Nikiwa sina kazi leo nikaamua kujishughulisha kidogo kwa kufanya kautafiti kangu ka-usafi (afya) wa hivi vi-mgahawa vya hapa mitaani kwetu tunakopatia chai na lunch. Nikaona nishughulike na nyendo zao za chooni kwanza. Nimepitia migahawa minne na kote nimekutana na mambo yanayofanana kwa 100%.
Nitasimulia cha mgahawa mmoja, kwa niaba ya mingine. Ikawa hivi;
Katoka chooni moja kwa moja hadi kwenye dishi lenye maji anayooshea vyombo na kutosa mkono wake wa kulia kujichuuzia maji kwa kutumia kiganja cha huo mkono wa kulia. Nilishangaa!
Kachukua sabuni ya unga ya kuoshea vyombo kwa mtindo wa kupamba (maana aliiweka tu katika chombo cha wazi (sahani) kwa kutumia mkono wake wa kushoto na kuendelea kujisuuzia maji na sasa akijihesabu ndo ananawa na sabuni.
Nikasema ngoja nifike na huko chooni kwenyewe kwanza nikaangalie mazingira. Nikaomba ruhusa kwamba naenda kujisaidia haja ndogo. Kwakuwa mi ni mzoefu wakaniruhusu......kufika huko Mungu wangu!!! Inye zinaonekana hovyo hovyo, uchafu mtupu.
Sili tena migahawani.