PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Klabu ya Simba imetangaza kuwa mashabiki wake wataruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 De Agosto utakaochezwa Oktoba 21, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo Oktoba 20, 2026, uamuzi huo umefikiwa baada ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya klabu ya Simba na 15 de Agosto, ambapo mashabiki walikubaliwa kuingia uwanjani.
Simba imesema hatua hiyo inalenga kutambua umuhimu na mchango wa mashabiki wake katika mchezo huo, huku ikiwashukuru kwa juhudi walizofanya kuhakikisha wanapata nafasi ya kushuhudia pambano hilo.
Aidha, klabu hiyo imetangaza kuwa mchezo huo utaoneshwa kwenye runinga kubwa (Big Screen) katika maeneo ya Mwembeyanga na Mbagala Zakheim, huku ikieleza kuwa taarifa za viingilio vya maeneo hayo zitatangazwa baadaye.