Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo!
Sisi tunatazama. Tunafuatilia kila kitu kwa ukaribu sana. Tunahakikisha hatutapitwa na chochote. Ingawaje kuna baadhi ya episodes hatuzielewi na kuzifanyia tathmini inachukua muda.
Katika mchezo wa Chess huo ndio napenda kuutumia katika mambo ya kisiasa. Kwa sababu unaakisi hali halisi ya Siasani.
Mchezaji huangalia kete za Mwenzake na zake. Lakini kwenye kucheza atacheza kete zake. Hiyo ni kanuni ya wachezaji wa kawaida.
Kwenye mchezo huohuo. Mchezaji mahiri haiishii kuzitazama kete za mwenzake bali huziwekea mitego na wakati mwingine huzicheza kete hizo bila adui kujua.
Kwenye Chess kuna mifumo na mbinu nyingi za kuhakikisha adui anacheza kete au mchezo unaotaka. Lakini mbinu kuu ni hizi tatu hapa:
1. FORCING MOVES(Kumlazimisha ajibu)
Hii ni hatua ya kwanza. Unacheza move ambayo mpinzani hawezi kuipuuza. Anaweza kuwa na majibu machache sana.
Moves kuu za forcing ni:
a) Check King iko hatarini, lazima ajibu ili kuokoa kete hii yenye nguvu.
c) Capture, unachukua njia muhimu na kumlazimisha aamue kama aachie kete au umiliki njia hiyo.
d) Direct threat — unatishia kumchukua Queen, kum-mate, au kushinda. Kwa sababu ukitishia Queen mchezo unaweza ukaishia hapohapo. Atacheza kete ambazo hakutaka kucheza. Na kete hizo amecheza kwa shinikizo Lalo.
Katika Siasa, mbinu ya kulazimisha mtu ajibu, ni mbinu inayotumika sana hasa Afrika na hususani hapa Tanzania.
Kwenye check king ni pale ambapo Unaleta hoja, kashfa, ushahidi, maandamano au changamoto ya kisiasa inayomlazimisha kiongozi ajibu hadharani.
Unapomu- attack kiongozi wa Chama kama Heche au Samia kwa kumpa kashfa fulani iwe ya kweli au sio ya kweli unatengeneza mazingira ya kukosa utulivu katika upande wa adui. Hata kama adui alikuwa na mipango mingine au kete zingine. Itampasa aziache na kulazimika kujibu hizo kashfa ambazo ni tishio kwa ushawishi wake. Hiyo ni check king.
Unatoa shutuma kiongozi fulani amefariki, au kuna mabilioni yanaliwa. Hata kama hayajaliwa itampasa wa upande wa pili ajibu hata kama angekuwa na kete nyingine.
2. Kumfanya achague unachotaka wewe hii kitaalamu wanaita Deflection Decoy.
Hapa ndipo unamshawishi/unalazimisha kete iondoke kwenye kazi yake ya ulinzi.
Mfano:
Mpinzani ana Queen inayolinda Rook. Unafanya threat(tishia) inayomlazimisha Queen hiyo ihame.
Queen ikiondoka → Rook inabaki bila ulinzi → unaichukua.
Iko hivi. Katika Chess kuna Kete inaitwa Queen ambayo inajukumu kubwa la kumlinda Rook. Unapotishia kete ya nguvu kama Queen usalama wa kete ndogo kama Rooks na pawns unakuwa mashakani.
Katika siasa, unatishia Kiongozi mkubwa na anapohama kwenye mfumo wake. Wadogo wa chini unaparamia. Hawa wadogo tayari ushawafanya hawamuamini mkubwa wao kwa kwa mbinu ya kwanza. Mbinu ya pili ni kumalizia kazi iliyoanzishwa na mbinu ya kwanza.
3. Kumfanya kila move iwe mbaya( ZUGZWANG)
Hii ndiyo mbinu ya juu zaidi. Hapa si lazima umtishie mate au kumshambulia moja kwa moja. unaweka mfumo ambao kila kete anayotaka kuicheza anaiona itamletea matatizo kibaya zaidi inakuwa zamu yake imefika na lazima acheze.
Mbinu hizo tatu zinetumiwa sana na CCM tangu 2015 mpaka hivi leo.
CCM iliona Tundu Lisu ambaye ni kiongozi Mkuu atawasumbua sana. Wakaona kete pekee ya kucheza ni kumtisha na kumfungia ili asiweze kuleta matatizo na kundi lililobaki litakosa muelekeo.
Unamuweka ndani, unazuia watu wasimuone. Kisha kete inayofuata ni mbinu ya Deflection. Ambayo hapa unamshawishi Heche ikiwezekana unamuwekea mazingira ya zugzwang. Yaani kumfanya Heche aone moves zake zinazofuata zote zimeharibiwa na Anamosa chaguo. Ni aidha ajisalimishe au akubali kucheza aumizwe polepole.
Unapofanya check King kwa kumzushia hoja Heche kwamba anafurahia Mwenyekiti wake Lisu kuwa Jela. Pia kusema amekula hela za Tone tone.
Kisha round hii kusema anazuia maridhiano wakati yeye ameridhiana ili apate Passport yake. Unagundua kwamba lengo la CCM ni lipi.
CCM ilijua kuwa itakuwa kazi rahisi baada ya kumweka Lisu ndani basi waliobaki ni kitonga. Lakini mchezo unawapa matokeo tofauti.
Kitu ambacho kwenye Chess ni muhumu kuliko vyote. Ni kuhakikisha adui yako hachezi kete zako.
Kwani akicheza kete zako ni kwamba utakabiliwa na internal conflicts. Na hii itapelekea kuanguka kwa Chama kutokea ndani.
CCM inajua hili. Kwamba kama wao kwa wao watakuwa maadui basi kazi ya Upinzani itakuwa rahisi.
Ndio maana Ndani ya CCM akizuka mtu yeyote au kundi lolote ambalo ni kinyume na Falsafa na Dira ya kiccm. Wanamuengue mapema.
Mbinu za kuiangusha CCM ni Mbinu ya Mchwa.
Kule Upareni kuna msemo usemao kidudu chehujie ndicho kila mbehu.
Msemo huo ukimaanisha, Mdudu mkimya, aliyenyamaza ndiye anayekula Mbegu.
Hauhitaji kelele, uroporopo, matangazo kuiangusha CCM.
CCM itaangushwa na Vidudu vyehujie. Naam vidudu vilivyonyamaza ambavyo hula kimyakimya.
Hata ndani ya CHADEMA wanaoiongusha CHADEMA ni wale wanaoaminiwa. Vidudu vyehujie. Wanakuja kugeuka dakika za jioni kabisa.
Unapomtathmini mtu kama Humphrey Polepole, Nchimbi, na wengineo ambao Nia yao ilikuwa kubwa kuliko mkakati waliokuwa nao.
Hii ikawafanya kwenye Drafti wakaliwa tutusa au kupigwa force king. Kulazimishwa.
Mbinu ya kuiangusha CCM ni kushambulia kutokea ndani kama kidudu chela mbehu.
Bila kelele.
Bila kuonyesha resistance.
Kwa sababu huwezi onyesha nguvu wakati huna nguvu au adui yako amekuzidi nguvu.
Lazima wewe upitie underground adui yako awe juu. Kama utajitokeza ni wakati wa Ambush ambalo uko 💯 a hundred percent unaenda kushinda kwa kupiga eneo nyeti kwa pigo moja tuu, na kama litahitajika la pili basi ni finishing
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam