Baada ya kufiwa na ndugu yangu ndiyo nimegundua Tanzania tunachemka

Tila-lila2

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
652
Reaction score
1,058
Tarehe 11 ilinilazimu kusafiri toka Shinyanga hadi Dar-es-Salaam kuhudhuria msiba wa ndugu yangu. Nilifika usiku na bahati mbaya tayari alishazikwa na ushiriki wa ndugu kwenye msiba wake uliwekewa masharti na uongozi wa Serikali.

Washiriki wa mazishi na hata msiba kwa ujumla walitengenezewa mazingira ya hofu kwa sababu vigezo vinavyosemwa kuhusu corona inaoenekana vilijitokeza katika kifo cha ndugu yangu. Tofauti na wengi kufariki wakiwa na umri umeenda kdg mdogo wetu huyu yeye alikuwa bado kijana chini ya miaka 40 na kifo chake kwa kweli kilikuwa ni cha ghafla sana sana na hakuna mtu aliamini kama angeweza kufariki kifo cha vile, kuugua matatizo ya kupumua na ndani ya siku tatu kufariki. Msiba wake umekuwa wa baridi sana na umetuumiza sana familia.

Ingawa hakuna mwanafamilia ameonekana kuwa na dalili za kuambukizwa na Marehemu leo hii ni siku ya nne Dar lakini kwake na marehemu panaogopwa na hata mimi natamani niijue kwanza afya yangu kabla sijarudi Shinyanga. Hatujui ndugu yetu alipatia wapi Corona ingawa mazingira yanaonesha ni kazini kwake (sipataji ili nisilete taharuki).

Ninachotaka kusema hata kama ni kweli kuna maelekezo ya kumalizika kwa uchunguzi wa vipimo kwanza ndipo WaTanzania waanze kupimwa kutambua corona, kwangu nailaumu sana Serikali. Kama mashine za vipimo hivi haziamiki kwanini Serikali isingeagiza vipimo vingine sehemu ingine haraka kwa ajili ya kuokoa afya za WaTanzania.

Kwanini Serikali isingelichukua suala hili kama dharura uchunguzi wa mashine hizo ufanyike usiku na mchana? Iwapo je mashine hizo kweli ni tatizo itachukuwa muda gani kupata zingine?

Hivi kwanini Serikali hii imeweka kiburi sana kuhusu jambo hili? Hivi ni kweli Rais wetu Mpendwa amefikia hatua hii kweli? Yaani waTanzania tunakufa yeye hashtuki kweli?

Hivi ni busara kweli kukubali kuwa hatuna uwezo wa kupata vipimo ambavyo tunaweza kuviamini? Nchi kwa kweli imekuwa ya ajabu sana.

Pamoja na kumkubali Rais wangu kwa hili hapana na inaniuma sana kuona watu wanapoteza maisha kwa sababu eti Nchi yetu haina mashine za kupima corona na zilizopo zinahisiwa kuwa mangumashi.

Ukiguswa na msiba wa corona ndiyo utaona machungu yake.
 
Pole sana kwa msiba uliowafika, kwa kifupi huwezi kujua namna hili janga linavyochukuliwa poa na madhara yake yanaumiza sana, huwezi kuelewa mpaka litakapofika kwa watu wako wa karibu.

R.I.P Ndugu Yetu
 
Umesena aliugua siku nne na leo no siku ya nne tangu msiba utokee?Angalia kazi ya ndugu yako ni ipi, mahusiano yake ya kimapenzi, mikopo, ushirikina, ujirani mwema n.k husababisha msongo wa mawazo, vifo vya ghafla na magonjwa yasiyoambukizwa.

***Usisahau kujifukiza Corona ipo**
 
Tarehe 11 ilinilazimu kusafiri toka Shinyanga hadi Dar-es-Salaam kuhudhuria msiba wa ndugu yangu. Nilifika usiku na bahati mbaya tayari alishazikwa na ushiriki wa ndugu kwenye msiba wake uliwekewa masharti na uongozi wa Serikali.

Washiriki wa mazishi na hata msiba kwa ujumla walitengenezewa mazingira ya hofu kwa sababu vigezo vinavyosemwa kuhusu corona inaoenekana vilijitokeza katika kifo cha ndugu yangu. Tofauti na wengi kufariki wakiwa na umri umeenda kdg mdogo wetu huyu yeye alikuwa bado kijana chini ya miaka 40 na kifo chake kwa kweli kilikuwa ni cha ghafla sana sana na hakuna mtu aliamini kama angeweza kufariki kifo cha vile, kuugua matatizo ya kupumua na ndani ya siku tatu kufariki. Msiba wake umekuwa wa baridi sana na umetuumiza sana familia.

Ingawa hakuna mwanafamilia ameonekana kuwa na dalili za kuambukizwa na Marehemu leo hii ni siku ya nne Dar lakini kwake na marehemu panaogopwa na hata mimi natamani niijue kwanza afya yangu kabla sijarudi Shinyanga. Hatujui ndugu yetu alipatia wapi Corona ingawa mazingira yanaonesha ni kazini kwake (sipataji ili nisilete taharuki).

Ninachotaka kusema hata kama ni kweli kuna maelekezo ya kumalizika kwa uchunguzi wa vipimo kwanza ndipo WaTanzania waanze kupimwa kutambua corona, kwangu nailaumu sana Serikali. Kama mashine za vipimo hivi haziamiki kwanini Serikali isingeagiza vipimo vingine sehemu ingine haraka kwa ajili ya kuokoa afya za WaTanzania.

Kwanini Serikali isingelichukua suala hili kama dharura uchunguzi wa mashine hizo ufanyike usiku na mchana? Iwapo je mashine hizo kweli ni tatizo itachukuwa muda gani kupata zingine?

