Baada ya kufunguliwa Dashbord kuna vitu havifanyi kazi

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
6,816
Reaction score
8,809
Wandugu habari za Usiku

Hii ni Gari mpya Nissan

Nilipeleka gari kufanyiwa Interior Design ikiwemo na dashbord

Ila imerudi Taa ya Airbag inablink tuu, nimeuliza nikaambiwa kwa kua iliguswa itazima yenyewe, nimebaki nimeduwaa

2. Gari ilikua na system kwamba kama hujatoa handbrake basi haitaondoka itakuonyesha handbrake hujatoa

Au kama ukishuka ukasahau kuweka handbrake basi ukifunga milango kwa remote lock haifungi na itapiga kelele hujaweka sawa kitu ndani

Sasa baada ya hiyo ID hivo vitu viwili hapo juu vina tatizo havifanyi kazi

Naombeni kujuzwa ili kama kuna shida kubwa nirudishe gari wairudishe vizuri kama ilivyokua

Gari ni Nissan Dualis

Cc;

boeng
 
Kuwa makini na mafundi mkuu wengi hizi gari hawana uzoefu nazo maana mtu hadi anakuwa fundi unaweza kuta hajawahi kukutana na Nissan!
 
Nissan wana wakala wao kila mkoa.. jaribu kuwasiliana na mawakala (authorized) wanaweza kukusaidia pia, ila jiandae maana wana bei sana kufanya marekebisho
 
Ungepata kuona jinsi hizo gari zinavyokua assembled viwandani Wala usingejaribu kulichokonoa hiyo dashboard
Kuna vitu vinawekwa kwa kutumia robots arms very precise and accurate kiasi hata Yule the best mechanic hawezi kufanya ,
 
Hapa mkuu wangu ndo umefinalize uzi huu, hii kitu ya interior design imejaa Huko insta balaa, yaani mtu kanunua gari zuri [mpya/used from Japan] eti analipeleka huko wanaanza kubomoabomoa ndani, mara abarishe rim aweke size kubwa, mara sijui android radio, mara waweke taa za kumulika ndani iwe kama buggati, upuuzi mtupu, gari ikitoka pale inaanza kuwa na magonjwa kibao...
Hiyo taa ya airbag ni very sensitive, yasije Maputo yakashindwa kuchomoza during accident fanya hima bro.
Mafundi wetu hawa kuweka tinted tu jasho linawatoka balaa sembuse hizo wiring
 
Nimekuelewa sana
 
Back
Top Bottom