Baada ya kugundua hutoishi milele, umechukua hatua zipi?

Baada ya kugundua hutoishi milele, umechukua hatua zipi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Chochote chenye mwanzo huwa kina mwisho.

Na wewe kama ulizaliwa, hutofikisha miaka 100 ya kuishi hapa duniani.

Ni muhimu kufahamu ya kuwa, na wewe una mwisho wako.

Kwa upande wangu, baada ya kuligundua hilo; nimekuwa nikiishi kwa kutenda wema sana bila kuwakwaza wengine.

Nimeacha mambo ya ujuaji ujuaji, na kutafuta mambo yanayonipa furaha zaidi.

Nimekuwa ni mtu wa kutembe tembea hapa na pale, viwanja vya hapa na pale n.k; lengo ni kujipa furaha.

Huwa sijibani kwenye kula kwa sababu yoyote ile, kwa sababu siku yangu ya mwisho sitaondoka na majengo wala mali yoyote ile.

Nikiona warembo wazuri ndio kabisaa, mwili unaishiwa nguvu.
Nitatumia akili na maarifa angalau awe karibu yangu; lengo ni kujipa furaha hapa duniani.

Je, kwa upande wako, baada ya kugundua hutoishi milele umechukua hatua zipi?​
 
Nmeachana na zile kelele za watu wa dini kwamba dunian tunapita hivyo raha na kula starehe hazina maana tusubiri maisha ya uzima huko mbinguni, ambako hakuna ushahidi kama kweli kuna raha ama kipigo.

Raha jipe hapa hapa dunian, kula bata kwa uwezo wako, watendee mema wengine as if unajitendea wewe mwenyewe, ishi maisha kwa furaha na si kumfurahisha mwingine.

Kwanini uishi kwa mateso kuyasumbukia maisha ya mbinguni usikokujua?, maisha ndio haya haya, acheni kujibana bana na kujitesa, wengine mnaishi kwa mateso pesa zenu wenyewe lakin zinawapa stress, kula bata wewe usijitese kama vile utaishi milele.
 
Baada ya kugundua kwamba sinto ishi milele....
Niliamua nisijenge nyumba njiani, maana duniani tunapita...🤨
Sasa kwanini nihangaike kujenga njiani....🙄
Usikute unamatumaini ya kupata yale majengo wanayohadithia yanapatikana mbinguni, kula raha lakini usitumainie kupata raha mahala pengine tofauti na dunian,
 
Back
Top Bottom