Bahati mbaya sana nchi yetu hakuna bima ya misitu,na misitu ya makampuni makubwa bima ziko nje ya nchi. Sio porojo, nimefuatilia sana hili suala kwa sababu lina niathiri kwa namna moja. Pili, ni ugumu ktk kupata hati miliki za mashamba tuliyootesha misitu yetu. Ngoja tuone hizi hati za kimila kama zitakubalika benki. Suala la tatu ni scale, huwezi kumwambia banker aje kuangalia robo eka ya miti, utakuwa unamtania, labda ukiwaita jamaa wa kupima hewa ya ukaa,hao ni size yao.
Kwa ufupi ni kwamba, misitu haina bima, pia hati kwa akina pangu pakavu ni tatizo, na scale ya shamba kwa wengi ni issue. Ila kwa wale walio na hati miliki, unaweza kuingia benki na kuvuta kitu.
Hivi ni banker gani atakupa mkopo kama huna hati,una robo eka na msitu hauna bima ya moto? Hata ile misitu ya serikali haina bima kabisa.