Baada ya kufuatilia uendaji wa chooni wa huyu dada muuza mgahawa, nimejiapiza sili tena migahawa ya uswahilini

Baada ya kufuatilia uendaji wa chooni wa huyu dada muuza mgahawa, nimejiapiza sili tena migahawa ya uswahilini

Kaka kuwa mpole ukifuatilia kila unachokula jinsi kinavyoandalia hata cha mkeo au dada wa ndani hutokula. Ni bora ujifanye hujaona wala hujui utaishia maisha safi.

Mama yangu aliwahi kuniambia kuwa hakuna sababu wala umuhimu wa kwenda kupima afya zetu kila mara hata kama hauumwi kwani tunatembea na magonjwa mengi mwilini bila kujua.
Kwako, unaweza ukaujenga utamaduni wa usafiekwa namna ambavyo kila anayefika, "anamezwa" na huo utamaduni. Hata ilifika siku anaondoka, anakuwa na "tabia" nyingine ya kiusafi.

Inawezekana. Nimefanya hivyo kwangu.
 
Huyo ni msafi.

Umewahi kuona mkaanga au mchoma chapati wewe? Sema hapana, hapa kijiweni yupo, akimsafisha mtoto ni kwamba kazi inaendelea.

Mungu tu analinda walaji
Kwa ufupi, hilo ni tatizo kwa maeneo mengi Tanzania. Nikiwa kijiji fulani wakati fulani, niliomba niandaliwe chakula fulani kwenye familia niliyokuwa nimejenga nayo mazoea.

Nilipokifuata chakula changu, mama mwenye nyumba alimwambia bintiye akipakue hicho chakula.

Kabla hajakipakua, alimsafisha kwanza mtoto aliyekuwa amejisaidia. Alipomaliza, alijinyunyizia maji mkono alioutumia kumsafisha mtoto.

Ilibidi nitafute jinsi ya kumkwamisha kunipakulia chakula, kwa sababu chombo chochote ambacho angekishika, ningekihesabu kuwa ni kichafu. Nilifanikiwa katika hilo, na bahati nzuri, hawakugundua nia yangu, kwa hiyo hawakukwazika.
 
Ni changamoto sana mkuu, juzi nimeenda kwenye mgahawa wenye hadhi hadhi, nimechukua takeaway, Dada akaweka kwenye chakula kachumbari ya tango kwa mkono, ikabidi chakula niamue kuwapa mbwa wangu. Nimegundua usipokuwa makini na hii migahawa, utakuwa unasumbuliwa sumbuliwa na tumbo
Unajua kwa nini kafanya hivyo? Ni kwa sababu na wateja wengi wanafanana naye kimtazamo, kwa hiyo wamwonapo akifanya hivyo wanaona ni kawaida.
 
Nikiwa sina kazi leo nikaamua kujishughulisha kidogo kwa kufanya kautafiti kangu ka-usafi (afya) wa hivi vi-mgahawa vya hapa mitaani kwetu tunakopatia chai na lunch. Nikaona nishughulike na nyendo zao za chooni kwanza. Nimepitia migahawa minne na kote nimekutana na mambo yanayofanana kwa 100%. Nitasimulia cha mgahawa mmoja, kwa niaba ya mingine. Ikawa hivi;

Katoka chooni moja kwa moja hadi kwenye dishi lenye maji anayooshea vyombo na kutosa mkono wake wa kulia kujichuuzia maji kwa kutumia kiganja cha huo mkono wa kulia.......nilishangaa!

Kachukua sabuni ya unga ya kuoshea vyombo kwa mtindo wa kupamba (maana aliiweka tu katika chombo cha wazi (sahani)) kwa kutumia mkono wake wa kushoto na kuendelea kujisuuzia maji na sasa akijihesabu ndo ananawa na sabuni.

Nikasema ngoja nifike na huko chooni kwenyewe kwanza nikaangalie mazingira. Nikaomba ruhusa kwamba naenda kujisaidia haja ndogo. Kwakuwa mi ni mzoefu wakaniruhusu......kufika huko Mungu wangu!!! Inye zinaonekana hovyo hovyo.....uchafu mtupu.

Sili tena migahawani......
Lakini si umeshakula sana na ukanenepa? Hivyo ulivyoviona ndiyo virutubisho ambavyo vimekupatia hiyo afya imara uliyo nayo.
 
Bongo watu wachafu balaa,Kuna nyumba fulani uku kitaa ninapokaa,Ina wapangaji kibao nikipitaga na Kuta mpangaji Mmoja anamtenga mwanae anajisaidia katikati ya uwanja na watu tunapita aisee uwa namuona uyo Maza mchafu balaa yaani anashinda kumtenga ata pembeni ya uwanja mafichoni mpaka uwanjani,mi ata nyumba yenye watoto wadogo wengi kupanga aisee siwezi
 
Nikiwa sina kazi leo nikaamua kujishughulisha kidogo kwa kufanya kautafiti kangu ka-usafi (afya) wa hivi vi-mgahawa vya hapa mitaani kwetu tunakopatia chai na lunch. Nikaona nishughulike na nyendo zao za chooni kwanza. Nimepitia migahawa minne na kote nimekutana na mambo yanayofanana kwa 100%. Nitasimulia cha mgahawa mmoja, kwa niaba ya mingine. Ikawa hivi;

Katoka chooni moja kwa moja hadi kwenye dishi lenye maji anayooshea vyombo na kutosa mkono wake wa kulia kujichuuzia maji kwa kutumia kiganja cha huo mkono wa kulia.......nilishangaa!

