Baada ya kumbamiza Mnamibia, Mwakinyo apanda chati za ubora duniani hadi namba 13

Ile inaitwa Boxing na sio Fighting...

Kama ni kutaka kujua mbabe wa taifa basi Kiduku apigane tu na mtu yoyote yule kwa kanuni za kimtaa...

Lakini kama ni boxing, mpiganaji aliye juu huwa ndiye muamuzi wa mapambano yake
shukran kwa elimu chief matumain yangu ni kua Itasaidia Wasiojua sheria za boxing wale wapenzi wa Nan mbabe
 
Ile inaitwa Boxing na sio Fighting...

Kama ni kutaka kujua mbabe wa taifa basi Kiduku apigane tu na mtu yoyote yule kwa kanuni za kimtaa...

Lakini kama ni boxing, mpiganaji aliye juu huwa ndiye muamuzi wa mapambano yake
Tatizo hawa vilaza wa mkata kimeo wanamsikiliza kilaza mwandamizi babu Tale bingwa wa kugonga meza bungeni
 
Eti Babu Tale anaomba pambano na mbeba tofali wake kama anaagiza supu ya utumbo bar.
😂😂 Hajui kuna taratibu Champez! ⭐️ Alimbamiza Sam nyumbani kwao akawa hapo alipo yeye anataka apate kamseleleko na yeye atafute wa kwenda kumgeuza ngazi halafu aje na mkanda uwekwe mezani wagombanie Champez! ⭐️ hapigan bila kuwepo mshipi (mkanda)
 
Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amepanda rank na kuwa nafasi ya 13 katika Ubora wa Mabondia duniani katika uzito wake wa super welterweight.

Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 24 aliyokuwa awali kabla ya kumpiga Bondia Julius Indongo wa Namibia kwa TKO round ya nne kwenye pambano la round 12 lililochezwa Ubungo Plaza September 3 2021

CC Ayo tv
kitu kinachoshangaza wengi ni namna mapambano yake ya hapa bongo yanayosimamiwa na wabongo, yanavyositishwa ghafla wakati bondia pinzani bado ana nguvu za kuendelea. wamelalamika sana mitandaoni watu, nashauri kwenye pambano lingine, wamuache apige mtu hadi adondoke chini asiamke kwa muda ili heshima isitiliwe mashaka. kwa mchezo wa juzi, wengi wanasema refa alisitisha mapema wakati indongo bado alikuwa na nguvu za kuendelea yaani haikuwa KO halali.
 
Kuna mlevi mmoja apa anauliza eti kwanini kiduku asitafute namna ya kupanda mwenyewe bila kupigana na mwakinyo
 
mwakinyo-2.jpg

BONDIA Mtanzania Hythani Hamza Halfan ama maarufu kama Hassan Mwakinyo wa uzito wa Super Welter amepanda kutoka nafasi ya 24 hadi nafasi ya 13 katika viwango vya ubora duniani huku akiwa namba moja Afrika.

Mwakinyo anashikilia ubingwa wa Afrika (ABU) kwa uzito wa super welter. Mwishoni mwa juma alitetea ubingwa wake kwa kumpiga Julius Indongo kutoka Namibia.

Alhamdulillah, Tumepanda tena. Nimepanda hadi nafasi ya 13 kwenye viwango vya ubora duniani kutoka nafasi ya 24. Na Nimeendelea kuwa Bingwa wa ABU na Bondia namba 1 Africa,’’ aliandika Mwakinyo katika ukurasa wake wa Twitter.

Hassan Mwakinyo alijitosa katika ulingo wa ngumi za kulipwa tangu mwaka 2015, na amewahi kushikilia mikanda kadhaa ya ubingwa ikiwemo ubingwa wa WBA pan African.

Sasa atafute mapambano nje ya nchi tuone akipigana kwa majaji wasio wa nyumbani hali itakuwaje, atafute na mabondia wenye viwango na umri wao usiwe umeenda sana.
 
Tutamkamata tumlete kwa nguvu ulingoni azichape na Kiduku asilete janja janja
Wee jamaa khaaaaa nyie ndo mnafanyaga watu wajaribu ili kuwa prove wrong halafu bahati mbaya wanapigwa sio kwamba hawawezi nop kwasbb wanakua na kitete.
 
mwakinyo-2.jpg

BONDIA Mtanzania Hythani Hamza Halfan ama maarufu kama Hassan Mwakinyo wa uzito wa Super Welter amepanda kutoka nafasi ya 24 hadi nafasi ya 13 katika viwango vya ubora duniani huku akiwa namba moja Afrika.

