Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Safi sana kwa huu uzi mzuri....Nakumbuka darasa la pili au la tatu kwenye shairi la karudi baba mmoja toka safari ya mbali kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili watoto wake wakaja ili kumtaka hali kama mnataka mali? Mtayapata shambani.
 
Aisee mitiki panda mbali na mazao ya chakula ,inashauriwa hivyo. Inataka maji mengi pia inatengeneza sumu inayoua mimea mingine karibu yake, ivyo usiweke karibu na mazao ya chakula wala miti mingine.

Siku zote nimekuwa nikijiuliza swali hili, je hii miti ya mitiki ni salama? Maana hawa wazungu huwa wanatuletea vitu vinavyo onekana vina faida kumbe baada ya miaka kadhaa ni kilio, ardhi inaishiwa rutuba. Kule mkoani Kagera kuna miti walileta wazungu miaka hiyo ya ukoloni, imechangia kwa kiasi kikubwa kuharibu ardhi, maana inakausha udongo.
 
Sio majina tu, hata koo zao ni tofauti. Ngoja nikabukue tena, nikupe tofauti ya kimaumbile ili hata kama unataka kununua basi kigezo cha kwanza kiwe umbile. Kuna masikio na idadi ya chuchu. Kuna urefu holizontally. Wajuba wasije wakakuuzia viguruwe dwarf.

AINA ZA NGURUWE (baadhi)

LARGE WHITE

-Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya nguruwe wa kufugwa nyumbani
-Kama jina lake lilivyo ana rangi nyeupe mwili mzima
-masikio yake yamesimama wima
-Ana sura iliyobonyea kwa ndani (dish faced)

LANDRACE
-Weupe mwili mzima
-masikio yamelala kabisa
-Wana ukubwa wa wastani

SADDLEBACK
-Ni wakubwa
-Wana rangi nyeusi na mstari mweupe kuzunguka shingo na miguu ya mblele
-Masikio yamelala kiasi
 
Nimebanwa hadi nasahau kutimiza ahadi, asante kwa kunisaidia kutimiza ahadi yangu kwenye jukwaa letu.
 
Mkuu hongera sana mwanzo mzuri
nami nataka kuwa na wazo kama lako unanishaurije nianzeje
maana nimechoka na kuajiriwa

Tafuta eneo zuri, kubwa na linalofikika nje ya mji bila kusahau suala la usalama.Angalia maji kama yanapatikana. Kwa nini eneo kubwa, sababu, baada ya muda mfupi utagundua kwamba huna sehemu ya kuweka wastes/mbolea za mifugo, huna jinsi ya kupanua mradi, huna jinsi ya kuongeza mradi uliozaliwa baada ya kuwepo raw material kutoka mradi wa kwanza, mfano, unazalisha mbolea nyingi sana ambayo ungetumia kulima bustani, unazalisha maziwa mengi,unahitaji kisehemu kujenga kakiwanda ka kusindika maziwa, etc.
 
asante kwa kunichauri ndugu yangu nitajihidi kuufanyia kazi ubarikiwe kwa mawazo haya
Tafuta eneo zuri, kubwa na linalofikika nje ya mji bila kusahau suala la usalama.Angalia maji kama yanapatikana. Kwa nini eneo kubwa, sababu, baada ya muda mfupi utagundua kwamba huna sehemu ya kuweka wastes/mbolea za mifugo, huna jinsi ya kupanua mradi, huna jinsi ya kuongeza mradi uliozaliwa baada ya kuwepo raw material kutoka mradi wa kwanza, mfano, unazalisha mbolea nyingi sana ambayo ungetumia kulima bustani, unazalisha maziwa mengi,unahitaji kisehemu kujenga kakiwanda ka kusindika maziwa, etc.
 
Mkuu kuhusu hali ya hewa ambayo mitiki inakubali hilo siwezi nikakupa jibu sahihi sana. Ila nifaamuvyo mimi ni kuwa mitiki inakubali sana sehemu za baridi. Hata sehemu za joto Kama Morogoro inakubali pia. Dar na pwani mitiki inaweza kukubari vizuri sana.Ukame ule Kama wa singida, Dodoma na shinyanga siyo mzuri Kwa maendeleo ya mitiki kwani itakufa Kwa kukosa maji. Haipendi sana sehemu yenye unyevu wa kupitiliza. Hapa morogoro Miti ya mitiki hulimwa sana mahenge , kilombero mvomero- hasa turiani na Iringa wameanza kulima Kwa kasi.

Soko la mitiki like wazi kabisa. Heka moja unaweza kutengeneza hadi 120 millions Tsh. Pia ukiwa na heka mbili za mitiki zenye umri wa miaka miwili unaweza ukaenda bank na kuvuta mkopo hadi sh 50 milioni. Ni akiba nzuri uzeeni( pension yako). Mimi ,nimejipangia kila mwaka kupanda si chini ya hekari tano za mitiki.

