Baada ya Kukamatwa na TAKUKURU Shaffih Dauda ajitoa kugombea Ujumbe TFF

Pole sana shafii
Muhulize
Mohammed Ally wazamani KTN alivyoumbuka kwenye Zoezi La Kupata Nafasi yakugombea ubunge

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi ni Muhulize au Muulize? Sipendi Watanzania ambao lugha Kuu yao ni Kiswahili halafu hawaijui ila Sisi ' Wageni ' ndiyo tunaijua vizuri kwa Kuiongea na Kuiandika.
 
hahaha Pamoja na kujitoa anatakiwa kujua kuwa TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi kama kawaida na ndio maana wameporwa simu zao...
Ukweli ni kwamba huko TFF kuna mianya ya kupiga pesa ndio maana alitaka kwenda....anayo yasema ameyafahamu leo?
 
Wapi nimeonyesha hayo ' Mahaba ' Kwake? Pumbavu!
Hehe..huyo ilikuwa lazima awe disqualified hata ka asingejitoa maana keshakiuka taratibu, eti ndondo Mwanza ndo imewakutanisha, kiongozi wa Dsm kilimpeleka nini pale? vipi wa Mbeya? wa Shinyanga? na vipi wa Simiyu? kweli ilikuwa bahati mbaya ile? yote ilikuwa ya kutia ndani tu.
 
Ana elimu gani ya Uandishi wa habari?

Hana Elimu yoyote ya Uandishi wa Habari na Utangazaji ila Kitaaluma ' Jamaa ' ni ' Mbobezi ' wa masuala ya IT akiwa kafanya Degree yake ya Computer Science pale IFM kisha Post Graduate yake kafanya Finance na Accounting isipokuwa huku katika Media alijiongeza tu ' Kiaina ' hasa kipindi kile alipoanza ' Kuchambua ' mipira baada ya kuwaiga ' Wakongwe ' akina Dk. Leakey Abdallah na Yule Sapi Mkwawa.

Aliyemtambulisha na kumfunidisha masuala ya Utangazaji na hadi kumpigania ale ' Shavu ' Clouds Media Group ni aliyekuwa ' Mshikaji ' wake wa siku nyingi Mtangazaji na Mchambuzi wa Michezo wa Efm Ibrahim Masoud ' Maestro ' ambaye hata hivyo sasa wawili hao ni ' Maadui ' wakubwa japo penye Watu huchekeana. Chuki yao kubwa ilitokana na Kitendo cha Shaffih Dauda kumuibua Bwana Said Selemani a.k.a Mbwiga wa Mbwiguke na kuanza kumtumia katika Kipindi cha Michezo cha Sports Extra na kumtambulisha katika ' Fursa ' zingine kitendo ambacho kilimfanya Mbwiga akubalike haraka kitu ambacho kilimkera mno ' Maestro ' ambayo ni Mtu mwenye hulka ya kupenda ukubwa na kutukuzwa.

Chuki za ' Maestro ' kwa Mbwiga Mbwiguke zilizidi kiasi kwamba Shaffih Dauda hakupendezwa nazo hivyo pakatokea sintofahamu kidogo hali iliyosababisha ' Maestro ' kususa na kuomba likizo kumbe huku nyuma alikuwa anafanya mipango ya kuhamia Radio ' hasimu ' ya Efm.

Moja ya ' dharau ' kama siyo ' roho mbaya ' ambayo Ibrahim Masoud ' Maestro ' alikuwa akimfanyia Mbwiga ni kila ambao Timu ya Mpira wa Miguu ya Clouds ilipokuwa ikienda kucheza mechi za Kirafiki alikuwa akimnyima namba kwa ' makusudi ' Mbwiga na kama hiyo haitoshi hata katika zile ' Posho ' Mbwiga alikuwa hapewi hata senti tano hali ambayo ilipelekea sasa si tu kumuudhi Shaffih Dauda bali hata ' Watangazaji ' wengine wa hicho Kipindi ndipo ikaonekana kwamba ' Maestro ' hatoweza kuishi vizuri hapo na wenzake na kuamua ' Kusepa ' zake Efm.

Kadri ambavyo ' Maestro ' alivyokuwa akimchukia ' Mbwiga ' ndiyo kwanza alikuwa kama vile anamfanya akubalike na Wasikilizaji na Watu wengi hasa kutokana na ' hulka ' yake ya kupenda ' Kuchekesha ' na ' Kutania ' sana hali ambayo huwachanagamsha wengi. Na kama mtakumbuka hata ile siku tu ambapo ' Maestro ' aliondoka rasmi CMG ' Mbwiga ' alisikika redioni akisema namnukuu " Woyooooooooooo Paka sasa kaondoka na Panya tunatawala.....Unamchezea Mzaramo Mbwiga Weye........Woyooooooooooooo.....tema mate kushoto unafukia kulia " mwisho wa kumnukuu Mbwiga.
 
Vipi kuhusu mlungula uliye toa na sasa unajivua gamba°?unajua uadilifu ni kitu muhimu kwa jamii,,,utashika mangapi mkuu jaribuni kukinai kwa kile ulicho nacho ebooooo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichokuuma ni nini hadi utumie neno kali hivyo?

Anyway, swali la msingi lipo pale pale...ametoa rushwa au hajatoa?.

PUNGUZA MAHABA KWA 'CMG' ili uelewa mambo mengi.

Sent from my SM-J120F using JamiiForums mobile app

Kama neno ' Pumbavu ' ni neno Kali nadhani leo hii Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ( 3 ) Mzee Benjamin William Mkapa ' Genius ' angeshashtakiwa na hata kuhukumiwa kwani ni neno ambalo hulipenda kulitumia sana kwa ' Wapumbavu ' wenzako ila mpaka leo ' anadunda ' zake tu. Kama haitoshi neno hilo hilo la ' Pumbavu / Pumbafu ' limetumika na Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake Kitakatifu cha Biblia mara 22 hivyo najivunia kuwa siyo neno baya kwakuwa hata aliyetuumba amelitumia vilivyo.

Kuniuliza kwamba ama Dauda alitoa Rushwa au hapana naona ni muendelezo wako ule ule wa ' Upumbavu ' niliouona Kwako kabla kwani kama ungekuwa una ' akili ' au ' IQ ' kubwa tu usingeuliza hili swali Kwangu wakati unajua fika kwamba tayari TAKUKURU / PCCB wanalifanyia Uchunguzi na Kisheria / Kimamlaka wao ndiyo wenye dhamana nzima ya kutuambia ukweli wote wa mambo Sisi Watanzania na hasa Wadau wa Michezo.

Halafu nikiwadharau kuwa hamjui ' Kufikiri ' mnanikasirikia na kuninunia.

Mwisho kwa faida yako tu ni kwamba........

Mjinga / Ngumbaru huwa anafundishika
Mpumbavu / Popoma hafundishiki ng'o hadi Kiama

Kila la kheri.
 
Maneno ya kwenye kanga hayo,anzisha kundi la taarab ili ukashambulie jukwaa.Wenye akili kubwa tunaongea maneno machache tu,bila matusi.
Ungejua kuwa kuna mamlaka 'TAKUKURU'usingekuja na mafuta kujaribu kumpamba mtuhumiwa.Funga mdomo.

Sent from my SM-J120F using JamiiForums mobile app
 
Thanks Kwa ufafanuzi bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hopeless Human being.
 
Kwani uchambuzi wa michezo ni kazi haramu?
 
Dah, aisee we jamaa mbishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…