Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

kama vile ni agent wa CIA nikiunganisha dots

maana tuliambiwa/kuna uzi ulisema ubalozi wa tanzania ulimtelekeza lakini ubalozi wa marekani ulimtembelea akiwa hospitali kama sijakosea
Cha kujiuliza ni why america wako nyuma ya dokta shika mpaka leo wakati tz haina mpango nae
 
Aisee, maneno mengi yanaungana na ukweli, ila in reality unawezaje kuwatoroka KGB kindezi ndezi kama alivyosema yeye?
Huyu dokta kuna vitu hatuweki wazi sana...Hili la kutoroka huenda alitoroshwa na hao waliompa msaada wa ndege
 
Ndio maana ana uhakika wa kununua ile mijengo,kumbe hela iko kwenye process!atapata hela yake,wamarekani wakisha kutumia kwenye mission kubwa kama hiyo lazima wakuwezeshe...
Wamarekani bado wako nyuma yake yawezekana kabisa huyu alikuwa undercover informer wa marekani
 
Naanza kupata mwanga kwa hili tukio na huyu mtu..kuna mambo yanafanyika hapa duniani ukisimuliwa unaweza dhani ni hadithi za juma na uledi..
HIi stori ilitoka kabla dokta hajatoka polisi...Lakini imeenda sawa na mahojiano aliyofanyiwa...Kuna kitu nyuma ya huyu mtu
 
Hili bashite hawezi kuamini kabisa ila jazia nyama Kwa kuweka na picha

Cold war iliwaumiza wengi mm luis nakubaliana naye 100%

Lakni balozi zetu za kiafrika suala kama hili hawawezi kuliona hata kidogo

Balozi zetu zenyewe huko marekani haziko salama nyendo zao zinafuatiliwa kila kukicha hapa kwetu mabalozi wao wanakula shumbwela na kuonekana miungu watu umasikini na ushamba utatumaliza afrika

Nasema tena Kwa kujiamini Tanzania hakuna spy anaweza kupandikizwa na kulifanikisha suala la shika tuache maigizo .shika apambane na umaarufu wake mungu ammbariki sana aendelee kuwa hai mpaka hapo atakapo ipata mizigo yake

Watu kama akina shika ni wengi na hili kosa alilifanya Mwl.J.K.Nyerere
Aliuamini sana mfumo wa kikomunist mpaka akawa anatoa vijana wetu kwenda nje bila document zozote
Kweli kabisa wanaenda kule wanaonekana kuwa magenious wanalishwa sumu na kufanikisha kazi za wengine badala ya kulisaidia taifa
 
Hivi nani
kama vile ni agent wa CIA nikiunganisha dots

maana tuliambiwa/kuna uzi ulisema ubalozi wa tanzania ulimtelekeza lakini ubalozi wa marekani ulimtembelea akiwa hospitali kama sijakosea
ana contact za huyu babu maana maneno ya kila mtu na lake mi huwa siyaamini.
 
Dr Shika nilivokuwa namfikiria kaniprove wrong kabisa baada ya kufatilia story yake hasa kwenye mitandao ambayo ni mahojiano ya ana kwa ana mzee ni mkweli na hana chembechembe za ubabaishaji ...very smart anajua anachokiongea na ndo kimenifanya niamini maneno yake ....

All in all i can sum up "ni maisha " tu kuchange ndo kumemfikisha hapo alipo

Respect to you Dr Shika
Taratibu watu wanamuelewa hata waliompuuza mwanzo
 
  • Thanks
Reactions: Lee
hUYU MZEE hizi story ana hallucinate atakuwa aliwapa hizo hadithi hao wenzake huko Russia,CIA FBI hawawezi kumtumia mtu kama yule wakawasiliana naye direct lazima awe na HANDLER wa ku exchange infos,sio wajinga eti waache traces za kijinga hivyo.
Huyu mzee kuna ukweli ndani yake kuhusu uspy...Yawezekana kabisa alikuwa anatumika
 
Chai tuu hii kwa hiyo vingunguti ndio kajificha FBI wasimpate...
Htafutwi na FBI bali inasemekana alikuwa anatumika nao alipokuwa urusi kitendo kilichopelekea shirika la kijajusi la nchi hiyo KGB kuwateka na kwenda kuwapa mateso makali kupelekea mpaka wenzake kufariki
 
Duuuh..., haya ndio aliyaeleza Dk. Shika, japo alisema kwamba waliomteka na kumkata vidole walikuwa wanataka dollar milioni 1.5 na sio kwamba walimtuhumu kwa uspy. Usalama wa taifa Tanzania wanakula pesa za bure tu, hii kazi uliyoifanya ilibidi wao ndio waifanye
Dk shika hapa katufumba kitu haiwezekani watu wakuteke wanataka fedha wakuponde ponde vidole, wakupige shoti za umeme, wakung'oe meno kwa plaizi,wakuvunje mbavu na kukuharibu sikio...Huyu alikuwa anabanwa kuhusu mambo aliyohisiwa
 
Dr. anizidi kituchanga aisee! kichwa changu mara kinakubali story zake mara kinakataa.endeleeni kufukunyua mtuweke huru,alafu nahitaji no. yake nimtumia vijicent vya kujikimu anatia huruma.
Kesho nitaenda kumtembelea nikipata nafasi...Kuna nguo na viatu sivitumii nataka kumpelekea
 
Kabisa mkuu akiwa mzima kuna vitu vitagunduliwa na kama bado ana connection na USA ni shida nyingine hiyo.
Rais wa kampuni sio mtu kidogo ,lazima ana info nyeti sana.
Yaani huyu ana data nyingi sana ndo maana alikuja kujificha na kuishi kwenye mazingira yenye low profile
 
Back
Top Bottom