ngumbuke
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 495
- 527
Kaka ninaendelea kufuatilia topic yako, inazidi kunifungua masikio na macho. Sawa na maneno " wana masikio hawatasikia wana macho hawataona" Ninamtukuza Mungu kwa ajili hili jukwaa na kukutuma ww uwe mlango wa wengine kupitia.. Shamba sijaliwekea Uzio mkuu. Bado nipo kwenye phase I .Katika phase hii kuna ni mradi wa kujenga mabada ya kuchukua nguruwe zaidi ya 1000. Maximum itakuwa 2,000. Phase hii itahusisha ujenzi wa mazingira ya kusaport kuku wasiopungua 40,000.
Phase II
ni ujenzi wa fance kuzungushia shamba langu lote. Hii hiyo itanichukua muda kidogo.
phase III
Ni kubadili vibanda vilivyopo na kujenga nyumba za kudumu za kuishi.
Hivyo sasa kuna nyumba ndogo ya udongo na bati anayoishi mfanyakazi wangu na mke wake. Pia kuna nyumba nyingine ya nyasi inayosubiri mtu wa kuishi. Kwa sasa Mimi naishi mjini nikitafuta pesa za kusapoti mradi kwani bado haujiendeshi. Baadaye nina mpango wa kufanya makazi huko.
Gharama za ujenzi bado napambana nazo. Ujenzi unaendelea. Bado haujakamilika.
Sidhani kama tunaojipanga kuanzisha miradi hii by january yutakuwa tumechelewa.
Kaka ninakusihi usituache hewani kwani elimu unayotuachia ni kubwa mno hasa kwetu sisi tulio kwenye ajira za kitanzania.
Endelea kutulisha sawa na haja za mipango yetu na Mungu azidi kukubariki!