Baada ya kushindikana kuwahamisha wapalestina, Gaza sasa kujengewa uwanja mpya wa ndege

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Jumuiya ya nchi za kiislamu OIC hapo juzi ilipitisha mpango wa kuijenga upya Gaza uliasisiwa na mawaziri wa nchi za kiarabu wiki mbilli zilizopita, Katika mpango huo jumla ya dola za Marekani bilioni 53 zitatumika kufanya ujenzi huo awamu kwa awamu.

Miongoni mwa miradi ya ujenzi huo ni pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa ndege ambapo sasa wapalestina chini ya mamlaka yao watakuwa huru kuingia na kutoka nchini mwao.

Mpango huo tayari umepelekwa kwa raisi Trump kupitia mjumbe wake wa mambo ya nje. Alipoulizwa kuhusiana na mpango huo ambao unapingana na kitisho chake chake cha awali cha kuifanya kivutio cha utalii,Trump amesema hakuna ambaye ana nia ya kuwahamisha watu wa Gaza.

 
Jirani zao watakuwa wanayumbisha ndege kila kukicha
 
isingekuwa ukichaa wa Trump hawa waarabu wasingefikiria kuwasaidia ndugu zao.
Hata mimi naamini hivyo.
Elsisi eti naye ndio amekuwa mbogo katika huu mpango.
 
US, Israel hawajatoa plan yoyote ile

Hiyo plan ya Misri na wenzao
 
Askari 75000 wa israel waliuawa au kujeruhiwa vita vya Gaza,na nusu ya reserve hawataki kwenda kuhudumu jeshini(yedioth ahronoth,hareetz)..hakuna anayetamani mbungi iendelee
Kuhusu za askari waliokufa na kujeruhiwa hilo sina hakika BUT kwamba askari wa Israel hawataki mbungi iendelee, hili nadhani sio la kweli, uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…