Baada ya kufuatilia uendaji wa chooni wa huyu dada muuza mgahawa, nimejiapiza sili tena migahawa ya uswahilini

Kwako, unaweza ukaujenga utamaduni wa usafiekwa namna ambavyo kila anayefika, "anamezwa" na huo utamaduni. Hata ilifika siku anaondoka, anakuwa na "tabia" nyingine ya kiusafi.

Inawezekana. Nimefanya hivyo kwangu.
 
Huyo ni msafi.

Umewahi kuona mkaanga au mchoma chapati wewe? Sema hapana, hapa kijiweni yupo, akimsafisha mtoto ni kwamba kazi inaendelea.

Mungu tu analinda walaji
Kwa ufupi, hilo ni tatizo kwa maeneo mengi Tanzania. Nikiwa kijiji fulani wakati fulani, niliomba niandaliwe chakula fulani kwenye familia niliyokuwa nimejenga nayo mazoea.

Nilipokifuata chakula changu, mama mwenye nyumba alimwambia bintiye akipakue hicho chakula.

Kabla hajakipakua, alimsafisha kwanza mtoto aliyekuwa amejisaidia. Alipomaliza, alijinyunyizia maji mkono alioutumia kumsafisha mtoto.

Ilibidi nitafute jinsi ya kumkwamisha kunipakulia chakula, kwa sababu chombo chochote ambacho angekishika, ningekihesabu kuwa ni kichafu. Nilifanikiwa katika hilo, na bahati nzuri, hawakugundua nia yangu, kwa hiyo hawakukwazika.
 
Unajua kwa nini kafanya hivyo? Ni kwa sababu na wateja wengi wanafanana naye kimtazamo, kwa hiyo wamwonapo akifanya hivyo wanaona ni kawaida.
 
Lakini si umeshakula sana na ukanenepa? Hivyo ulivyoviona ndiyo virutubisho ambavyo vimekupatia hiyo afya imara uliyo nayo.
 
Bongo watu wachafu balaa,Kuna nyumba fulani uku kitaa ninapokaa,Ina wapangaji kibao nikipitaga na Kuta mpangaji Mmoja anamtenga mwanae anajisaidia katikati ya uwanja na watu tunapita aisee uwa namuona uyo Maza mchafu balaa yaani anashinda kumtenga ata pembeni ya uwanja mafichoni mpaka uwanjani,mi ata nyumba yenye watoto wadogo wengi kupanga aisee siwezi
 
Mi ntaendelea kula tu. Miaka yote hii nione kinyaa leo?
 
Kuna siku nilichungulia ndani ya ndoo tuliyokuwa tunanawia mikono Kwa Maza lishe aisee nilikuta Kuna uchafu WA kutosha ndani😀😀pia nishashudia kunguru wanakunywa maji wanayonawa wateja kabla ya kula,mama lishe wengi miyeyusho
Hawastahili kulaumiwa, wa kulaumiwa ni sisi ambao tumeona kasoro lakini tukafumbia macho. Alau hata mleta uzi kachukia hatua ya "kupiga" kelele mtandaoni.

Mi ilifikia hatua mpaka nikawa nafikiria kuwa huenda mtazamo wangu una kasoro. Ni kutokana na kukereka na hali ya uchafu wakati wengine wengi wakiona ni kawaida.
 
Blazameni tu huyo nae kama vp pika geto kwako mtu amenawa kabisa unajiongelesha je angetoka toilet na kuliunga kwenye chapati ungesemaje?behave bro
 
Kuna maeneo mengi tu wanayouza supu huwa wanashika kwa mkono wa kushoto nyama zilizoiva wanazokatia wateja wa supu.
 
Hujawahi kujua katika migahawa na bar jagi au birika linalonawashia watu mikono hurudishwa kwenye bakuli la maji machafu yaliyonawiwa na ndio hilo hilo hutumika kuchota katika ndoo maji ya kukunawashia mikono??
Nilishawahi kufanya kazi kwenye shule moja binafsi iliyokuwa na ngazi ya chekechea hadi kidato cha Nne.

Nilishangaa kukuta ndoo za chooni na bafuni ndizo zinazotumika kusombea maji ya jikoni. Fikiri ndoo ya chooni kuingizwa kwenye kisima kinachotunza maji yanayotumika kwenye campus nzima ya shule! Si ajabu watoto walikuwa hawakomi kupatwa na minyoo aina ya "ascaris"

Cha kushangaza, hakukuweko na Mwalimu hata mmoja aliyeona kuwa hilo ni tatizo.

Namshukuru Mungu nilifanikiwa kuwabadilisha katika hilo.

Mwanzoni nilitumia mbinu ya ukali nikakwama. Baadaye, nikabadili mbinu, nikatumia "bottom up approach" ikafanikiwa na ikawa ni tabia ya hiyo shule. Miaka mingi imeshapita, lakini naamini hiyo tabia ya usafi ingalipo kwenye hiyo shule, au imeboreshwa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…