Naomba wanaofahamu zaidi mazingira na faida ya mitiki wanisaidie Katika kumwelimisha huyu ndugu.

Mimi naweza nikakuuzia miche ya mitiki Kwa sh 300 Kwa mche.

Mkuu, ni umbali gani unatakiwa kupanda mtiki hadi mtiki? Namaanisha intavo... Mimi nipo Pwani na viheka vyangu kama 20 hivi nataka kama Mungu akipenda nivipige mitiki afu mambo mengene yaendelee mbele. Jaman shamba halitupi...
 
Kwa mujibu wa watalaam wa misitu, ili upate mavuno mazuri ya mbao, tumia 3m x 3m na kama unataka kupata boriti ( mlingoti) nzuri, basi tumia 2m x 2m.
 
Malila asante sana kwa kunihakikishia vpmo. Hapo juu kuna mtu kauliza swali ambalo nadhan halikujibiwa kwa ufasaha. Kuhusu kupata mkopo bank miti inatakiwa iwe na umri gani na unahitaji vitu gani?
 
Umri wowote kuanzia miaka mitatu.
 
Malila asante sana kwa kunihakikishia vpmo. Hapo juu kuna mtu kauliza swali ambalo nadhan halikujibiwa kwa ufasaha. Kuhusu kupata mkopo bank miti inatakiwa iwe na umri gani na unahitaji vitu gani?
Kuhusu vitu vinavyohitajika malila atatueleza.
 
Bahati mbaya sana nchi yetu hakuna bima ya misitu,na misitu ya makampuni makubwa bima ziko nje ya nchi. Sio porojo, nimefuatilia sana hili suala kwa sababu lina niathiri kwa namna moja. Pili, ni ugumu ktk kupata hati miliki za mashamba tuliyootesha misitu yetu. Ngoja tuone hizi hati za kimila kama zitakubalika benki. Suala la tatu ni scale, huwezi kumwambia banker aje kuangalia robo eka ya miti, utakuwa unamtania, labda ukiwaita jamaa wa kupima hewa ya ukaa,hao ni size yao.

Kwa ufupi ni kwamba, misitu haina bima, pia hati kwa akina pangu pakavu ni tatizo, na scale ya shamba kwa wengi ni issue. Ila kwa wale walio na hati miliki, unaweza kuingia benki na kuvuta kitu.

Hivi ni banker gani atakupa mkopo kama huna hati,una robo eka na msitu hauna bima ya moto? Hata ile misitu ya serikali haina bima kabisa.
 
Malila ahsante sana kwa ufafanuzi wako nmependa sana hiyo. Kweli Tz yetu hii ni matatizo... Mkuu tumeyavulia ni sharti tuyaoge, vyo vyote vile.
 
Niko na pilika za kupata hizi hati za kimila. Zikikubalika benki,basi tutakuwa tumetoka kaka. Kaza buti, usiache kupima hewa ya ukaa, huenda ikawa mkombozi wa nguvu zaidi kwa wadau wa misitu.
 
Hiyo hewa ya ukaa inapimwaje?
 
Niko na pilika za kupata hizi hati za kimila. Zikikubalika benki,basi tutakuwa tumetoka kaka. Kaza buti, usiache kupima hewa ya ukaa, huenda ikawa mkombozi wa nguvu zaidi kwa wadau wa misitu.

Malila, hewa ya ukaa ndo kitu gani tena kaka? Na je inapimwaje? Embu nifumbue macho mwenzako...
 
Ni carbon dioxide,
Kwenye respiration ya miti,kuna wakati mti huhitaji oxygen na baadae hutoa carbon dioxide ambayo tena huchukuliwa na mimea hiyo hiyo na mwisho hutoa oxygen.

Kilichotokea duniani ni kwamba hewa ya carbon dioxide imezidi sana(shughuli za viwanda), kiasi kwamba mimea iliyopo haiwezi kufyonza yote, hata maji hayawezi kufyonza, hata udongo hauwezi kufyonza kuimaliza nk. Kwa hiyo wenye dunia wamekuja na mpango wa kuongeza miti zaidi ( mkataba wa kyoto) duniani. Nchi zote zenye viwanda vingi pamoja na makampuni yenye viwanda yanachangia mfuko huu.

Kwa hiyo mtu ye yote aliyeotesha miti baada ya mwaka 1990, yaani baada ya Mkataba wa Kyoto anastahili kulipwa posho kwa sababu miti yake inapunguza hewa hiyo. Kwa hapa Tz SUA ndio wanashughulikia suala hilo.

Watalaamu hawa wa SUA, wanapima kipenyo cha mti,wanachukua umri wa mti,kupitia formula yao wanapata Biomass, kutokana na Biomass hiyo wanapata uzito wa hewa hiyo kwa tani. Bei kwa tani moja ni siri mkuu.Kuna makampuni kadhaa ya misitu wameanza kulamba malipo, ni malipo manene kaka.

Nimekupa kwa ufupi sana,ili walau ujue kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom