Ushauri:- magari yote yanayotoka gongo la mboto kwenda mjini kupitia barabara ya Uhuru yote yapite daraja la mfugale, kisha barabara ya buguruni Rozana inyooshwe kwenda barabara ya Nyerere ikiungia pale NBC, magari kutoka Tabata na Kwa Mnyamani ndiyo yapite buguruni shell kufuata barabara ya Uhuru kwenda mjini. Magari kutoka Gongo la mboto kwenda Ubungo tu ndiyo yakunje pale tazara kwenye daraja la Mfugale, pale buguruni shell kutoka tazara magari yasipinde kulia kufuata barabara ya uhuru. Abiria wote kuelekea Gongo la mboto kutoka mjini wapande na kuteremka kwenye kona ya Rozana.
Abiria kutoka Ubungo kwenda Gongo la mboto na mbagala ndiyo wapande na kuteremka buguruni shell kituo cha sasa.
Magari yanayotoka mbagala kwenda Rozana nayo yaungane na yale yanayotoka gongo la mboto kwenye daraja la Mfugale.
Daraja la Mfugale liongezwe mpaka pale NBC ili magari yanayotoka Rozana yapite chini kuingia barabara ya Nyerere.
Nina uhakika foleni ya Tazara kutoka bandarini na mbagala itapungua.
Injinia Mfugale weka mchoro.