Kachukua sabuni ya unga ya kuoshea vyombo kwa mtindo wa kupamba (maana aliiweka tu katika chombo cha wazi (sahani)) kwa kutumia mkono wake wa kushoto na kuendelea kujisuuzia maji na sasa akijihesabu ndo ananawa na sabuni.

Nikasema ngoja nifike na huko chooni kwenyewe kwanza nikaangalie mazingira. Nikaomba ruhusa kwamba naenda kujisaidia haja ndogo. Kwakuwa mi ni mzoefu wakaniruhusu......kufika huko Mungu wangu!!! Inye zinaonekana hovyo hovyo.....uchafu mtupu.

Sili tena migahawani......
Mi ntaendelea kula tu. Miaka yote hii nione kinyaa leo?
 
Kuna siku nilichungulia ndani ya ndoo tuliyokuwa tunanawia mikono Kwa Maza lishe aisee nilikuta Kuna uchafu WA kutosha ndani😀😀pia nishashudia kunguru wanakunywa maji wanayonawa wateja kabla ya kula,mama lishe wengi miyeyusho
Hawastahili kulaumiwa, wa kulaumiwa ni sisi ambao tumeona kasoro lakini tukafumbia macho. Alau hata mleta uzi kachukia hatua ya "kupiga" kelele mtandaoni.

Mi ilifikia hatua mpaka nikawa nafikiria kuwa huenda mtazamo wangu una kasoro. Ni kutokana na kukereka na hali ya uchafu wakati wengine wengi wakiona ni kawaida.
 
Kaka kuwa mpole ukifuatilia kila unachokula jinsi kinavyoandalia hata cha mkeo au dada wa ndani hutokula. Ni bora ujifanye hujaona wala hujui utaishia maisha safi.

Mama yangu aliwahi kuniambia kuwa hakuna sababu wala umuhimu wa kwenda kupima afya zetu kila mara hata kama hauumwi kwani tunatembea na magonjwa mengi mwilini bila kujua.
Blazameni tu huyo nae kama vp pika geto kwako mtu amenawa kabisa unajiongelesha je angetoka toilet na kuliunga kwenye chapati ungesemaje?behave bro
 
Siwalaumu! Ni mama zetu, dada zetu, ndugu zetu, kwa hiyo ni sehemu yetu! Inawezekana, hata mimi, kama nisingepita mazingira niliyoyapita, ningekuwa kama wao. Lakini ukweli ni kwamba hali ya usafi binafsi nchini Tanzania bado uko chini sana.

Naamini hawakusudii kufanya hivyo, bali ndiyo mtazamo wao. Wanaona wako sahihi, hasa ikizingatiwa kuwa ndivyo walivyolelewa.

Kuna mahali nilikuwa nimepiga kambi ya kikazi, na nikawa naenda kula kwenye mghahawa uliopo maeneo ya jirani. Nilifikia hatua nikaamua kuwapa bure "kijiko/kishikio" cha kushikia chapati. Nilikuwa nakereka, unaagiza chapati, mhudumu anatoa kwa mikono mitupu ambayo imetoka kuhesabu hela, na wakati mwingine ameshika na vitu vingine na maeneo ya mwili wake kama kichwa, n.k.

Nilikuwa napenda sana kutafuna karanga zilizokaangwa, zile zinazofungwa kwenye vipakiti vya nailoni. Nilikoma kufanya hivyo kutokana na nilichokishuhudia kikifanywa na mkaanga karanga wakati akiendelea na zoezi la ukaangaji karanga.

Binafsi, naona kuna uhitaji mkubwa sana wa semina za usafi kufanywa, ikibidi, kwa kila kaya nchi nzima bila kujali kama ni familia ya wasomi au la.
Kuna maeneo mengi tu wanayouza supu huwa wanashika kwa mkono wa kushoto nyama zilizoiva wanazokatia wateja wa supu.
 
Hujawahi kujua katika migahawa na bar jagi au birika linalonawashia watu mikono hurudishwa kwenye bakuli la maji machafu yaliyonawiwa na ndio hilo hilo hutumika kuchota katika ndoo maji ya kukunawashia mikono??
Nilishawahi kufanya kazi kwenye shule moja binafsi iliyokuwa na ngazi ya chekechea hadi kidato cha Nne.

Nilishangaa kukuta ndoo za chooni na bafuni ndizo zinazotumika kusombea maji ya jikoni. Fikiri ndoo ya chooni kuingizwa kwenye kisima kinachotunza maji yanayotumika kwenye campus nzima ya shule! Si ajabu watoto walikuwa hawakomi kupatwa na minyoo aina ya "ascaris"

Cha kushangaza, hakukuweko na Mwalimu hata mmoja aliyeona kuwa hilo ni tatizo.

Namshukuru Mungu nilifanikiwa kuwabadilisha katika hilo.

Mwanzoni nilitumia mbinu ya ukali nikakwama. Baadaye, nikabadili mbinu, nikatumia "bottom up approach" ikafanikiwa na ikawa ni tabia ya hiyo shule. Miaka mingi imeshapita, lakini naamini hiyo tabia ya usafi ingalipo kwenye hiyo shule, au imeboreshwa zaidi.
 
Back
Top Bottom