Baada ya kufiwa na ndugu yangu ndiyo nimegundua Tanzania tunachemka

, by the way lengo lake siyo kupewa pole bali kuelezea hali halisi aliyopitia kuhusiana na msiba wa ndugu yake, Period
Kwani kuna MTU alizihitaji hizo information? Anaanza kubwabwaja tu ohhh mimi nimefiwa na ndugu kwa corona ohhh kilienda kilirudi ushahidi hamna. kwani kuna MTU alimuomba alete hizo bwabwaja zake?

Kama lengo lake sio kupewa pole lengo lake lilkikuwa nini alitaka mchango au ? Nyooo Nani ampe mchango kwa msiba hewa? Humu jamii forums?
 
kuna waliojifunza na kuguswa, kama wewe unaona haikuhusu unaweza kukaa kimya maana hii ni public forum kila mtu yupo huru ku share, usiwazuie watu kuzungumza
 
tuwekee vyeti vyao vya vifo vinavyoonyesha wamekufa kwa corona tukuamini vinginevyo Wewe ni mwongo tu kama waongo wengine ila wako umekubuhu kwa kuwa unapitia kwenye kusingizia vifo hewa
Wewe ni fala
 
Nimekufuatilia sana ndugu. SIkutaka kubishana na wewe manake inawezekana we ni wa nyumba nyeupe mnaojaribu kuzuia taarifa. Nimerudi Shinyanga jana nikiwa nakuombea Mungu akuepushe na hili janga. Manake jana pia nimesikia mwenzangu aliyekuwa na siha njema tu niliyesoma naye Mazengo Sekondari miaka ya 90 mwishoni amefariki kwa dalili za gonjwa hilo hilo.
 
Manake jana pia nimesikia mwenzangu aliyekuwa na siha njema tu niliyesoma naye Mazengo Sekondari miaka ya 90 mwishoni amefariki kwa dalili za gonjwa hilo hilo.
Kikwete alisema cha kusikia changanya na za kwako kwa hiyo uliposikia kafa kwa corona ukaamini uliona hicho cheti cha kifo kinasomeka kuwa kafa kwa corona?
 
Time ya kuchunguza mashine za kupima corona iliagizwa mpaka May 13 iwe na majibu, leo 18 ndio inategemewa kuwasilisha taarifa. Kenya vipimo vipo mpaka Namanga , ndani ya 45 minutes majibu yametoka, madereva endelea na safari au abouturn. Afya wataalamu wanatimuliwa, kuna nini?
Pole sana kwa msiba uliowafika, kwa kifupi huwezi kujua namna hili janga linavyochukuliwa poa na madhara yake yanaumiza sana, huwezi kuelewa mpaka litakapofika kwa watu wako wa karibu.


R.I.P Ndugu Yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kweli kweli!
 
Mkuu karibu nyumbani kwangu Mbagala...jumapili ni Kigodoro tu mwendo wa kutimua vumbiiii
#AfterCoronaBaash
 
Huu ugonjwa umefanywa kuwa janga la familia.

Kwamba upo na unaua? Hadi yakupate kama kwa mleta mada. Mithili ya wale wachuma majanga.

Watoto wadogo hadi wa chekechea wanapokwenda shule na kurejea majumbani, (kwa kuanzia) nadharia ya kila mtu achukue tahadhari inakuwa haina tofauti na kuhadharisha mbuzi.
 
Hizi kauli za kwamba hadi yakukute ndio ujue kuwa corona ipo na inauwa zinanishangaza maana kama ugonjwa ni janga la dunia na ni ugonjwa hatari iweje tena iwe hadi uone ndugu yako akifa ndio ujue uwepo wa huu ugonjwa?
 



Umeandika vizuri ila hiyo “buana” hapo mwishoni ndo umeharibu.
 
Covid ipo tuendelee kujikinga hivi yule mke wa mzee leta nini kime mkwapua fasta hivo
 
Broo taja eneo alilokuwa anafanya kazi ndugu yako utakuwa umeokoa maisha ya wengi

Kama unaficha basi na wewe huna tofauti na hao ssm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…