Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

[
Mkuu heshima kwako

Napata wasiwasi mkubwa sana kuhusu maelezo yako, unasema baada ya kufika Moscow leo sijajua leo unaamanisha leo 15th November au lini??

Pili umemtaja Elibariki Dishon kama Mtanzania aliyekupokea hilo pia linatia shaka kwa sababu zifuatazo. Mimi ninaishi Moscow na nina familia na tuna umoja wa Tanzania hapa ( Diaspora) na jina hilo ulilitaja sijawahi kulisikia labda kama huyo Elibariki amekuja Moscow mwezi uliopita.

Pili Dr baada ya kupatwa na masaibu ya kukatwa vidole alikimbilia ubalozi wa Tanzania Moscow, kipindi balozi akiwa Patric Chokala na alisaidiwa kuondoka, naweza kukutajia hata mtu aliyempeleka uwanja wa ndege( na ahata ubalozi haukuwahi kujua sababu ya masaibu yake) ila kwa ufupi ilionekana ana matatizo ya afya ya akili.

Kwa wanaojua utaratibu wa address za Russia utaona shaka kabisa na address za hiyo kampuni

Kama uko Moscow ingia inbox nikakuribishe kwangu tuzungumze

Kwa hili la dr shika ni kweli kabisa...huyu mzee ni hatar tupu..movie aliyoicheza kwenye mnada mzito kama ule alafu akaibuka kinara na talk of the day inadhihirisha huyu mtu sio wa kawaida..hata bunge anaweza lipua huyu
 
Dr Shika nilivokuwa namfikiria kaniprove wrong kabisa baada ya kufatilia story yake hasa kwenye mitandao ambayo ni mahojiano ya ana kwa ana mzee ni mkweli na hana chembechembe za ubabaishaji ...very smart anajua anachokiongea na ndo kimenifanya niamini maneno yake ....

All in all i can sum up "ni maisha " tu kuchange ndo kumemfikisha hapo alipo

Respect to you Dr Shika
Ni kweli mkuu anaongea anachokiamini. hana chembechembe za uongo, mungu amsimamie afanikishe mpunga wake.
 
[
Mkuu heshima kwako

Napata wasiwasi mkubwa sana kuhusu maelezo yako, unasema baada ya kufika Moscow leo sijajua leo unaamanisha leo 15th November au lini??

Pili umemtaja Elibariki Dishon kama Mtanzania aliyekupokea hilo pia linatia shaka kwa sababu zifuatazo. Mimi ninaishi Moscow na nina familia na tuna umoja wa Tanzania hapa ( Diaspora) na jina hilo ulilitaja sijawahi kulisikia labda kama huyo Elibariki amekuja Moscow mwezi uliopita.

Pili Dr baada ya kupatwa na masaibu ya kukatwa vidole alikimbilia ubalozi wa Tanzania Moscow, kipindi balozi akiwa Patric Chokala na alisaidiwa kuondoka, naweza kukutajia hata mtu aliyempeleka uwanja wa ndege( na ahata ubalozi haukuwahi kujua sababu ya masaibu yake) ila kwa ufupi ilionekana ana matatizo ya afya ya akili.

Kwa wanaojua utaratibu wa address za Russia utaona shaka kabisa na address za hiyo kampuni

Kama uko Moscow ingia inbox nikakuribishe kwangu tuzungumze
Mimi mazungumzo ya wazi hapa ndo nayataka, sikujata jina lake kamili kwa sababu za usalama wake maana habari hizo na nyingine alizotoa ni za kutisha,

pili usijidanganye kwamba watanzania Wote wako kwenye umoja huo, nenda pale chuo st Petersburg nenda Moscow mzima utakutana na watanzania, ambao hawako katika umoja huo,
Umoja huo au wa watanzania au watanzania wengi wanaoishi nchi mbali mbali huwa unakuwa engineered na balozi zetu ambazo ukimbilia sana michango , lakini pia watu mbali mbali wana mambo mengine ya privacy, hawataki kujiexpose kwenye umoja kwa sababu zao japo ina weza kumcost akipata tatizo lakin balozi zetu mtu akipata tatizo response haiwi nzuri mi nimeexperience suala hilo sana,

Hata hotel nilipo ngoja niame aisee maana
 
Aisee huyu mtu sio wa kupuuzwa na kama ni mtu wa hivyo anaweza asichukue muda maana inaonekana ana mengi sana ya watu na siri nyingi kama kuna uwezekano akae chini ya uangalizi maalumu
 
alafu kuna watu wabishi sana, anashangaa address kuwa bx 9 moscow, hajui kwamba hata mifumo yetu baadhi tuliifuma uko,

kuna nchi zinaspesfy na codes kabisa lakin nyingine zinatumia box kawaida, alafu urusi watu ni maskini., sema serikali ndo imejikita kwenye mizinga tu na nuclear
Ujamaa umewagharimu wale jamaa
 
Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha.

Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja (Elibariki Dishon) anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik.

Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi huku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa Marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Afrika, na amekuwa akitafutwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi.
Mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo.

Shirika la Lancerfort limekuwa likimiliki asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhili wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na Urusi.

Wametelekeza mali nyingi kukiwemo na private jets na magari ya thamani.

Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katiKa nchi nyingi,

Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa, mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa Siera Leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakini Rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa Urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,

Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato,

WITO KWA BALOZI ZETU TUNAOMBA MUWASAIDIE HAWA WATANZANIA WANAOKUWA NA MATATIZO MUWASAIDIE

Tukiachana na Shika wapo watanzania wengi wanaokosa msaada wa karibu sana kutoka Kwa balozi zetu hizi ,

Ukisoma ukatafakari haitadhuru

Tufanye nimemaliza

KUNA MENGI SITAYAANDIKA HAPA KUTOKANA NA KUJUA KWAMBA KUMBE HII ISHU NI CRUCIAL , NA KULINDA USALAMA WA DR,

PIA YATAENDELEA KUWA KUMBUKUMBU ZANGU NA KUZIPELEKA MAALI ZITAITAJIKA KWA KUMSAIDIA DR,

USIKURUPUKE KUKOPI HABARI HII, MAANA CODES ZOTE NINAZO MIMI UTASHINDWA KUITETEA,MTU PEKEE MWENYE UWEZO WA KUWEKA EVIDENCE NI MIMI, IKITOKEA UKAKOPI SEMA UMEITOA WAPI,

Britanicca

fac4c12cdf742cab874da9e575e22549.jpg

mwongo kama wewe sijawahi kumwona

web site faki; haifai kabisa

maelezo ya dr niyauwongo ya kutudanganya tulioishia manzese,

money transfer kwa cheque? dunia gani.

kama mmepiga uwongo si muwe waledi? hata matapeli wa tunduma wanawazidi

vipi
 
sasa nimeamini wewe ni Muongo! ni kweli sio wote ambao wako kwenye umoja ila tunajuana wengi hasa walioakaa muda mrefu hapa. Watanzania ambao hupenda kujificha ni wale ambao hawana documents na maisha yao ya kuzuga na ujanja ujanja na na hata hao tunawafahamu. Tunafanya vikao hata watu wa St Peters huja moscow na umoja hauna michango!! acha fix na story ya kutunga, huyo ana matatizo mpelekeni hospital
 
mwongo kama wewe sijawahi kumwona

web site faki; haifai kabisa

maelezo ya dr niyauwongo ya kutudanganya tulioishia manzese,

money transfer kwa cheque? dunia gani.

kama mmepiga uwongo si muwe waledi? hata matapeli wa tunduma wanawazidi

vipi
Maelezo yangu umeona kuna sehemu nimetaja kunieleza yeye? Baada ya kumteka walimpa dawa ya kuyumbisha dish, sijasema mengi
 
Yaani watu ni wabishi sijawahi kuona... Polisi wamechukua benki statement worth and with said amount na hakuna aliyebisha on top wameweza kumuachia kwa kujidhamini still kuna mtu anawasiwasi na huyu Jamaa... Ulizeni waliokuwa wanaenda Urusi Miaka yake na kazi gani walikuwa wakiifanya..
kwa faida ya wote mkuu, waliokuwa wakienda miaka ile walikuwa wakifanya shughuli zipi ili tujifunze
 
siwezi sema ni mbinu za ccm, ila mm niachotaka kusema hapa..huyu shika, ni mtu makini sana na ambaye anatumiwa na watu wasiojulikana kwa mission isiyojulikana hadi sasa.

Kwa website aliyoitaja jana , ukiingia huko huwezi amini ukubwa wa kampuni yake ambayo kwa maelezo yake anasema iko nchi nyingi. Pia, pale chini kwenye hyo website kuna address yao..sina hakika km huko Moscow nako wanatumia P.O.BOX... Anyway.. kwa ufupi kuna maswali mengi kuliko majibu.

Ila hyo mission ilikuwa pia planned na hao YONO.. kwani walianza kutoa warning kuwa atakaye vuruga huo munada atawajibishwa kisheria..walijuaje km siyo kuwa nao walikuwa part of the mission?? Anyway itafahamika tu..km babu wa loliyondo. Time will tell.
Kati ya Wateja wote kamera zilikuwa kwa Dr.Shika. .
Itafahamika tu!!!!
 
  • Thanks
Reactions: MC7
[
Mkuu heshima kwako

Napata wasiwasi mkubwa sana kuhusu maelezo yako, unasema baada ya kufika Moscow leo sijajua leo unaamanisha leo 15th November au lini??

Pili umemtaja Elibariki Dishon kama Mtanzania aliyekupokea hilo pia linatia shaka kwa sababu zifuatazo. Mimi ninaishi Moscow na nina familia na tuna umoja wa Tanzania hapa ( Diaspora) na jina hilo ulilitaja sijawahi kulisikia labda kama huyo Elibariki amekuja Moscow mwezi uliopita.

Pili Dr baada ya kupatwa na masaibu ya kukatwa vidole alikimbilia ubalozi wa Tanzania Moscow, kipindi balozi akiwa Patric Chokala na alisaidiwa kuondoka, naweza kukutajia hata mtu aliyempeleka uwanja wa ndege( na ahata ubalozi haukuwahi kujua sababu ya masaibu yake) ila kwa ufupi ilionekana ana matatizo ya afya ya akili.

Kwa wanaojua utaratibu wa address za Russia utaona shaka kabisa na address za hiyo kampuni

Kama uko Moscow ingia inbox nikakuribishe kwangu tuzungumze

Spasiba dedyushka,dah!ila una moyo kweli,moscow kwa hao vishoka ndio chaka lako!
 
Back
Top Bottom