Mwakinyo anashikilia ubingwa wa Afrika (ABU) kwa uzito wa super welter. Mwishoni mwa juma alitetea ubingwa wake kwa kumpiga Julius Indongo kutoka Namibia.

Alhamdulillah, Tumepanda tena. Nimepanda hadi nafasi ya 13 kwenye viwango vya ubora duniani kutoka nafasi ya 24. Na Nimeendelea kuwa Bingwa wa ABU na Bondia namba 1 Africa,’’ aliandika Mwakinyo katika ukurasa wake wa Twitter.

Hassan Mwakinyo alijitosa katika ulingo wa ngumi za kulipwa tangu mwaka 2015, na amewahi kushikilia mikanda kadhaa ya ubingwa ikiwemo ubingwa wa WBA pan African.

Hongera Mwakinyo
 
Wee jamaa khaaaaa nyie ndo mnafanyaga watu wajaribu ili kuwa prove wrong halafu bahati mbaya wanapigwa sio kwamba hawawezi nop kwasbb wanakua na kitete.
Mwakinyo asijifiche kwenye professionalism ,tutamleta kimabavu stejini
 
Ile inaitwa Boxing na sio Fighting...

Kama ni kutaka kujua mbabe wa taifa basi Kiduku apigane tu na mtu yoyote yule kwa kanuni za kimtaa...

Lakini kama ni boxing, mpiganaji aliye juu huwa ndiye muamuzi wa mapambano yake
Kama anakataa kupigana na walio chini yake hata yeye asingeweza kupata pambano la kupigana na walio juu yake maana kama wangekuwa na mawazo kama yake wasingekuwa wanakubali kukipiga naye...
 
[emoji23][emoji23] Hajui kuna taratibu Champez! [emoji294]️ Alimbamiza Sam nyumbani kwao akawa hapo alipo yeye anataka apate kamseleleko na yeye atafute wa kwenda kumgeuza ngazi halafu aje na mkanda uwekwe mezani wagombanie Champez! [emoji294]️ hapigan bila kuwepo mshipi (mkanda)

Wabongo wana fikiri watu wana pigana
Pigana tu kizembe
 
Kama anakataa kupigana na walio chini yake hata yeye asingeweza kupata pambano la kupigana na walio juu yake maana kama wangekuwa na mawazo kama yake wasingekuwa wanakubali kukipiga naye...

Hata mimi kuna wakati nilikuwa na fikra kama hizi zako mkuu, lakini baadaye nikaja kujua inategemea umeachwa hatua ngapi na mtu aliye juu yako ili aweze kukufikiria kukupa nafasi ya kurushiana masumbwi naye...
 
mwakinyo-2.jpg

BONDIA Mtanzania Hythani Hamza Halfan ama maarufu kama Hassan Mwakinyo wa uzito wa Super Welter amepanda kutoka nafasi ya 24 hadi nafasi ya 13 katika viwango vya ubora duniani huku akiwa namba moja Afrika.

Mwakinyo anashikilia ubingwa wa Afrika (ABU) kwa uzito wa super welter. Mwishoni mwa juma alitetea ubingwa wake kwa kumpiga Julius Indongo kutoka Namibia.

Alhamdulillah, Tumepanda tena. Nimepanda hadi nafasi ya 13 kwenye viwango vya ubora duniani kutoka nafasi ya 24. Na Nimeendelea kuwa Bingwa wa ABU na Bondia namba 1 Africa,’’ aliandika Mwakinyo katika ukurasa wake wa Twitter.

Hassan Mwakinyo alijitosa katika ulingo wa ngumi za kulipwa tangu mwaka 2015, na amewahi kushikilia mikanda kadhaa ya ubingwa ikiwemo ubingwa wa WBA pan African.

Angewataja hao mabondia walimzidi ubora. Kwa haki kabisa waandaaji wa mapambano ya mwakinyo na Class Ibrahim wanatuleteaga mabondia wa ajabu kabisa.
Ebu tuleteeni hiyo list ya hao mabondia bora 20 kwenye uzito anaopigana Mwakinyo tuone ni kina nani hao.

Kuna watu wanapiga ngumi nyie. Ooòhhh shauri yenu.
 
Tutamkamata tumlete kwa nguvu ulingoni azichape na Kiduku asilete janja janja
Hatutaki hizo tunataka heshima kutambulika duniani , ubabe mkagombanishe mbwa .
 
Back
Top Bottom