Hivi kwanini Serikali hii imeweka kiburi sana kuhusu jambo hili? Hivi ni kweli Rais wetu Mpendwa amefikia hatua hii kweli? Yaani waTanzania tunakufa yeye hashtuki kweli?

Hivi ni busara kweli kukubali kuwa hatuna uwezo wa kupata vipimo ambavyo tunaweza kuviamini? Nchi kwa kweli imekuwa ya ajabu sana.

Pamoja na kumkubali Rais wangu kwa hili hapana na inaniuma sana kuona watu wanapoteza maisha kwa sababu eti Nchi yetu haina mashine za kupima corona na zilizopo zinahisiwa kuwa mangumashi.

Ukiguswa na msiba wa corona ndiyo utaona machungu yake.
Pole sana mkuu,kuficha ficha mambo ndio unazidi kuvuruga,kwanini usiseme kazini kwake ili watu wachukue tahadhari ya kutoambukiza wengine? Ungeweka wazi hata kwa codes ili wafanyakazi wenzake waweze kujitenga na familia pia kupiga nyungu na kutumia dawa asili unavyoficha sehemu ya kazi yake unazidi kuongeza janga zaidi.

Covid inasumbua kama una kinga dhaifu ,wenye kinga dhaifu sio tu watu wenye umri mkubwa hata wenye magonjwa ambayo yanapunguza kinga nao wanakuwa na kinga dhaifu hata kama wana umri mdogo.
 
Acha uongo wako wewe!! Tumeshawajua janja yenu!!
 
Huyo ni muongo tu
 
Roho ya marehemu ipumzike kwa amani....
Hofu n zaidi ya korona,pia ugonjwa wa shambulio la moyo ni hatari sana hapo nyuma kidogo umeondoa wengi na sasa ukichanganya na huyu mnyamwezi wa wuhan basi tafrani tupu.

Endeleeni kufuata hatua zinazotakikana ili kujikinga na mnyamwezi wa wuhan....
 
Daaah.... Bora umeujua ukweli juu ya serikali uliyokuwa ukiisapoti hapo kabla.
Siku nyingine usijiweke pembeni kutetea haki na utu ukidhani upo salama sana hapa duniani!

Madhila na manyanyaso wanayopata wenzako yanaweza kukufika muda wowote tena kwa kusababishwa na hao unaowafagilia leo...!!
Usiyumbishwe baada ya kuufahamu ukweli...!!
 
Tarehe 11 ilinilazimu kusafiri toka Shinyanga hadi Dar-es-Salaam kuhudhuria msiba wa ndugu yangu. Nilifika usiku na bahati mbaya tayari alishazikwa na ushiriki wa ndugu kwenye msiba wake uliwekewa masharti na uongozi wa Serikali.

Washiriki wa mazishi na hata msiba kwa ujumla walitengenezewa mazingira ya hofu kwa sababu vigezo vinavyosemwa kuhusu corona inaoenekana vilijitokeza katika kifo cha ndugu yangu. Tofauti na wengi kufariki wakiwa na umri umeenda kdg mdogo wetu huyu yeye alikuwa bado kijana chini ya miaka 40 na kifo chake kwa kweli kilikuwa ni cha ghafla sana sana na hakuna mtu aliamini kama angeweza kufariki kifo cha vile, kuugua matatizo ya kupumua na ndani ya siku tatu kufariki. Msiba wake umekuwa wa baridi sana na umetuumiza sana familia.

Ingawa hakuna mwanafamilia ameonekana kuwa na dalili za kuambukizwa na Marehemu leo hii ni siku ya nne Dar lakini kwake na marehemu panaogopwa na hata mimi natamani niijue kwanza afya yangu kabla sijarudi Shinyanga. Hatujui ndugu yetu alipatia wapi Corona ingawa mazingira yanaonesha ni kazini kwake (sipataji ili nisilete taharuki).

Ninachotaka kusema hata kama ni kweli kuna maelekezo ya kumalizika kwa uchunguzi wa vipimo kwanza ndipo WaTanzania waanze kupimwa kutambua corona, kwangu nailaumu sana Serikali. Kama mashine za vipimo hivi haziamiki kwanini Serikali isingeagiza vipimo vingine sehemu ingine haraka kwa ajili ya kuokoa afya za WaTanzania.

Kwanini Serikali isingelichukua suala hili kama dharura uchunguzi wa mashine hizo ufanyike usiku na mchana? Iwapo je mashine hizo kweli ni tatizo itachukuwa muda gani kupata zingine?

Hivi kwanini Serikali hii imeweka kiburi sana kuhusu jambo hili? Hivi ni kweli Rais wetu Mpendwa amefikia hatua hii kweli? Yaani waTanzania tunakufa yeye hashtuki kweli?

Hivi ni busara kweli kukubali kuwa hatuna uwezo wa kupata vipimo ambavyo tunaweza kuviamini? Nchi kwa kweli imekuwa ya ajabu sana.

Pamoja na kumkubali Rais wangu kwa hili hapana na inaniuma sana kuona watu wanapoteza maisha kwa sababu eti Nchi yetu haina mashine za kupima corona na zilizopo zinahisiwa kuwa mangumashi.

Ukiguswa na msiba wa corona ndiyo utaona machungu yake.
Endelea kumpenda rais wako mpendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole sana kwa msiba wa ndugu yako.

Taarifa za ugonjwa wa Corona kutoka sehemu mbalimbali duniani zinaonyesha ni nadra sana kwa vijana wenye afya nzuri kufariki kutokana na COVID.Ndugu yako alikuwa anasumbuliwa na matatizo mengine ya kiafya kabla kuugua huu ugonjwa?
 
Back
Top Bottom