Baada ya kukaa masaa matatu kwenye foleni, nauliza, hatuwezi kujenga flyover juu ya Mfugale bridge?

Baada ya kukaa masaa matatu kwenye foleni, nauliza, hatuwezi kujenga flyover juu ya Mfugale bridge?

Mi mwenyewe nimepita sasa hivi.
Waliamua kujijengea wenyewe wakitoka airport wapite kiulaini.

Mi nadhani wangeteneza roundabout buguruni ili kuruhusu magari kutoka tazara yawe yanasogea haraka.

Kwa sasa traffic police wa tazara akiruhusu magari kuja buguruni, wa buguruni anakuwa ameyazuia yanayotoka tazara. Hawana mawasiliano. Kwa hiyo, pale kwa mfugale yatavuka magari machache tu na foleni ya buguruni inakuwa darajani tayari.

Roundabout buguruni ingesaidia sana kama pale ubungo.

Au hadi awepo mchina?
 
Mradi wa Tazara ume jengwa sivyo kabisa. Wakuu walitaka Jina tu , Ego inawasumbua.
Mradi ulikua ni Change over...sio Bridge. Tazara ilikua hakuna gari ina simama kila gari inapita juu chini .
Leo mradi huu haukusaidia lolote foleni ya magari makubwa yatokayo Bandarini.
Masaa yanayo potea pale ni mengi sana.
Watu wamekimbilia kupeana majina tu lakini zero


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Tatizo Hakuna connection kati ya daraja na hapo Junction ya Buguruni.

Panaleta bottleneck effect jam inahamia Buguruni
Yaani unaweza ukatamani umcharaze kiboko yule Traffic wa pale Buguruni, ni vyema wakatumie radio calls ili ku-synchronise uitaji wa magari kati ya traffic wa Tazara na yulewa Buguruni, haiwezekani wa Tazara anaruhuzu magari halafu wewe unayazuia, halafu wa Tazara akiyazuia wewe ndio unayaruhusu, sasa maana yake nini hiyo? nadhani mtu bila kuwa na degree asiruhusiwe kuongoza magari.., ni ujinga huu..!!!
 
Foleni ya sehemu hii inachangizwa na vitu viwili kwanza malori yanayotoka bandarini ukiona umefika njia hii pita service road kuanzia pale sokota utapitia nyuma huku kwenye maduka ya hardware utokee karibu na TCC kisha ingia nyerere rd au pitia njia ya mchicha kutokea magorofani au kuna rough road pale njia ya wizara ya kilimo kisha ingia nyerere road pili uwepo wa traffic police tazara junction na buguruni sijui hawa jamaa wana watu wao wanawavusha kutoka town yaani upande huu wa bandari zikizidi sana ni dakika mbili kuvuta na kiukweli taa zinafanya vizuri kuliko hawa jamaa either way


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom