Baada ya kumsikiliza mama wa Feitoto, ni dhahiri Fei na familia nzima wamerubuniwa

adriz Una akili nyingi bro....nmekuelewa na upande wa simba tumieni akili acheni kupindisha, huyu feisal kaleta tamaa, na mwisho wa tamaa ni Mauti. Asipokuwa makini feisal tunamzika mapema
 
Mzeee umemaliza yote
 
Kwanza hana shukran kipindi anaibuliwa si alifanya majaribio upande wa pili na wakampatia dau dogo, ila Yanga wakaja na kubwa wakati huo. Hadi anasaini mkataba wa pili dau liliongezeka hadi 4m.
Pia Timu inayotaka kumpatia dau kubwa kama wanamthamini hivyo wanashindwa nini kubisha hodi Yanga na kuomba transfer yake. Mnataka mpira biashara kwa kuoneana huruma hakuna kitu kama hicho.
Nguvu yako ya majadiliano kutokana na kiwango chako ndio kitakupa thamani zaidi muda huo wa kuongeza mkataba na si katikati ya mkataba
 
Poor reasoning

Mwambie Azizi Ki kuanzia leo awe ana chukua 4M kwasababu kuna timu ya majimaji ilikosa pesa ya nauli
Mkuu, makubaliano ya malipo hayaangaliwi wewe unauhitaji kiasi gani na hela, Bali kiwango ndio kinaamua. Wakati mshahara wake unatoka 1.6 kwenda 4, kwa wakati ule, waliona ni sahihi. Sasa kiwango kinapopanda, badala ya kusema unanyonywa, omba maboresho ya mkataba. Je,Fei alishawahi kuomba maboresho ya mkataba?
 
Poor reasoning

Mwambie Azizi Ki kuanzia leo awe ana chukua 4M kwasababu kuna timu ya majimaji ilikosa pesa ya nauli
Aziz ki hakusaini mkataba wa kulipwa milion 4 kwahyo analipwa kulingana na mkataba wake.. kinachomaanishwa hapo fei anasema 4Mil ni ndogo mpaka alikua ana kula ugali na sukari..ndomana huyo kahoji milion 4 ndogo ki vp kama maji maji wote walikosa milion 1 ya kuwarudisha kwao!
 
Kuongeza maslahi hakukataliwi na ni makubaliano ya pande mbili,kama unaona maslahi ni madogo omba kuuzwa kwa kufuata taratibu sio kutaka kuondoka kihuni, ukiona shida subiri mkataba wako uliosaini mwenyewe ukiwa na akili timamu uishe uende unapotaka.
 
Mmmh hapana. Kwa Tanzania hii ya leo, huo ni mshahara mdogo kwa mchezaji tegemeo wa timu kama Yanga huku kwenye timu hiyo hiyo kuna wachezaji wanalipwa zaidi ya milioni 20, gap hiyo ina matatizo.

Linganisha vipato vya kina Diamond, Harmonize na Marioo ndiyo level anazotakiwa kuingiza mchezaji kama Feisal kama mmoja wa mastar wazawa. Hii najumuisha mshahara na mazagazaga mengine anayolipwa ndani na nje ya club.

Kiukweli kwa mpira wa sasa, kiwango cha chini cha malipo kwa timu kama Yanga au Simba kinatakiwa kuwa around milioni 8-10 na hii ni kwa wale wachezaji ambao ni wasugua benchi.
 
Feisal alichukua maamuzi ya ghafla kwa sababu watu waliomtaka walimwaminisha kwamba ishu ni ndogo tu...

Lakini mambo hayakua hivyo, kwenye mpira na usajili hakuna kitu kama hicho anafanya Feisal wafuatiliaji wa mpira wanajua hili

Dogo ni aombe yanga wasimkamie tu wasisumbuane nae manaa yanga hizi ligi ndo wanapenda Sana aisee na watamsumbua Sana sio kidogo
 
Wew
Wewe umeusoma huo mkataba au na wewe unanyesha ufupi
 
Poor reasoning kwaiyo kama kuna watu wanalipwa laki 5 na yeye ndo asiseme mshahara mdogo. Angalia value ya kile mtu anacho fanya sio kufananisha mshahara na watu wengine. Kuna watu wanalipwa million 10 na bado wanalalamika mshahara mdogo.

Back to the topic Feisal anahaki ya kulalamika it doesn't matter ametumia njia gani he's fighting for his life akilkosa maslahi mazuri kesho mkamkuta amechakaa nyie nyie ndo mtakae msema vibaya

Hili jambo ni lakuweka hisia pembeni na kuangalia uhalisia zaidi
 
Kuanzia leo, nimekutoa kwenye kundi la mbumbumbu. Nadhani wewe ndio Kolo pekee mwenye akili. Ilikuaje ukashabikia hilo li timu la mbumbumbu lakini?

Feitoto na familia yake wanadhani haya mambo yanaendeshwa kwa emotions na kutia huruma. Hawajui kama haya mambo yanaendeshwa kwa mikataba inayotambulika kisheria.

Huwezi kusaini mkataba wa milioni nne, alafu ukalipwa milioni kumi. Utalipwa hiyo milioni nne, mpaka mtakapoweka makubaliano mapya. Kusema ulikula ugali na sukari, haibadilishi makubaliano ya mkataba wako wa kulipwa milioni nne!
 
Soka sio kama siasa kwamba mzawa ndio mwenye haki, Soka ni biashara ndio maana hata huko tunakoiga mzawa sio hoja ila kipaji na mchago wa huyo mchezaji mwenyewe kwenye hiyo biashara.
Naamini unajua kina Ronaldo, Messi huko waliko wanalipwaje kwa wiki ukilinganisha na Wazawa.
Fei ana mkataba ambao kwa kipindi anausaini thamani yake ilikuwa hiyo anayolipwa, angesubiri mkataba mwingine au kufata taratibu za kuvunja mkataba ili aende sehemu anayoona ina maslahi makubwa kitu ambacho kila mtanzania anataka iwe hivyo, ila uhuni huu haukubaliki kwa kisingizio cha kuonewa.
 
Poor reasoning

Mwambie Azizi Ki kuanzia leo awe ana chukua 4M kwasababu kuna timu ya majimaji ilikosa pesa ya nauli

Wewe inaonyesha ni wale wale
Mwili mkubwa akili kisoda
Ss hapo Aziz Ki anaingia vp ktk ishu ya Zanzibar fainest
 
Hivi unadhani mshahara wa SAKHO unalingana na wa KAPOMBE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…