Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Jamani watu wengi wamenipm Kwa ushauri na maeneo Morogoro. Kwa leo na kesho ninapatikana hapa dar maeneo ya mabibo hostel(kituo). Mahal I : lunch time hotel. Tunaweza tukashauriana mambo mengi. Nawatakia jioni njema..
Kwa sasa niko na NDESSA hapa mabibo hostel tunabadilishana mawazo.
 
Hongera mkuu kwa kulianzisha! Maneno yako hapo juu yananiuma sana jinsi tuliokwenye ajira tunavyoona manyanyaso! Mshahara wa kupimiwa hata ujitumeje? Baadhi ya kazi nyingi hakuna uhusiano kati ya kipato na kuchapa kazi! Hizi ajira zetu nyingine unakuta mvivu anatesa wachapakazi wanaadhirika! Kubebana, na ubaguzi wa kila aina, ukipishana kauli na boss kazini jua imekula kwako! Wanaonufaika ni wale wanaojua kujipendekeza na kupeleka majungu kwa wakubwa. Wakati mwingine ukiwa mchapakazi unajengewa chuki wakidai unakihelehele! Ukileta kutaka kutumia utaalamu sana baadhi ya maeneo ya kazi unaonekana unaleta usomi unabigwa benchi. Eneo pekee ambako mtu unafursa kutumia vipawa vyako, utaalamu wako na yote ulivyojaaliwa na Mola kwa manufaa yako ni kwenye ajira binafsi! Uwoga wa baadhi yetu ndiyo kaburi letu, nimejiwekea kipindi cha mpito miaka 3 nikamilishe nyenzo za kuanzia maana jamani mikakati ni muhimu pia! Hata Robert Kiyosaki alijiandaa kabla hajatimua! Naamini hata Chasha alijiandaa pia. Mkuu Chasha nasema nitachoma MELI! Liwalo na liwe!!
mkuu uko sahihi kabisa. Kabla ya kuacha kazi ni muhimu kuhakikisha unatumia vyema mshahara na mikopo Katika kuanzisha shughuli za ujasiriamali. Ikishasimama ndiyo unajiondoa.
 
Hongera sana mkuu huo ni mwanzo mzuri tena sana, kitu cha msingi me ninakushauri zidisha commitment kwa sasa and then at the end of the day money will work for you and not you to work for money. Ni hayo tu mkuu.
 
aisee nimeipenda hii,,niko njiani kufuata nyayo zako,now najipanga kuwatafuta wadau wenye ujuzi wa miti ili nipate mawili matatu kabla ya kuanza,lakini kabla ya mwaka huu kuisha nitakuwa na la kusimulia kama wewe hapo mkuu...kwakweli mafanikio yapo karibu kuliko tunavyodhani,kama tukiwa na jicho ya udadisi...kaza mwendo kaka.
 
Mkuu kuhusu hali ya hewa ambayo mitiki inakubali hilo siwezi nikakupa jibu sahihi sana. Ila nafamuvyo mimi ni kuwa mitiki inakubali sana sehemu za baridi. Hata sehemu za joto Kama Morogoro inakubali pia. Dar na pwani mitiki inaweza kukubari vizuri sana.Ukame ule Kama wa singida, Dodoma na shinyanga siyo mzuri Kwa maendeleo ya mitiki kwani itakufa Kwa kukosa maji. Haipendi sana sehemu yenye unyevu wa kupitiliza. Hapa morogoro Miti ya mitiki hulimwa sana mahenge , kilombero mvomero- hasa turiani na iringa wameanza Kilimanjaro Kwa kasi.

Soko la mitiki like wazi kabisa. Heka moja unaweza kutengeneza hadi 120 millions Tsh. Pia ukiwa na heka mbili za mitiki zenye umri wa miaka miwili unaweza ukaenda bank na kuvuta mkopo hadi sh 50 milioni. Ni akiba nzuri uzeeni( pension yako). Mimi ,nimejipangia kila mwaka kupanda si chini ya hekari tano za mitiki.

