Baada ya kufunga maombi, rafiki yangu akapatwa na janga

Baada ya kufunga maombi, rafiki yangu akapatwa na janga

Usimuache mtu mchawi aishi wateketeze wote na mganga wake kupitia maombi ya usiku wa manane na kufunga tatu kavu.
 
Mimi mchawi akinijia namtumia mishale milioni 60 ya moto kwa damu ya YESU Kristo. Huwa awarudi na wachawi wenzao upata maisha.
 
Piga dua la kuua mchawi Ili ajue ulozi akawalozi wajinga wasio na neno.
 
Jina la Yesu utenda Kazi kwa mtu yeyeto ni unlimited, halina gharama, upatikana kwa wingi, mda wote tena ni bure.
Nashangaa vipofu wanaoenda kutapeliwa wakati hata wao wanaweza afanyacho mtume na Nabii
 
Mchawi, mganga, sijui Jinni hata awe na phd ya ulozi, kamtolea Sana shetani kafara, sijui ana degree za juu kabisa ashatoka kwenye ubinadamu yaani kafikia level ya kupeleka maombi yake kwa wale majemedari 6 wa shetani kina lucifuge lofokale na majemedari wengine wa shetani, hawezi vuka ACDs 40% wakati Jesus Christ ana ACDs 100%.
So usiogope wala kumuogopa mchawi, sijui jinn sijui mganga. Ukiogopa tu umeruhusu hofu ( MONSTER SPIRIT 👹💀 ) ndio itakayokumaliza.
Mchawi, jinni ucheza na hofu yako ni lazima wakutishe kwanza.
Thus wakoloni awakuruhusu wala kuipa hofu nguvu thus walimudu kuwatawala waafrika ikiwemo na wachawi sugu hata kuwapeleka utumwani.
Uchawi ungekuwa na nguvu kihivyo zaidi ya kupewa nguvu na propaganda tu mkoloni asingeweza kumtawala mwafrika.
 
Huu mchezo ni mwingi sana katika dunia ya leo, hatari sana, huwa nasema hata haya mateja mengi sio hiyari yao!, kuna kuwa na issue imepigwa au kufanywa pengine na wazazi wao lakini gagula aliwaficha kuhusu matokeo ya mbeleni. /OVA.
 
Maombi ndiyo njia sahihi ya kupambana na vita ya kiroho na siyo kukimbilia kwa waganga wa kienyeji, Maombi yana nguvu ya ajabu hasa kama una imani.
 
Habari wana JF?

Natumaini mnaendelea vizuri!

NB: Nimeandika hii kwa niaba! Nimesimuliwa hadi chozi likatoka.

Wapwa, kuna suala linaniumiza sana kichwa nalo ni kuhusiana na kinachompata rafiki yangu kwa sasa.

Stori iko hivi:
Mimi na rafiki yangu tulikutana katika harakati za maisha, tukaamua tufanye harakati zetu kwa ushirikiano pia kama familia.

Tulifungua biashara na kwa vile rafiki yangu hakuwa na ueledi na ile biashara, niliisimamia mimi mwenyewe.

Kiumri rafiki yangu ni mkubwa, anafamilia na mimi sina familia(Single) yaani tunaishi nyumba moja(Kwake).

Sasa rafiki yangu katika harakati ghafla akawa amepata harakati zingine za kusafirisha mizigo kutoka dubai kuja Tanzania.

Maisha yakaendelea hivo, ilikuwa siku, miezi, sasa ni kama mwaka na nusu. Yeye akawa anasafiri mi nabaki na familia yake na anaweza akawa anamaliza wiki kadhaa ndio anakuja.

Rafiki yangu akawa akija ananisimulia, amenunua nyumba kubwa na magari matatu tayari, akawa haulizii hata ile biashara yetu inaendeleaje.

Katika ile biashara mi nikaona inakuwa ngumu, hata nikifanya matangazo kwenye radio, vipeperushi, wateja sipati. Hata nikipata wateja ni kidogo. Nikipata hela haikai, yote inaisha hata hakuna cha maana nilichofanya.

