benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Sote tunafahamu kuwa katika mwaka wa kwanza wa uongozi wa Rais Samia Suluhu, Serikali imefanikiwa kujenga vyumba vipya vya madarasa 15,000 kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari pamoja na shule za msingi (shule shikizi).
Mwaka uliokwisha (2022) Serikali imejenga vyumba vya madarasa 8,000 kwa ajili ya wanafunzi wa Sekondari wanaoanza masomo Januari 2023. Ikumbukwe wanafunzi hawa ndio zao la kwanza la wanafunzi walioanza darasa la kwanza kwa elimu bure kwa ruhusa ile ya mwaka 2016 na hii inakuja na ziada ya wanafunzi 400,000.
Kazi kubwa imefanyika kwenye ujenzi wa MIUNDOMBINU lakini ni wazi kuwa "next move" inapaswa kuwa UWEKEZAJI na kutoa AJIRA kwa HARAKA na UKUBWA kwa walimu kuendana na ongezeko la wanafunzi wanaofikia 1,073,941 mwaka huu 2023.
Serikali imeajiri walimu wa sekondari 3,000 mwaka 2021 na wengine 4,800 mwaka 2022 hii inatupa jumla ya 7,800. Tukijumumlisha na idadi ya Walimu waliokuwepo mwaka 2020 (Kwa mujibu wa BEST) ambao ni 84,614 ni wazi kuwa sasa kuna walimu takribani 92,414 kwenye shule za Sekondari 2023.
"KWA NAMBA HIZI NI WAZI KUWA BAADA YA KUJENGA MADARASA SASA NI ZAMU YA RAIS SAMIA KUWEKA KIPAUMBELE KATIKA KUBORESHA ELIMU (UBORA WA ELIMU) NA HILI SASA LINAHITAJI WALIMU BORA WA KUTOSHA, IDADI YA VITABU NA VITENDEA KAZI PAMOJA NA VITI NA MADAWATI ILI SASA MATUNDA YA UWEKEZAJI ULIOFANYIKA YAANZE KUONEKANA"