Baada ya kufutiwa kesi ya Uhujumu Uchumi, Raia wa China watoka Nduki mahakamani

Baada ya kufutiwa kesi ya Uhujumu Uchumi, Raia wa China watoka Nduki mahakamani

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia kesi ya uhujumu uchumi na kuwaachia huru wafanyakazi sita wa kampuni ya meli ya Sinota Shipping Company waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na ndege mmoja aina ya tausi.

Washtakiwa hao ambao wote ni raia wa China ni Jin Erhao (35), Chengfa Yang (49), Ren Yuangqing (55), Shu Nan (50), Chen Shinguang (45) na Gu Jugen (57) wote wakazi wa mtaa wa Sokoine, Ilala jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa baada ya kuachiwa walitoka mahakamani huku wakikimbia na kupanda gari kisha kuondoka.

Mwananchi
 
Wakikumbuka mazingira ya mahakamani chini ya ulinzi, na jela chini ya ulinzi, familia zao walizoziacha China, halafu ghafla mnaambiwa mko huru kukimbia ni lazima tena inawezekana safari ya kurudi China imeshaanza kwa miguu, ndege watapandia mbele ya safari.
 
Hawakuamini macho yao kwa experience ya maisha ya China kesi ya uhujumu uchumi ni kufa kwa shaba, sumu au kunyongwa..walifikiri ingekuwa hivyo na huku alipowahi kuishi Mwendazake
 
Ila Hapa bongo kuna mashtaka mengne ya ajabu yani mtu unamweka mahabusu kisa tausi kweli itahitajika miaka mngne 300 kufikia level ya wenzetu
 
Washtakiwa hao ambao wote ni raia wa China ni Jin Erhao (35), Chengfa Yang (49), Ren Yuangqing (55), Shu Nan (50), Chen Shinguang (45) na Gu Jugen (57) wote wakazi wa mtaa wa Sokoine, Ilala jijini Dar es Salaam.
Watu watano tausi mmoja lazima mhusika awe mmoja, anywaya hkauna hata kavideo??
 
Ila Hapa bongo kuna mashtaka mengne ya ajabu yani mtu unamweka mahabusu kisa tausi kweli itahitajika miaka mngne 300 kufikia level ya wenzetu
Inatofautiana nini na Viwanja vya ulaya unapokamatwa kwa kukutwa na kobe au vinyonga? Kuna maswali yanatokana na makuzi yako huko porini ulikowalima manati ndege wote mbele yako. Yaani unaona ni mzaha tu!
 
Washtakiwa baada ya kuachiwa walitoka mahakamani huku wakikimbia na kupanda gari kisha kuondoka.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kama nawaona vile
 
Haina kutembea kwa kudeka. Ni mbio kali kama Nyambui. Mbio zao ni original kabisa hata India huzipati.🤣🤣🤣🤣
 
Yani mtanzania akikutwa na nyara za serikali anafungwa maisha ila mchina anaachiwa huru
 
Back
Top Bottom