Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Kaka ninaendelea kufuatilia topic yako, inazidi kunifungua masikio na macho. Sawa na maneno " wana masikio hawatasikia wana macho hawataona" Ninamtukuza Mungu kwa ajili hili jukwaa na kukutuma ww uwe mlango wa wengine kupitia.
Sidhani kama tunaojipanga kuanzisha miradi hii by january yutakuwa tumechelewa.
Kaka ninakusihi usituache hewani kwani elimu unayotuachia ni kubwa mno hasa kwetu sisi tulio kwenye ajira za kitanzania.
Endelea kutulisha sawa na haja za mipango yetu na Mungu azidi kukubariki!
 
Kaka bado nafuatilia kwa makini topic yako yenye kutujenga sisi wenye kiu ya mabadiliko ya kiuchumi.
Sidhani kuwa mimi niliyeanza kuuona mwanga huu hivi karibuni kuwa nitachelewa nikianza mradi kama huu januari.
Endelea kutulisha chakula hiki na Mungu atakubariki. Ninaamini hapo ulipo ni mbali kiuchumi ingawa naelewa namna unavyosugua kichwa na kwangu ni changamoto kubwa.
Hongera kwa hatua uliyofikia. Mungu akubariki sana!
 
 
Pia MKUU Malila bado nasubiri khs Ile shule uliyoahidi khs ukoo wa hawa Nguruwe 7bu nategemea kuingia kwenye hii maneno kuanzia January nimepata EKA1 Mlandizi kwahiyo nakusanya Taarifa ili ikiwa ni pamoja najua aina na tabia zao kwa Ujumla na niaina gan nzuri kwa Kufuga! Natanguliza shukrani sorry ikiwa niki Nje ya mada wakuu!
 
Mkuu malila unajua sijafatilia sana post zako ila nazidi kujifunza jinsi ulivyo dip katika fani hii. Nazidi kuelimika. Nashukuru Mungu kunipa uwezo wa kujifunza haraka. Tupo pamoja mkuu. Hawa wa maziwa sijawahi kuwafuga na kwa somo lako sitowafuga kabisaa.
 

Unaweza kununua madume haya ya kisasa ya mbuzi wa maziwa ili upate crossbreed. Kizazi utakachopata hapo ni kizuri sana mkuu.
 
Mkuu Mungu akuzidishie,nashawishika sana na uziwako huu wenye maudhui ya ukombozi kiuchumi
 
na mm nseme hongera sn pia MUNGU akubariki kwa kutokua mchoyo na kuamua kushare with us hatua ulizo pga big up sn kama hutojali ntaku-pm kwa info zaid, kngne klicho nifurahisha ni kua mm mwnyw ni mkaz wa morogo hongera mwana morogoro mwenzang!
 
Wakuu nimefanikiwa kutotolesha vifaranga vingi sana. Shida iliyopo ni vifaranga kuugua ugomjwa unaosababisha viduae kwa maana za kujikunyata na kutochangamka. Msaada wa aina ya CHANJO ya kuwaponya vifaranga wangu. Other wise mambo yangu yanaendelea kuwa super. Very soon I am going to be big dad.
 

Vinajikunyata tu basi? hakuna Dalilu zingine? kama kinyesi chao, make kujikunyata tu inaweza kuwa ni baridi pia, so jaribu kuchunguza na mambo mengine hasa Kinyesi chao kikoje,
Na unatakiwa kwa makini sana kwa sababu mara nyingi vifo vingi sana hutokea kwenye vifaranga hasa wiki kama 3 za mwanzo,
 
Kuna wawili ambao wako dhaifu kabisa. Siyo baridi.
 
Mkuu pole sana ila usikate tamaa, je uliwapa chanjo yoyote? Wako wiki ya ngapi? Kwanza watenge wagonjwa, osha vyombo na ondoa vinyesi vyao wiki 3 za mwanzo ulitakiwa uwe umewapa chanjo ya kideri na amprolium kuzuia coccidiosis. Nenda famasi waelezee dalili zote kama ni kideri utapewa antibiotics kuzuia baadhi ya vifaranga., lakini wakimaliza kumbuka kuwapa amprolium wiki ya 3. Pamoja na antibiotics nunua vitamin kuwapa nguvu na kinga. Naomba usome uzi wa Kubota kaelezea humo. Kujikunyata au kuvaa koti ni dalili ya homa na hutokea kwa magonjwa mengi tofauti. Kila la heri.
 
Asante mama Joe. Vile vifaranga Vyangu viwili vimekufa leo. Nimesikitika na kuumia sana. Ninapambana kuvilinda vingine visife kwa kuwapatia CHANJO .
 
Pole sana mkuu,ila naamin mungu yu pamoja na jitihada zako na hatakuacha nyuma hata mara moja.hizo ni baadhi ya changamoto lakin kumbuka kuwa hakuna hali ya kudumu na kupotea ndo kujua njia mkuu.

asante mama joe. Vile vifaranga vyangu viwili vimekufa leo. Nimesikitika na kuumia sana. Ninapambana kuvilinda vingine visife kwa kuwapatia chanjo .
 
Ninao large white na landrace na pia cross breed ya hao

Nini kinawatofautisha! Niyupi bora kati yao na Mbegu yake inapatikana wapi? mi niko DAR natamani kujua cz nami nataka kuwafuga hawa wanyama naomba kuelimishwa wandugu!
 

Mkuu hongera sana.
All I can say ni kuwa nimesoma kila post ktk uzi huu...na nimepata ARI mpya ktk mawazo yangu. Mungu akubariki sana coz naamini umewapa CHANGAMOTO watu wengi kupitia uzi huu...mimi nikiwa mmoja wapo.

Nimechukua namba yako uliyoitoa hapa ktk uzi huu...naomba usinichoke coz "nitakusumbua" sana.

Ubarikiwe!
 

Unaponunua nguruwe wa kufuga angalia idadi ya chuchu za majike. Nimeona nitoe hii njia rahisi ya kujua mbegu nzuri ya hawa nguruwe.

Nguruwe jike mwenye chuchu 12 au 14 ni mzuri sana kwa sababu anaweza kuzaa mizao mpaka mitano bila kubadilika umbo lake(kunenepa mpaka kushindwa kuinuka) na hivyo kukuhakikishia faida kubwa. Ukiona jike mwenye chuchu 16 au 18, ujue huyo anaweza akazaa vizuri mara mbili,halafu akanenepa sana hadi kuburuza tumbo,kundi la large white wanaangukia hapa. Kundi hili la chuchu nyingi ni wazuri sana kwa biashara sababu wananenepa haraka sana,tatizo ndilo hilo la kununua majike kila wakati.

Kwa hiyo, kupitia ujanja wa kuhesabu chuchu, unaweza chagua mbegu sawa na plan zako. Kwa anayeanza, ni bora kuanza na hawa wa chuchu chache ili upate wazazi wengi wanaoweza kutema mzigo wa nguvu kwa muda mrefu. Mradi ukishasimama,unaanza kuchanganya na hawa wa chuchu nyingi.

Nguruwe ni heavy feeder, andaa bustani kabisa kwa sababu anazalisha mbolea bora nyingi kwa muda mfupi.
 
Nimeisoma hii mkuu malila. Pamoja na sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…