Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Miongoni mwa watu ambao hawajachukulia mda ni huyu boya
 
Mmh haya mambo ni mkanganyiko hatupaswi kupinga sana au kukubali sana maana Balozi aliyemsaidia kasema hakuwa na lolote isipokuwa alitekwa na Majambazi wakitaka MAPESA yake aliyokuwa anajigamba kuwa anayo. Mm yangu
macho na masikio

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Unamuongelea Mudi Bilali?

Anyway ..to cut the story short ...hao jamaa wako wengi sana.nawafahamu baadhi yao.
Kumbe. Ila makamba wanamuonea

Kuna mzee mmoja wa uko bk amekaa.sana uswis
Kuna mzee wa nuclear
Kuna mzee wa vitalu
Kuna Byansheko
Wengi
 
Hiki kizazi cha vikaptura na jinsi model wanafkiri kuangalia movies za ki spy wanajua kila kitu kinachoendelea katika ulimwengu wa kijasusi huenda dr shika alikua ni asset ya cia kuna vitu sio vya kubeza hasa kampuni ikijihusisha na petroleum na agriculture

Huyu mzee sio wa kumbeza wala kumuweka in ndani wenzetu huwa wana play longshot games huwezi amini
 
Aiseeeeeee ndo umenifungua leo akli yngu kumbe ndo hali halic bhna
 
Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha.

Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja (Elibariki Dishon) anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik.

Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi huku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa Marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Afrika, na amekuwa akitafutwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi.
Mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo.

Shirika la Lancerfort limekuwa likimiliki asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhili wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na Urusi.

Wametelekeza mali nyingi kukiwemo na private jets na magari ya thamani.

Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katiKa nchi nyingi,

Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa, mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa Siera Leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakini Rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa Urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,

Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato,

WITO KWA BALOZI ZETU TUNAOMBA MUWASAIDIE HAWA WATANZANIA WANAOKUWA NA MATATIZO MUWASAIDIE

Tukiachana na Shika wapo watanzania wengi wanaokosa msaada wa karibu sana kutoka Kwa balozi zetu hizi ,

Ukisoma ukatafakari haitadhuru

Tufanye nimemaliza

KUNA MENGI SITAYAANDIKA HAPA KUTOKANA NA KUJUA KWAMBA KUMBE HII ISHU NI CRUCIAL , NA KULINDA USALAMA WA DR,

PIA YATAENDELEA KUWA KUMBUKUMBU ZANGU NA KUZIPELEKA MAALI ZITAITAJIKA KWA KUMSAIDIA DR,

USIKURUPUKE KUKOPI HABARI HII, MAANA CODES ZOTE NINAZO MIMI UTASHINDWA KUITETEA,MTU PEKEE MWENYE UWEZO WA KUWEKA EVIDENCE NI MIMI, IKITOKEA UKAKOPI SEMA UMEITOA WAPI,

Britanicca

fac4c12cdf742cab874da9e575e22549.jpg
Huyo si Franco yupo na Dr
 
Swali: Kwanini Dr Lous Shika amechanganyikiwa au ni mbinu za CCM ilitusahau tukio la Lissu?
Akili zako wewe inatakiwa ukapimwe kwani MTU amekizuia kuendelea na mjadala wowote mbona kuna mikumbwa inaendelea licha ya hili sakata la Dr mwenzangu
 
kagasheki hapana..sio

mudi bilali...likely

nyalandu true dat

kuhusu huyu take it from me
Pamoja na yule maswi
Na huyu aliyetoka.. Akaenda kule...na sasa tena katoka kule..ila hataki tena kwenda popote?
 
yule hapana.amekosa tu dili na njaa zimekuwa nyingi..nenda pale kwa kina mlatie utamfahamu huyo jamaa vizuri
😀 njaa... Vyuma vimeishiwa grisi ... Naona kapi na nzuri zinaendelea kujitenga.. Muda ni tiba!
 
Niliangalia na kusikia maelezo ya Dr. Shika youtube alivyoelezea kutekwa kwake na kukimbia nchi na jinsi malipo yake yanavyoshughulikiwa, kwa kweli That guy anachoongea kina ukweli by 90%.

Nashauri ubalozi wa Tanzania nchini Urusi wawasiliane na ubalozi wa Marekani hukohuko kuconfirm madai ya Daktari ili kama ni kweli haki yake ipatikane.
 
Back
Top Bottom