Naomba wanaofahamu zaidi mazingira na faida ya mitiki wanisaidie Katika kumwelimisha huyu ndugu.

Mimi naweza nikakuuzia miche ya mitiki Kwa sh 300 Kwa mche.

mkuu naomba uniuzie mbegu kwani nipo mbali na namna ya kusfirisha miche ni ngumu, naomba uniuzie mbegu
 
mkuu naomba uniuzie mbegu kwani nipo mbali na namna ya kusfirisha miche ni ngumu, naomba uniuzie mbegu

Tuwasiliane. Upandaji . Nakushauri upande wakati wa mvua. Kusafilisha unaweza kutumia Kwa mabasi.
 
Mkuu kama naweza kupata shamba la hekari tatu mpaka tano kwa garama ya laki nne mpaka tano maeneo hayo naomba unisaidie hata kwa mawasiliano ya huyo mtu. Bado nipo chuo lakini nimeona ni investment ambayo naweza kuimudu kwa pesa ya boom. btw hongera sana kwa kuwa mbunifu.
 
Miongoni mwa siku ambazo najivunia kuwa mwanachama wa JF ni leo!

Nikiri kuwa nimepata shule ya maana sana kwa leo, nina eneo la takribani ekari 12 mpango ilikuwa ni kuligawa.

•Ekari 2 mazao ya chakula, yaani kuhakikisha kuwa ndani ya mwaka mmoja sinunui mahindi wala maharage kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya chakula, ziada nauza kwa ajili ya kununua aina nyingine za vyakula.

• Ekari 5 kuzipanda mananasi, kila ekari inaingia karibu miche 3500 nanasi halina tabu sana kwenye kulilea, likiwa tayari unauza ukiwa shamba moja kwa sh 550/ ukipeleka mwenyewe sokoni ni sh 1000/= Hesabu inakuwa hivi miche, 3500 kwa hekari moja mara 5 = 17500, chukulia umepata mananasi 17000 mara 550 (ukiuuzia shamba) = 9,350,000/= (Mananasi si zaidi ya miezi 11).

• Ekari 3 natupia mitiki hakiba ya baadae kwa ajili ya makamanda wangu 2, wakifikisha miaka 20 itakuwa tayari kuvuna.

• Mifugo ekari 1, kipaumbele ni kuku, mbuzi na ng'ombe. Sasa hivi ukiwa na ng'ombe 4 ulio walisha vizuri kima cha chini ukiwauza wote ni karibu 1.6M, hapo bado kuku, na mbuzi.

Mpango ni kuwa na hekari 40 kabla ya kufikisha 35
 
Vizuri. Nimeipenda hii. Keep it up!
 
Jamani kuna watu wengi sana wananiuliza Kwa pm uwezekano wa kupata mashamba. Imeniwia vigumu sana namba kuweka namba yangu hadharani, ukizingatia watu wengi mnatumia majina ya kuchonga.
 
