Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Pole sana mkuu yaani panya ni balaa hata paka pia, mimi ndo maana huwa naona bora nipande miti ya vivuli kama sina uwezo wa ukuta nijenge full suti ya mabati na madirisha ya wavu makubwa kupitisha hewa. Panya wanakula chakula pia wanaleta magonjwa. Hapa Kubota alielezea mbinu ya kufukia ndoo kwenye maeneo unayoona wanapenda kutembelea nje ya banda nadhani na wewe fukia ndoo yenye maji jirani na hilo shimo na kwingine. Hebu msome tena kwenye ile thread. Halafu angalia chakula chao hadi wiki ya 4 ni starter halafu unahamia finisher hadi wawe vinyoya wakubwa. Mungu akutie nguvu.

Nilitaka kumshauri aweke mapaka shume ili yaende sambamba na hao panya kumbe paka nao anakula hao kuku?
 
Mmmm siku nyingi sijalutana na paka amekamata panya. Mimi paka wa nje uko ukisahau mlango wa banda wanapiga kucha vifaranga au kuwala, waweza kuta hadi 8 wameumizwa. Wakati ukiacha chakula ovyo panya wanahamia. Ufugaji ni kuwa alert ukitubu ugonjwa unakutana na paka, panya, ukivuka vyote soko lakini ktk yote mwisho faida hukosi ni mitihani tu.
Nilitaka kumshauri aweke mapaka shume ili yaende sambamba na hao panya kumbe paka nao anakula hao kuku?
 
fafanua,wanakufa kwa ugonjwa au wanashambuliwa na hao panya?
Vifo vya ugonjwa nimeanza kuvizuia. Vifo vya sasa vinasababishwa na panya.vifaranga 8 vilivyotoka jana 6 vimeliwa. Kwa sasa tunajaribu kutengeneza kijumba kidogo cha waya wa fance ili tuwafunike. Fance hiyo ni ile ndogo ambazo panya hawawezi kupita. Kama nikifanikisha hilo nitarudi kwenu kwa mlejesho. Kama una kazi wazo lolote la ziada kunisaidia mkuu.
 
Kwa sasa kuku wangu wanaendelea kutaga kwa spidi inayonifanya niamini kuwa ni kwa uwezo wa aliye juu tu. pia wameanza kutotoa. Hata kama kwa kuuza mayai tu sasa nitaweza kumlipa mfanyakazi. Nawakaribisha sana vijana wenzangu kwenye ufugaji. Kama mnazitaka Mali ni kweli mtazipata shambani. Tusiangalie ukubwa wa ELIMU yetu bali tuangalie namna tunavyoweza kujikomboa kiuchumi pasipo kupiga kelele kwa seikali kwamba haiongezi mishahara. Pia kwa waliokosa ELIMU hakuna haja ya kujiona wanyonge karibuni tuje tufuge. Mungu aliye juu atatubariki na kutujaza zaidi ya shetani anavyowajaza wezi wa kutumia karamu.

hongera Mkuu kwa yote na kutupa moyo kumbe inawezekana.
Inaonyesha shamba lako ni nje ya mji,swali ni je unaishi hapo hapo kwenye shughuli zako za ufugaji ama umejenga kibanda kwa ajili ya mtu kusimamia shuhuli hizo?na ulinzi inakuaje maeneo kama hayo
 
Ninamshukuru Mungu kwamba leo sijapokea taarifa ya vifo vitokanavyo na panya. kijumba cha wavu wa waya tulichokijenga na kuwafunika vifaranga kimesaidia sana. Hali ikiendelea hivi panya watakuwa wanawasikia sauti tu za vifaranga wangu wakifurahi ndani ya nyavu huku wakiendelea na misosi. Hakika panya walikuwa wananinyima usingizi. Nitawawekea picha ya kijumba changu cha vifaranga ili na nyinyi mjifunze mbinu hiyo. Tupo pamoja wajasiriamali. Mungu ni mwema siku zote.
 
Safi sana mkuu, hiyo ndo Swaga yeyewe, na unachosema ni kweli Kuajiriwa ni utumwa wa hali ya juu kabisa na husababiha hadi kilema cha ubongo, hakuna jambo baya kama kukaa kusubili mwisho wa mwezi au kuwa chini ya himaya ya mtu mwingine,

Wewe pambana tu hakuna kisicho wezekana chini ya Jua

Chasha mimi kilichonikera sana kwenye kuajiriwa mpaka kufikia kuuona ni utumwa ni ile hali ya expenditure yangu kudhibitiwa na mtu mwingine. Hata kwenye ajira binafsi expenditure iko controlled lakini i love the difference: that i am now the controller. na hakuna kitu kilikuwa kinaniboa kama mambo ya likizo!! leave request hapana aisee. mbaya zaidi sisi wengine tunataka tufanye kazi vizuri, ionekane mwisho wa mwezi ule chako sasa hukohuko mko na watu wanawaza wizi tu kwenye procurements! this put me off to no end. kazi haziendi kutwa kufatilia madili.

Kwahiyo mkuu Eberhard nakupongeza sana, umechagua jema sana, na hutojuta. we kaza tu. kwanza umeni inspire sana. Mjasiriamali wa kweli utamjua tu(matumizi mazuri ya eneo)
 
Ndoto zangu wewe umezitimiza, ila ipo one day nitakutafuta kaka kwa ushauri wa ana kwa ana. Ongera sana
 
Tuko pamoja wakuu. Pale juu nimewaongezea picha za mwendelezo wa utanuzi wa banda langu la nguruwe na namna navyowalinda vifaranga vya kuku wangu na panya kwa kutumia wavu.
 
