Stoudemire
JF-Expert Member
- Mar 24, 2012
- 839
- 207
Pole sana mkuu yaani panya ni balaa hata paka pia, mimi ndo maana huwa naona bora nipande miti ya vivuli kama sina uwezo wa ukuta nijenge full suti ya mabati na madirisha ya wavu makubwa kupitisha hewa. Panya wanakula chakula pia wanaleta magonjwa. Hapa Kubota alielezea mbinu ya kufukia ndoo kwenye maeneo unayoona wanapenda kutembelea nje ya banda nadhani na wewe fukia ndoo yenye maji jirani na hilo shimo na kwingine. Hebu msome tena kwenye ile thread. Halafu angalia chakula chao hadi wiki ya 4 ni starter halafu unahamia finisher hadi wawe vinyoya wakubwa. Mungu akutie nguvu.
Nilitaka kumshauri aweke mapaka shume ili yaende sambamba na hao panya kumbe paka nao anakula hao kuku?