Hongereni sana sana wakuu! Mimi pia ni mdau mpya wa kilimo huu mwaka wa 3 sasa. Kwakweli nilisukumwa na manyanyaso ya ajira kama kubota alivyoeleza hapo awali.
Nilikua na vihela kiasi nikanunua mashamba kwa hasira. Nina shamba ruaha mbuyuni, bwawani, kilolo na tanangozi.
Kikweli niliingia kwa nguvu na kupanda vitu vingi kutokana na ushauri wa watu.
Mh wadau kuvuna nilivuna ila kutokana na kukosa usimamizi wa kuaminika niliibiwa kidogo nichanganyikiwe.
Watu ni wezi ajabu! Yani unapigwa mpaka unajiuliza kama aliekufanyia ivyo ni binadamu au.
Hivyo kwa sasa nimeamua kuanza shamba 1 kwanza pole pole ambalo ninasimamia kiurahisi.
Shamba la eka 100 nimetenga eka 60 za kupanda miti. Kila mwaka napanda pines na eukalyptus eka 8. nimepanda eka 16 mpaka mwaka jana.
Kwenye upandaji wa miti natumia mbolea, aisee miti inakua haraka ajabu, nashauri kwa yoyote anaepanda miti atumie mbolea. Nasubiri mwaka wa 4 insha Allah niongee na wadau kupata hela za hewa makaa.
Eka 20 nimeweka ajili ya kulima mahindi,maharage,njegere na alizeti. Kuna nyanya na mboga mboga lakini hizi ni kwa ajili ya vijana wa shamba na nyumbani.
Pia nina kuku kiasi na kondoo. Nafkiri kabla ya mwisho wa mwaka nafkir kuongeza ngombe.
Eka 20 zingine ni pori nitaenda nalo mdogo mdogo.

Takribani kilomita 10 kutoka shamba langu kuna mzungu alitokea zimbabwe ana shamba lake. Wakuu mkienda kuona hamtaamini mko Tanzania! Niliangalioa lile shamba nikajiuliza sana sisi waswahili tunashindwa nn. Jamaa wana kuku,kondoo na ngombe utafkiri siafu! Wanapeleka mayai dar na south africa na kuprocess beef na lamb into sausages and other products for export.
Maisha yako relaxed na wanahela za kutosha!
Nikawaza nyamgluu na tudegree twangu nahangaishana na mwajiri kwa peanut salary kweli nikiamua kutulia kwa kilimo ntashindwa? Wakati watu wanaongezeka kila siku na kila wakila lazma waende choo na kesho wale tena!
Kuna wadau hapa JF tunasaidiana sana mawazo katika PM, nashukuru sana na tuendelee kuwa pamoja.
 
mitiki nimepanda hekari 8. Nina progranu ya kupanda hekari 5 Kay zaidi kila mwaka. Kwa mfano shamba lingune nilishanunua ambalo hekari tano zitapandwa mitiki mwakani.

Hili eneo lako lipo umbali gani toka Msamvu?
 
Mkuu kuhusu hali ya hewa ambayo mitiki inakubali hilo siwezi nikakupa jibu sahihi sana. Ila nifaamuvyo mimi ni kuwa mitiki inakubali sana sehemu za baridi. Hata sehemu za joto Kama Morogoro inakubali pia. Dar na pwani mitiki inaweza kukubari vizuri sana.Ukame ule Kama wa singida, Dodoma na shinyanga siyo mzuri Kwa maendeleo ya mitiki kwani itakufa Kwa kukosa maji. Haipendi sana sehemu yenye unyevu wa kupitiliza. Hapa morogoro Miti ya mitiki hulimwa sana mahenge , kilombero mvomero- hasa turiani na Iringa wameanza kulima Kwa kasi.

Soko la mitiki like wazi kabisa. Heka moja unaweza kutengeneza hadi 120 millions Tsh. Pia ukiwa na heka mbili za mitiki zenye umri wa miaka miwili unaweza ukaenda bank na kuvuta mkopo hadi sh 50 milioni. Ni akiba nzuri uzeeni( pension yako). Mimi ,nimejipangia kila mwaka kupanda si chini ya hekari tano za mitiki.

Naomba wanaofahamu zaidi mazingira na faida ya mitiki wanisaidie Katika kumwelimisha huyu ndugu.

Mimi naweza nikakuuzia miche ya mitiki Kwa sh 300 Kwa mche.

