Baada ya kugundua Google chrome inakusanya taarifa zangu nyingi niliwahama, ni mwaka wa pili sasa natumia Brave Browser.

The best browser
 
Ndugu.. Google wakufanyie espionage kwa kipi hasa.. una kipi ww cha kufatiliwa taarifa zako na goggle?

Yale yale ya wapuuzi wachache wanonunua IPHONE wakisema ina security ya data zao.. unajiuliza kwa kipi hasa walichokuwa nacho mpk wazingatie security.. utakuta videos za snapchat.. tu.
 
Hii ni Kama indirect free kick.
Mnaitwa wateja( User ) na hamnunui kitu bali unauzwa Mana Jf ipo connected na Google.
Asanten Feeders wa Chat GPt.
 
Hapa solution achana na internet ili upate usalama unaouhitaji. Kuhamia browser nyingine ni KUOSHA MAJI KWA KUTUMIA MAJI 🤣🤣🤣
 
Hakuna mtu anaetaka kuchunguzwa, google wanarahisisha hata watu wengine wakifanikiwa kuingia kwenye email wanapata taarifa nyingi zinazorekodiwa na google.
 
Taarifa zako zina umuhimu gani hata uhangaike kuzificha?
 
Taarifa zako zina umuhimu gani hata uhangaike kuzificha?
Hio chrome ukiitumia mtu anaweza kujua hata user name yako ya jamiiforums akipata access ya email yako.

Kumbuka mapolisi wakiweza kupata access ya laini yako tu wanaweza kureset passwrd ya email yako, hapo mchezo umeisha wanaweza kuziona username na apassword zote za mitandao tofauti tofauti.
 
Kivipi wanapata access ya laini yangu ?

NA ni kivipi wakiwa na namba za simu watapata email yangu,naona umeirudia sana ebu ielezee kidogo mkuu
 

Mosi ukitumia tu internet hayo unayo yaogopa yapo wazi... hujui chochote kuhusu Brave wanafanya nini

Pili unanini cha kuficha hadi uogope Google kuhifadhi data zako?

Tatu unaongea kirahisi sana kwamba mtu aki pata tu access ya email au sim card yako basi kapata password zako zote..... sio kweli, depends na settings zako

Nne mambo mengi uliotaja kuhusu Google kuhifadhi ni hiari yako na sio lazima

Mwisho matangazo ndio kipato chao so get used
 

As long as you didn't design the browser, I bet you, you are not safe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…