Tatu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2006
- 1,143
- 372
Baada ya kumaliza degree yangu ya pili na kuona kuwa ajira kama ajira haiwezi kuwa mkombozi wangu kiuchumi niliamua nifatilie mawazo mbalimbali ya ujasiriamali. Nikafikiria ujasiriamali wa kiubunifu wa hali ya juu ndiyo utakuwa mkomnozi wangu kiuchumi. Nimeanza Kwa kununua shamba lenye ukubwa wa hekari 11 nje kidogo ya mji wa Morogoro ( Kwamakunganya-majichumvu). Imenigharimu 1.3 m kununua eneo hili lote.. Nililipia taratibu hata sasa bado nadaiwa sh 60 elfu nayotegemea kuimalizia after 2 weeks. Sehemu kubwa ya shamba langu nimepanda mitiki.
Baada ya kufatilia humu nikagundua kuwa mradi wa nguruwe na kuku wanalipa sana. Kwa kuwa imani yangu inaniruhusu nikaona ni laziima niifanya hii ya kitimoto pia. Hivyo nikaanza maandalizi ya kufuga nguruwe na kuku pia. Hivyo nilianza Kwa kuanzia kuchimba na kujengea tangi la maji chini. Ilimigharimu Kama miezi miwili tangu langu la maji kukamilika. Tangi langu la maji Lina uweze wa kujaza maji lita 30 elfu. .
Baada ya hapo nikaanza maandalizi ya ujenzi wa banda la nguruwe na la kuku. Baada ya mabanda yangu kukamiliaka nilisafiri hadi singida kufata kuku. Bei ya kuku singida inalidhisha sana. Ili upate kuku wa bei rahisi inakupasa uende kijijini ambako kuu huuzwa cheap. Hivyo nilisafiri hadi kijijini ambako nililinunua kuku 31 ambao ndiyo nimeanza nao.. Kwa upande wa nguruwe nimeanza na 12 ambao niliwanunua wakiwa na miezi mitano. Pia nimeweka kanga na mbuzi Kwa ushauri wa marafiki.
Ninashukuru Mungu ninaanza kuwaona kuku wameanza kutaga Kwa fujo. Pia ninamshukuru Mungu Kwa kuwa ninaona ninaanza kuwa muajili pole pole. Pia ninamshukuru Mungu ninaona mawazo ya kunyanyasika( kuajiliwa) yanaanza kupotea taratibu.
Kupitia uzi wangu huu nitakuwa nawataarifu maendeleo ya mifugo yangu Kama sehemu ya kuwatia moyo wajasiriamali wenzangu. Morogoro ni sehemu ambayo wajasiriamali mnaweza kutimiza ndoto zenu Kwa kuwa Ardhi inapatikana Kwa bei nafuu na ni Karibu na Dar kwenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali.
Hongera sana ndugu. Kwa kweli unahitaji pongezi kwa uamuzi, ujasiri, kazi na hatua uliyofikia.
Mzee wangu aliacha kazi wakati nikiwa mdogo sana akaanza kilimo na ufugaji. Ng'ombe mmoja alikuwa anatoa mpaka lita 24 za maziwa asubuhi na lita mpaka 18 jioni kama wakila vizuri na maji ya kutosha. You can imagine how much milk we were getting from 4 - 6 cows. Tulikuwa tunauza maziwa na mengine tunagawa kwa ndugu wa karibu na marafiki. Kilimo kilikuwa cha maharage na mahindi. Tulikuwa tunalima mpaka heka 300 za maharage.
Kipindi hicho sikuelewa kwanini mzee aliacha kazi akiwa kijana bado. Baadae baada ya kumaliza college na kufanya kazi kwa miaka 3 ndio nikapata sababu.
Keep it up. Everybody has to start somewhere.
You have chosen the right path. Wish you all the best.