Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Hongera sana mkuu Eberhard nimefuatilia post zote Mungu akupe zaid na usiache kutupa updates zaid
 
Last edited by a moderator:
Jaman naomba kuulza mitiki ndio mimea gani na inafaida gani, kazi zake hali kadhalika, nashukuru kwa ushirikiano wenu
 
naomba kuuliza. mabanda ya nguruwe ni muhimu kua na umeme? na mpk kuuzwa nguruwe mzima anakua na kilo kati ya ngap kwa kukadiria
siyo lazima kuwa na umeme. Mimi pia sina umeme.
 
Baada ya kumaliza degree yangu ya pili na kuona kuwa ajira kama ajira haiwezi kuwa mkombozi wangu kiuchumi niliamua nifatilie mawazo mbalimbali ya ujasiriamali. Nikafikiria ujasiriamali wa kiubunifu wa hali ya juu ndiyo utakuwa mkomnozi wangu kiuchumi. Nimeanza Kwa kununua shamba lenye ukubwa wa hekari 12 nje kidogo ya mji wa Morogoro ( Kwamakunganya-majichumvu). Sehemu kubwa ya shamba langu nimepanda mitiki.

Baada ya kufatilia humu nikagundua kuwa mradi wa nguruwe na kuku wanalipa sana. Ninaomba kukili kwamba miongoni mwa post ambayo serious nilihaidi kuifanyia kazi ni Anza hivi mpwa wangu. Kwa kuwa imani yangu inaniruhusu nikaona ni laziima niifanya hii ya Anza hivi mpwa wangu. Hivyo nikaanza maandalizi ya kufuga nguruwe na kuku pia. Hivyo nilianza Kwa kuanzia kuchimba na kujengea tangi la maji chini. Ilichukua Muda wa miezi miwili tangu langu la maji kukamilika. Tangi langu la maji Lina uweze wa kujaza maji lita 30 elfu.

Baada ya hapo nikaanza maandalizi ya ujenzi wa banda la nguruwe na la kuku. Baada ya mabanda yangu kukamiliaka nilisafiri hadi singida kufata kuku. Bei ya kuku singida inalidhisha sana. Ili upate kuku wa bei rahisi inakupasa uende vijijini ambako kuku huuzwa cheap. Hivyo nilisafiri hadi kijijini ambako nililinunua kuku 31 ambao ndiyo nimeanza nao.. Kwa upande wa nguruwe nimeanza na 12 ambao niliwanunua wakiwa na miezi mitano. Pia nimeweka kanga na mbuzi Kwa ushauri wa marafiki.

Ninashukuru Mungu ninaanza kuwaona kuku wameanza kutaga Kwa fujo. Pia ninamshukuru Mungu Kwa kuwa ninaona ninaanza kuwa muajili pole pole. Pia ninamshukuru Mungu ninaona mawazo ya kunyanyasika( kuajiliwa) yanaanza kupotea taratibu.Kwa sasa nguruwe wangu wameshabeba mimba hivyo nategemea kuanza kuona mabanda yangu yakijaa vitoto vya nguruwe hivi punde.
Kupitia uzi wangu huu nitakuwa nawataarifu maendeleo ya mifugo yangu Kama sehemu ya kuwatia moyo wajasiriamali wenzangu. Morogoro ni sehemu ambayo wajasiriamali mnaweza kutimiza ndoto zenu Kwa kuwa Ardhi inapatikana Kwa bei nafuu na ni Karibu na Dar kwenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali.
Mimi nikupe pongezi kwa kufanya kazi yenye tija. mana hatua moja huanzisha nyingine, hapo utapata mawazo mapya ya kuimprove project yako. Ila sina uzoefu sana na faida ya kufuga kuku wa asili ambao si "chotara". kwakuwa hawa chotara wanakuwa na uzito mzuri wakishafikisha miezi sita na kuanza kutaga pia.
 
Kaka Eberhard hongera kwa hatua ulizopiga mpka sasa,,,, Mungu akupe nguvu na akili ya kuweza kupambana na challenges za apa na pale,,,
Pili nilikuwa naomba ur dials maana nilikuwa nataka kujifunza meng kutoka kwako
 
Asante. Tuko pamoja.
 
Kaka Eberhard nami kama kijana mwenzio nikupe hongera sana kwa mafanikio hayo uliyopiga umeniispire sana na hichi ulichokifanya nami nashawishika kuondoa uoga kwenye malengo yangu kwakua na mimi nina tagert ya kufanya biashara ya kilimo but naomba nikuulize kitu mtaji imekua ni tatizo kwa vijana wengi hapa tz kujitosa katika biashara je wewe mwenzetu mtaji wa kuanzisha hii project uliutoa wapi mana kwa mtizamo wa haraka haraka si chini ya milioni kadhaaa zimeshatumika hadi hapo!! Ni hayo tu mkuu, asante
 
Mtaji Niliutoa kichwani. Brain yangu ni super brain. Mimi naamini katika mawazo. Huwa naanza kuwaza kisha mawazo yangu ndiyo yananiletea pesa. Kitu kikubwa ni kutokuwa na haraka. Nenda taratibu. Ukishakuwa na wazo na kulioganize sawasawa ndipo anza kufikiria pesa. Katika kufikiria unaweza kupata point ya kuanza nayo. Katika nchi hii kuna maeneo ambayo unaweza kupata hekari ya ardhi kwa sh 50,000/- Tafuta mazingira yanayofanana na na mtaji wako siyo vyema kung`ang'ania kufuga kuku masaki wakati kipato chako hakikuwezeshi kuanzisha ufugani mkubwa pale. Tafuta mazingira sahihi.
 
Nashukuru sana mkuu Eberhard kwa kuweza kupata muda wa kujibu swali langu kwani najua unashughuli nyingi kwa sasa lakini nilikua na swali la nyongeza kidogo, mkuu kwenye majibu yako hapo kwenye swali la msingi haujanifafanulia clearly je, mtaji ulikopa benki? Ulidudunduliza kidogo kidogo au uliazima pesa kwa ndugu jamaa na marafiki? Naomba tusaidie hapo mana wengine tumekwama hapo japo tunamawazo mazuri sana!! Asante
 
Genius., My ways are not ua ways. We may not give you fish but we shall tell you how to catch fish from the river. I shall never tell u where I got money till I know you physically. We do not give you notes but we shall teach you how to make your own good notes. It is my hope that you are going to make best notes. We believe that u are good so we advise you so ua becoming better.
 
Mi nadhani huu Uzi ungeendelea coz umetusaidia wengi Jamani kubadilisha fikra zetu..hongera sana Mkuu Eberhard..!
 
Back
Top Bottom