Mkuu,hivi kwa heka moja nikitaka kupanda mitiki,kitaalam nitahitaji miche mingapi?na ilo la kua teak ikifikisha miaka miwili unaweza pewa mkopo,je ni kwa kuanzia heka mbili na kuendelea au hata kwa heka moja?na mwisho mkuu,je hiyo mikopo masharti yake ni yapi,kuna mikoa maalum iliyochaguliwa au ni popote Tanzania?
 
unaajiriwa kwa muda wa miaka 30 unapata pension lets say ya shs mil 40,wakati ukijipanga ktk ujasiriamali utahangaika mwaka mmoja wa kujiestablish,40 mil can be generated on year,bravo eberhard.

Hii nimeipenda, so so true.
 
Hongereni sana sana wakuu! Mimi pia ni mdau mpya wa kilimo huu mwaka wa 3 sasa. Kwakweli nilisukumwa na manyanyaso ya ajira kama kubota alivyoeleza hapo awali.
Nilikua na vihela kiasi nikanunua mashamba kwa hasira. Nina shamba ruaha mbuyuni, bwawani, kilolo na tanangozi.
Kikweli niliingia kwa nguvu na kupanda vitu vingi kutokana na ushauri wa watu.
Mh wadau kuvuna nilivuna ila kutokana na kukosa usimamizi wa kuaminika niliibiwa kidogo nichanganyikiwe.
Watu ni wezi ajabu! Yani unapigwa mpaka unajiuliza kama aliekufanyia ivyo ni binadamu au.
Hivyo kwa sasa nimeamua kuanza shamba 1 kwanza pole pole ambalo ninasimamia kiurahisi.
Shamba la eka 100 nimetenga eka 60 za kupanda miti. Kila mwaka napanda pines na eukalyptus eka 8. nimepanda eka 16 mpaka mwaka jana.
Kwenye upandaji wa miti natumia mbolea, aisee miti inakua haraka ajabu, nashauri kwa yoyote anaepanda miti atumie mbolea. Nasubiri mwaka wa 4 insha Allah niongee na wadau kupata hela za hewa makaa.
Eka 20 nimeweka ajili ya kulima mahindi,maharage,njegere na alizeti. Kuna nyanya na mboga mboga lakini hizi ni kwa ajili ya vijana wa shamba na nyumbani.
Pia nina kuku kiasi na kondoo. Nafkiri kabla ya mwisho wa mwaka nafkir kuongeza ngombe.
Eka 20 zingine ni pori nitaenda nalo mdogo mdogo.

Takribani kilomita 10 kutoka shamba langu kuna mzungu alitokea zimbabwe ana shamba lake. Wakuu mkienda kuona hamtaamini mko Tanzania! Niliangalioa lile shamba nikajiuliza sana sisi waswahili tunashindwa nn. Jamaa wana kuku,kondoo na ngombe utafkiri siafu! Wanapeleka mayai dar na south africa na kuprocess beef na lamb into sausages and other products for export.
Maisha yako relaxed na wanahela za kutosha!
Nikawaza nyamgluu na tudegree twangu nahangaishana na mwajiri kwa peanut salary kweli nikiamua kutulia kwa kilimo ntashindwa? Wakati watu wanaongezeka kila siku na kila wakila lazma waende choo na kesho wale tena!
Kuna wadau hapa JF tunasaidiana sana mawazo katika PM, nashukuru sana na tuendelee kuwa pamoja.
mkuu nimeipenda hii nitakupm unipe ushauri, i will appreciate that.
 
Hongera sana Eberhard,
mi pia ni mdau, nilianza mwaka juzi kwa kununua mashamba, so far nimeshapanda mitiki huko mkoa wa pwani na pines huko iringa, miti yote inaendelea vizuri, nategemea 5 years from now nitaanza kuvuna. Pia nina mpango wa kuweka mifugo kama kuku na mbuzi na kulima mbogamboga by next year. Biashara ya upandaji miti ni nzuri sana hasa kwa wale waajiriwa kwani ahiitaji usimamizi wa karibu sana.
kwakweli inafurahisha sana kuona kumbe WATZ tunaweza tengeneza pesa nyingi tu bila kula rushwa. all the best
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom