Baada ya Kufuta “Law School” Mawakili wasomi na walio bora watapatikanaje?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Sote tu Mashuhuda wazuri wa baadhi ya habari zinazotangazwa katika Vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii kuhusu Kesi zinazoendelea, ambapo kuna baadhi ya kesi nyingi hushtakiwa nazo watu pasipo hata wao kutenda makosa hayo.


Lakini Baadhi ya Mawakili wanaojua Vizuri Sheria na waliopita katika Taasisi hiyo na kupata mafunzo kwa vitendo wamekuwa wakifanya kazi zao ipasavyo na kwa weledi kuhakikisha walioonewa wanapata haki zao.

Ni Taasisi hiyo hiyo ndio iliyotoa Mawakili hao ambao watu wengi wamekuwa wakiwasifia.

Nadhani walioanzisha “ Law School” huenda kuna Mapungufu waliona na ndio maana wakaja na Mpango mzuri wa kuhakikisha kuwa Mwanasheria anakuwa ameiva kisawa sawa kwenye Taaluma hiyo.


Nimepitia sababu kadhaa za kuanzishwa kwa Taasisi hii Muhimu kwa nchi kwa maoni yangu nimeona ilikuwa bado ina umuhimu Mkubwa kwani ilisababisha Wanasheria wengi wajitume zaidi ili kufikia Viwango vya kutosha.

Ushahidi ni kwamba tunao Mawakili wazuri waliopata mafunzo kwa vitendo wakitetea watu walio onewa ba kubambikiziwa Kesi.

Tunatakiwa tusome na kuelewa misingi ya kuanzishwa Jambo fulani ndani ya Jamii.

Wazee walikaa na kuona kuna mapungufu ndipo kuamua kuanzisha kitu cha kusaidia Taaluma ya Sheria kuwa vizuri.

Tufikirie Upya.
 

Attachments

  • 2D2678A7-0458-4B92-A2CB-2E2A6B9A8E60.jpeg
    160 KB · Views: 11
  • CEB76FC2-D1DE-424E-8887-B37E0EA48145.jpeg
    165.2 KB · Views: 11
  • 6C8AE6E1-BBB8-455C-855E-FC25D465B252.jpeg
    122.7 KB · Views: 11
Moderator JamiiForums ni kwanini mnaruhusu nyuzi za upotoshaji?

Japo sikubaliani na uwepo wa Law School of Tanzania, ila siyo kweli kwamba taasisi hii imefutwa, isipokuwa sheria imebadilishwa kwamba taasisi ipanue Wigo wa mafunzo yake badala ya kutoa mafunzo ya uwakili pekee.

Marekebisho yamefanyika katika vifungu vya 2 na 5 vya The Law of Tanzania Act.
 
Unadhani mwaka mmoja unasoma nini cha zaidi? through practice and engagement, self-initiative and struggle ndiyo utakuwa wakili mzuri! Jiekee mkakati wa kusoma kesi tatu kila siku za court of appeal...., and the like, utona matoke yake
 
Toa tu maoni vzr ili kila mtu aelewe
Unadhani mwaka mmoja unasoma nini cha zaidi? through practice and engagement, self-initiative and struggle ndiyo utakuwa wakili mzuri! Jiekee mkakati wa kusoma kesi tatu kila siku za court of appeal...., and the like, utona matoke yake
sawa Mwanasheria wangu
 
Law School of Tanzania haijafutwa na utaratibu ni ule ule, ili uweze kuwa Wakili wa kujitegemea, wakili wa serikali au hakimu lazima ukasome law School au ufanye kazi kwenye vitengo vya sheria serikalini kwa miaka 10 ndio utakuwa wakili.
 
Mtoa mada ulikuwa ndotoni kwamba LAW SCHOOL kimefutwa?.
 
Law School of Tanzania haijafutwa na utaratibu ni ule ule, ili uweze kuwa Wakili wa kujitegemea, wakili wa serikali au hakimu lazima ukasome law School au ufanye kazi kwenye vitengo vya sheria serikalini kwa miaka 10 ndio utakuwa wakili.
Asante kwa ufafanusi maana mtoa mada alipotosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…