Miongoni mwa siku ambazo najivunia kuwa mwanachama wa JF ni leo!

Nikiri kuwa nimepata shule ya maana sana kwa leo, nina eneo la takribani ekari 12 mpango ilikuwa ni kuligawa.

•Ekari 2 mazao ya chakula, yaani kuhakikisha kuwa ndani ya mwaka mmoja sinunui mahindi wala maharage kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya chakula, ziada nauza kwa ajili ya kununua aina nyingine za vyakula.

• Ekari 5 kuzipanda mananasi, kila ekari inaingia karibu miche 3500 nanasi halina tabu sana kwenye kulilea, likiwa tayari unauza ukiwa shamba moja kwa sh 550/ ukipeleka mwenyewe sokoni ni sh 1000/= Hesabu inakuwa hivi miche, 3500 kwa hekari moja mara 5 = 17500, chukulia umepata mananasi 17000 mara 550 (ukiuuzia shamba) = 9,350,000/= (Mananasi si zaidi ya miezi 11).

• Ekari 3 natupia mitiki hakiba ya baadae kwa ajili ya makamanda wangu 2, wakifikisha miaka 20 itakuwa tayari kuvuna.

• Mifugo ekari 1, kipaumbele ni kuku, mbuzi na ng'ombe. Sasa hivi ukiwa na ng'ombe 4 ulio walisha vizuri kima cha chini ukiwauza wote ni karibu 1.6M, hapo bado kuku, na mbuzi.

Mpango ni kuwa na hekari 40 kabla ya kufikisha 35

Kama mnataka mali mtayapata shambani
 
Tuko pamoja wakuu. Pale juu nimewaongezea picha za mwendelezo wa utanuzi wa banda langu la nguruwe na namna navyowalinda vifaranga vya kuku wangu na panya kwa kutumia wavu.

vp kule ndani kabisa kama mwendo wa dak 20 kwa bodaboda hakuna matatizo ya kuuziana mashamba? kuna mtu ana eka kama 20 anataka kuniuzia shamba ambalo limekatwa visiki ila havijang'olewa. nasikia kuna watu wanalima ufuta, alizeti, na matikiti vipi hayo mazao yanakubali kweli au wanafanya kul
azimisha?
 
Mazao yote uliyoyataja yanakubali sana huko. Usinunue shamba bila kumuona mwenyekiti wa majichumvi anaitwa mzee mayala. Yeye ana database ya maeneo yote. Naamini umenipata vinginevyo unaweza ukapata hasara.
 
Miongoni mwa siku ambazo najivunia kuwa mwanachama wa JF ni leo!

Nikiri kuwa nimepata shule ya maana sana kwa leo, nina eneo la takribani ekari 12 mpango ilikuwa ni kuligawa.

•Ekari 2 mazao ya chakula, yaani kuhakikisha kuwa ndani ya mwaka mmoja sinunui mahindi wala maharage kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya chakula, ziada nauza kwa ajili ya kununua aina nyingine za vyakula.

• Ekari 5 kuzipanda mananasi, kila ekari inaingia karibu miche 3500 nanasi halina tabu sana kwenye kulilea, likiwa tayari unauza ukiwa shamba moja kwa sh 550/ ukipeleka mwenyewe sokoni ni sh 1000/= Hesabu inakuwa hivi miche, 3500 kwa hekari moja mara 5 = 17500, chukulia umepata mananasi 17000 mara 550 (ukiuuzia shamba) = 9,350,000/= (Mananasi si zaidi ya miezi 11).

• Ekari 3 natupia mitiki hakiba ya baadae kwa ajili ya makamanda wangu 2, wakifikisha miaka 20 itakuwa tayari kuvuna.

• Mifugo ekari 1, kipaumbele ni kuku, mbuzi na ng'ombe. Sasa hivi ukiwa na ng'ombe 4 ulio walisha vizuri kima cha chini ukiwauza wote ni karibu 1.6M, hapo bado kuku, na mbuzi.

Mpango ni kuwa na hekari 40 kabla ya kufikisha 35
Aisee mitiki panda mbali na mazao ya chakula ,inashauriwa hivyo. Inataka maji mengi pia inatengeneza sumu inayoua mimea mingine karibu yake, ivyo usiweke karibu na mazao ya chakula wala miti mingine.
 
Mkuu hongera sana mwanzo mzuri
nami nataka kuwa na wazo kama lako unanishaurije nianzeje
maana nimechoka na kuajiriwa
mie naona kama mtoa mada ameeleza kila kitu cha muhimu kinachotakiwa kwako ni kuedit kutokana na mazingira, na mtaji ulio nao pia na eneo unaloishi
 
vp kule ndani kabisa kama mwendo wa dak 20 kwa bodaboda hakuna matatizo ya kuuziana mashamba? kuna mtu ana eka kama 20 anataka kuniuzia shamba ambalo limekatwa visiki ila havijang'olewa. nasikia kuna watu wanalima ufuta, alizeti, na matikiti vipi hayo mazao yanakubali kweli au wanafanya kul
azimisha?

Gwe Mponji bikoolesya ilenga emigunda egyo. Ngonyonywa nkamu!
Hongera mkuu kwa kukata shauri.
Juzi nilikuwa bagamoyo maeneo ya Mbwawa kwenye bonde la mto Ruvu. Actually ni maeneo mazuri.Wakati wao wanazungumza BRN kisiasa acha sisi tujipange.
 
Back
Top Bottom