Mwili wangu ukabadilika. Nikawa nahisi muwasho baadhi ya sehemu za mwili. Mwili ukawa wa kivivu. Akili ikalala, kuamka naamka saa nne asubuhi. Nikisema nifanye jambo la maana, akili inaleta uvivu silikamilishi jambo. Mara nikaanza kuwa nahisi kuna vitu vinanitembelea mwilini.

Sasa, baada ya kuulizia kwa watu wanaofahamu hiyo hali, nikaambiwa nimerogwa, nina jini pia. Nimefungwa kwa nguvu za giza.

Baada ya kuambiwa hivo, nikaona dalili pia, ikabidi nifunge maombi.

Sasa ni miezi kama miwili hivi ninaomba na ninamuomba Mungu kuwa 'Aniondelee shetani huyu aliye katika mwili wangu. Na kama ametumwa na mtu kuja kuiba baraka zangu na kuharibu maisha yangu, eeh Mungu muwajibishe mtu huyu. Yale yote aliyonifanyia yamrudie yeye'.

Wapwa, baada ya kuendelea na maombi, rafiki yangu hadi sasa ndiye amekuwa matatizoni. Amekula hasara ya mamilioni ya pesa kwa muda tu huu mfupi. Anadaiwa mali za watu. Hadi sasa, yupo gerezani. Nyumba yake imechukuliwa na gari zake zote.

Wapwa, baada ya kukaa kutafakali, nimeona kama msukosuko wa rafiki yangu ni kama ndio mkanda uliofunga maisha yangu, kwani kuna baadhi ya maneno nakumbuka yanadhihirisha kuwa inawezekana ikawa.

Kuna siku tulikuwa tunaangalia movie, ilikuwa inazungumzia jinsi familia inavyopambana kuokoa maisha ya mtoto wao aliyekuwa anatatizo la figo. Wazazi hao, waliamua kuenda kuteka mtoto mwingine ili wamtoe figo.
Sasa nikamuuliza rafiki yangu kwamba 'Hivi unaweza ukatoa uhai wa mtu mwingine ili maisha yako yaendelee kuwa mazuri?'

Rafiki yangu akajifanya kama hajasikia. Nikarudia tena kumuuliza, ila aliinamisha kichwa na kuwa kama mtu mwenye wasiwasi na hakujibu chochote.

Kingine ni kuna msemo niliwahi kuusikia kutoka kwa watu akisema kamwe hawezi kuniachia niende. Sasa nikajiuliza, haiwezi niachia kivipi?.

Kiukweli wapwa, hayo ndiyo yaliyopo hadi sasa. Kesi inaendelea na mimi maombi yanaendelea. Nikizidi kuomba kesho inazidi kuwa kubwa. Mimi naihurumia familia yake!

Mimi sihukumu moja kwa moja kuwa anaweza kuwa yeye, ila tu ninahisi kutokana na yanayoendelea, kwani kwa mtu mwenye akili na uelewa, kama kuna vitu haviko sawa anatambua tu.
Mkuu haujamshikia mtu panga wala bunduki Wala kumshutumu mtu. ENDELEA kupiga maombi kuokoa nafsi yako, awe anahusika juu ya kufunga baraka zako au ahusiki "VITA SI VYAKO BALI MUNGU ANAKUPIGANIA"
 
Ngoja na Mimi nianze kuingia kwenye Maombi Maalum niongee na Baba yangu alie sirini
 
Endelea kukaza hadi uone mwisho wake,ukilegeza akipata nafuu ndio utakuwa mwisho wa maisha yako
 
Mkuu haujamshikia mtu panga wala bunduki Wala kumshutumu mtu. ENDELEA kupiga maombi kuokoa nafsi yako, awe anahusika juu ya kufunga baraka zako au ahusiki "VITA SI VYAKO BALI MUNGU ANAKUPIGANIA"
Barikiwa sana!
 
Back
Top Bottom