Baada ya kusikia vitu kama mchanga unamwaga batini usiku wa manane nimetoka nje kuangalia ila sioni kitu, nini tatizo?

Wachawi hao na hiyo ndio ishara yao,kuisikia mchanga unachururizika au muda mwingine vishindo kabisa juu ya dari.
 
Wajuaji hamkosekani.
 
Kama ingekuwa ni nyumbani kwako ningekushauri ufanye zindiko.

Watu huwa hawahamii kwenye nyumba walizozijenga bila kuzizindika.
 
Umenikumbusha jamaa yangu mmoja w kilundi aliniadisiaga stori. Kuna nyumba walipanga. Kukawa na kawaida mara nyingi usiku kusikia kishindo kikubw juu ya bati.

Wapangaji sametimes akikaa huulizana kama wanasikia hicho kishindo, wakasema wanasikia na itakuwa wachawi

Basi jamaa mmojawao akatengeneza shoti ya umeme, akaunganisha kwenya bati na akaweka plag standby. Basi siku moja usiku kikasikika kishindo kwenya bati basi jamaa faster aka place plag kikasikika kitu kama kinabiringika kikasiika kitu kimaanguka chini puuu!. Keshe yake wanasikia baba mwenye nyumba anaumwa kapata ajari sura yote imevimba
 
Sema tu usichanganye majini na malaika waliyoasi ni viumbe aina mbili tofauti mkuu, majini ndio hawa wenye kushiriki mapenzi,kuzaa na hadi kufariki kitu ambacho ni tofauti na asili ya malaika waovu.
 
Hao wanga ndo wanatua hivyo! Pole sana.... kama unaweza kachukue maji ya Baraka kwenye kanisa lolote katolic mwaga juu ya hilo paa- na chumbani.... usije wakakuchanja chale za Matako😂😂
 
Kama ingekuwa ni nyumbani kwako ningekushauri ufanye zindiko.

Watu huwa hawahamii kwenye nyumba walizozijenga bila kuzizindika.
Mpaka sasa nimeishi kwenye nyumba mbili za kujenga mimi,sijawahi kufanya zindiko,kwenye nyumba niliyopo nina kama mwaka sasa,sijawahi kuona kelele,shida yoyote wala nini,sikatai uwepo wa nguvu za giza ,ila siamini katika kufanya zindiko kwenye mji wangu
 
Hapo inategemea na maeneo unayoishi , circle ya watu ulionao maana siku zote mbaya hatoki mbali.
 
Hapo inategemea na maeneo unayoishi , circle ya watu ulionao maana siku zote mbaya hatoki mbali.
Hakuna kitu kama hicho,nyumba yangu ya kwanza wakati najenga kila mtu alishangaa,maana nilijenga karibu na mbibi ambaye anaogopeka sana pale kijijini ,but nimeishi kwa nyumba hiyo 9years bila shida
 
unafahamu mti wa mbaazi
 
ujue nyumba yako inachezewa na wachawi yaani dalili sio hizo tu ziko nyingi tu mfano: mapaka kulia usiku nyumbani kwko au dirishani kuota unachunguliwa dirishani watoto kulia sana usiku kwako nk.. Mkuu kama bado unyo hayo matatizo nitafute ili nipate kukutibia na kuondosha hayo matatizo.
 
Wenzake walipokuwa wanasoma habari za Contraction na expansion ulikuwa unasema tutatumia wapi huu ujinga. Leo bati linalia wakati wa contraction unasema wachawi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…