nchi. Sio porojo, nimefuatilia sana hili suala kwa sababu lina niathiri kwa namna moja. Pili, ni ugumu ktk kupata hati miliki za mashamba tuliyootesha misitu yetu. Ngoja tuone hizi hati za kimila kama zitakubalika benki. Suala la tatu ni scale, huwezi kumwambia banker aje kuangalia robo eka ya miti, utakuwa unamtania, labda ukiwaita jamaa wa kupima hewa ya ukaa,hao ni size yao.
Kwa ufupi ni kwamba, misitu haina bima, pia hati kwa akina pangu pakavu ni tatizo, na scale ya shamba kwa wengi ni issue. Ila kwa wale walio na hati miliki, unaweza kuingia benki na kuvuta kitu.
Hivi ni banker gani atakupa mkopo kama huna hati,una robo eka na msitu hauna bima ya moto? Hata ile misitu ya serikali haina bima kabisa.
Malila ahsante sana kwa ufafanuzi wako nmependa sana hiyo. Kweli Tz yetu hii ni matatizo... Mkuu tumeyavulia ni sharti tuyaoge, vyo vyote vile.
Hiyo hewa ya ukaa inapimwaje?Niko na pilika za kupata hizi hati za kimila. Zikikubalika benki,basi tutakuwa tumetoka kaka. Kaza buti, usiache kupima hewa ya ukaa, huenda ikawa mkombozi wa nguvu zaidi kwa wadau wa misitu.
Niko na pilika za kupata hizi hati za kimila. Zikikubalika benki,basi tutakuwa tumetoka kaka. Kaza buti, usiache kupima hewa ya ukaa, huenda ikawa mkombozi wa nguvu zaidi kwa wadau wa misitu.
Malila, hewa ya ukaa ndo kitu gani tena kaka? Na je inapimwaje? Embu nifumbue macho mwenzako...