Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Iko hivi, nchi hii ili uwe mwizi na fisadi mwenye mafanikio basi ni lazima uwe na mafungamano na chama tawala na serikali yake. Yaani kama uko nje ya mfumo basi hakikisha unakula vizuri na walio ndani, wape 10% zao.
Vigogo wa chama na serikali ndio wamehodhi biashara zote kubwa kubwa, na wanafanya biashara hizo kwa njia zisizo halali.
Imagine wewe ni afisa wa serikali unapigiwa simu kuwa huo ni mzigo wa mheshimiwa fulani fanya wepesi. Ukileta ubishi basi kesho unajikuta umepigwa uhamisho kwenda chakechake huko. Anayekuja kuchukua nafasi yako lazima akae kwenye mstari!
Haya ni matokeo ya asili ya historia yetu ya mfumo wa kidikteta wa chama kimoja. Kwenye nchi zote zenye mifumo hiyo basi rushwa, ufisadi na wizi huwa unafanywa na vigogo wa chama na serikali. Mifano hai kwa sasa ni China na Urusi, mafisadi wao ni vigogo serikalini kama sisi huku.
Baada ya mzalendo JPM kuingia magogoni, kwanza alijaribu kupambana na wezi hao huko huko ndani ya chama, lakini baadae alishauliwa kwa usahihi kabisa kuwa ili kuivunja network ya waandamizi wezi basi ni lazima ajenge CCM mpya kabisa.
Na alitaka kuwavuta wazalendo kutoka nyanja zote kama vile vyama vya upinzani, taasisi za elimu ya juu, vyombo vya ulinzi na usalama N.K ili kuumaliza kabisa ule mfumo wa zamani.
Mwisho wa siku aliangushwa na watu ambao hakutarajia wangemwangusha, vyama vya upinzani! Kundi hili lilitumiwa na wana mtandao kuhujumu juhudu za JPM tena wengi wao bila hata ya wenyewe kujua.
Mwisho wa siku tuko hapa tulipo. Ndugu zangu wa upinzani ukiwemo Tundu Lissu haya mliyataka wenyewe. Natumaini mioyo yenu imejaa furaha namna nchi inavyoendeshwa kwa sasa.