KERO Baada ya kuanza kwa safari za SGR, hizi ni changamoto zake zilizojitokeza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mimi nikafikri unaripoti kama ulivyoona kumbe na wewe ni vya kusimuliwa!
 
Kama kawaida ya maccm watauza hii reli Watampa dp word kwa mikataba ya kifisadi muda si mrefu wakisingizia serikali haiwezi kuhudumia

Swali ni je kabla ya kuanza kwa mrdi walijipanga kuendesha kwa ufanisi na faida ukikamilika?
 
Huo mfumo wa tiketi tunaufanyia timing tuuhujumu kama ule wa BRT ili tuibe vizuri. Sisi ndio Watanzania na jasiri haachi asili.
 
Sasa ndio kwanza treni imefanya safari moja wakuu kweli mnataka kusiwe na changamoto yoyote kweli?

Unawalaumu hao wahudumu hawana uzoefu, like serious mkuu?
Mkuu CHADEMA imetuletea taifa la hovyo kabisa! Yaani wao kila kitu ni pinga pinga tu! Hapa Magu apewe maua yake kwa kweli. Sasa wanataka waingie na viroba ndani ya SGR utafkri Waha wanatoka stesheni ya Kigoma!
 
Kila Mtanzania anataka huduma perfect kwa ajili yake.jambo ambalo haliwezekani. Mapungufu ya hapa na pale hayakosekani.
Kama ni kweli wameuza siti moja kwa watu wawili wote wakawa na ticketi inayofanana namba; SIO TATIZO LA KUPUUZIA, tuacheni ubabaishaji kwenye mambo ya msingi. Kwanza ni kuleta usumbufu mkubwa kwa abiria, lakini pia ni wizi kwa kuwa ticketi moja inakuwa haifahamiki/haihesabiki
Hapo kuna uzoefu gani unatakiwa? wakati wa majaribio ndio ulikuwa wakucheki hivyo vitu....
 
hakika umenena jambo muhimu. Tusingumzie huko tu . Karibia kila mahali customer care ni zero. Mimi naona watanzania hatuuelewi msemo wa MTEJA NI MFALME VIZURI. yaani inabidi kabisa ikiwezekana iwepo compaign ya customer care mtaa kwa mtaa. Tunapoteza na kufukuza wateja kila mara Kwa sababu ya lugha chafu na kutojali huduma tunayotoaaa. ILA KWA WATU WANAOJITAHIDI TUWAPE MAUA YAO PIA AMBAO NI BARBERSHOP 👏👏👏👏
 
Kwanini haya tusichukulie kama mapendekezo kwa ajili ya maboresho? Ili tutende haki,inabidi tuwape muda fulani.

Majibu tunayo ya nini kitatokea,maana tuna uzoefu na biashara za serikali,lakini, tusiwape sababu ya kujitetea. Ni mapema mno kuwawashia moto.
 
Boda boda ni mtaji wa wanasiasa kutoka pande zote. Kila mtu anaogopa wagusa
 
😂😂😂 Yaani sisi wabongo tumekalia kuangalia madhaifu tu kuliko maeneo yaliyopatiwa sasa trip moja tu kasoro nyingi sana kitu ambacho ni lazima hayo kutokea
 
Ni kweli ila wahudumiwa nao wapo ambao ni kisanga
Nmeshuhudia hili last weekend abiria anataka abend siti ya basi ilhali nyuma amekaa mjamzito
Au haya mabasi luxury ya kwenda mikoani, utakuta bus lina A/C na madirisha yamefungwa ili kuzuia ubaridi usitoke nje, abiria anafungua madirisha makusudi ili aweze kutema mate na kupunga upepo......Jamii ya Watanzania ni washamba mno na tuna mengi ya kujifunza kwa kweli.
 
Mkuu Jamaa Mbishi , sasa ateme wapi mate ?? ndani ya basi ??
 
Hakuna mbongo aliyekamatwa akinya hadharani kweli au kujaribu kuvunja vioo vya behewa makusudi?
 
Salama ya SGR ni kupewa mwekezaji. Inaweza kwenda kama mabasi ya mwendo kasi. Tunajijua wenyewe akili zetu zilivyo
 
Nimo kwenye treni ya SGR kila anayeongea na simu lazima aseme niko kwenye treni ya SGR, ni kama sisi sote tumekuwa chawa wa hii treni
 
Suala la ticketing system ni la muda, kuanzia kwenye testing, walifanyie kazi lifikie internation standards maana mradi kama huo haiwezekani ukwa na ticketing system mbovu kiasi hiko
 
Kila Mtanzania anataka huduma perfect kwa ajili yake.jambo ambalo haliwezekani. Mapungufu ya hapa na pale hayakosekani.
Hilo la boda Boda vituoni wawekewe utaratibu mzuri.
 
Subirini mvua na wamachinga treni pindi umeme ukikatika mtauziwa power bank mpaka mtakoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…