Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Hii si siri tena.
NCCR Mageuzi ni kama imeshakufa Kigoma. Mtu pekee ambaye pengine alionekana anaweza kuwakilisha chama hicho kwenye Dunia ya Mawese Ni David Kafulila. Amefanya majaribio kadhaa kuhakikisha anarudi mjengoni lakini amekwama. Sasa analia, kutweta na kusaga meno. Ubunge kaukosa. Kilichobaki ni kulea mtoto.
Hata hivyo, taarifa za ndani zinasema kuwa Mwanasiasa huyo kijana na machachari ambaye alitikisa hapo nyuma kwenye sakata la ESCROW Akaunti kwa sasa anajiandaa kutimikia CHADEMA. Mazungumzo yanaendelea vema chini ya ushawishi wa Kada wa CHADEMA, Malisa Godlisten Joseph.
Taarifa zinasema kuwa Malisa na Kafulila ambaye alibatizwa jina la 'Tumbili' wameshakaa vikao kadhaa na kuna mambo wameafikiana. Hata hivyo kuna jambo moja ambalo ndilo kiini na masharti ya Kafulila kuhamia CHADEMA. Kama litafanikiwa basi njia nyeupe kuhamia Ufipa. Jambo hilo ni uwezeshwaji kifedha. Kafulila anataka alipwe kiasi cha shilingi milioni 5 kwa Mwezi kwa kipindi chote ambacho amekosa ubunge. Kwamba, kiasi hicho kitamsaidia kujenga utulivu wa kiakili na hivyo kupata fursa ya kutosha kukitumikia chama chake kipya, CHADEMA kwa masharti kuwa mkoa wa Kigoma uwe na wabunge wa CHADEMA angalau 2 kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020.
Je masharti hayo CHADEMA watatekeleza? Na je kama watatekeleza, Kafulila ataweza kupambana na CCM na ACT ambao wameshaweka mizizi kwenye mkoa huo? Tusubiri na tuone.