Baada ya kusoma vitabu zaidi ya 300, nimegundua kumbe nilitakiwa kusoma Biblia tu

Nimekuelewa ongeza hata katiba za nchi zote zimezingatia biblia fatilia muda wa kustaafu maaskofu na majaji wa mahakama
Katiba zote ni matokeo ya uwepo wa Biblia. Chochote ndani ya katika kinachopingana na kinachosisitiza Biblia kipengere hicho kinavunja katiba mama ambayo ni Biblia kauli za Mungu.
 
Kila kitu kinamtegemea mwenzake, hiyo ndio life cycle.
 
Maandishi ya Biblia hayana Logic.By the way Bible nayo ni mawazo ya watu kama mawazo yaliyo katika vitabu vingine.
Biblia ni kitabu pekee duniani ambacho maneno yake yananguvu ya kubadilisha mtu milele. Hutu tuvitabu twingine tunakupa hamasa tu lakini havina uwezo wa kukubadilisha kwenye dimensions zote.
 
Ila Bible unatakiwa uisome kwa kutulia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndio wanakuharibu akili.
Sijaona contradiction hata moja hapo ila nimeona watu ambao vichwa vyao ndio vinacontradiction na wanatikiwa waponywe vichwa kwanza kabla hawajapata tiba za Biblia.
Usiwaamini hao, niamini mimi itakusaidia sana.
 
Mimi nakuhurumia sana ila unajua fika mambo ya Mungu ni imani na sio physical things or reasoning?
Huyu tunaenda naye taratibu tu ni mtu mwema sio lazima aelewe kila kitu leo.

Mindset yake inatakiwa kufanyiwa spiritual fumigation. Akili yake ameruhusu ichezewe na wajanja wa dunia. Kila anachokisema huwa sio product ya fikra zake bali ni matokeo ya ulevi wa mijadala ya kumpinga Mungu kwa miaka mingi, na tatizo sio ulevi huo bali wapishi wa mivinyo aliyonyweshwa wamemzidi akili.

Ni mtu mwema tu tutaenda naye taratibu huku tunamfanyia mind detoxification kidogokidogo.
 
Nimekuwa naona jinsi unavyopambana kuwapinga wanaoamini uwepo wa Mungu.
Ni kwa sababu hajiamini au hana uhakika na huo msimamo wake, hivyo huko kupambana au kushambulia dini ni kitu chenye kumpa faraja. Silaha yake ni kutaka kuonyesha makosa ya vitabu vya dini ili kuhalalisha kutokuwepo kwa Mungu ila anasahau imani ziko nyingi sana na wengine hawaamini dini wala vitabu vya dini ila wanakubali uwepo wa Mungu.

Wakana Mungu wengi ukiangalia hoja zao utagundua matatizo yao ni ya kidini zaidi kuliko uwepo wa Mungu.
 
What a coincedence here!!! Umeshakata agano la kale lote mkuu?
Agano la kale ndio msingi wa Biblia.
Hasa Torah (vitabu vitano vya kwanza vya Biblia). Biblia yote imetokea hapo.

Kama hujui torati, maandiko lazima yakuvuruge hasa ukikutana na wavurugaji. Ila maandiko yote nayaamini. Hayana shida kabisa na yote yanaprinciples zilizo juu ya kitabu chochote duniani.
 
Kwamba naweza kujifunza Forex kwenye Biblia yaani Time flame, chart, lot size, take profits zote nazipata kwenye Biblia

Unamaanisha Mimi Product designer naweza jifunza Algment, typography, Contrast, prototype nk kwenye Bliblia

Yaani Mimi Naweza jifunza Grammer, Tense na kingereza kwa ujumla kwenye Biblia

Kwamba Mimi Developer naweza jifunza kuandika Lines za codes, Alogarithim, nikajifunza software za kuwanazo, laptop iwe na ukubwa gani nk

WHAT THINKING IS THIS
 
Kwanini usimuelekeze akasome biblia kwanza??
Hawa vijana wa kisasa wengi hawaamini Biblia. Promotions za kuishusha Biblia zimetanda kila kona. Sasa angalau aanzie huko duniani ili dunia imrudishe kwenye Biblia kama solution ya kila kitu.

Rabbi Daniel hana jipya zaidi ya kusoma biblia na kuandika Best selling books. Wenda akajifunza kitu kikamrudisha na yeye aangalie Biblia inaweza kumsaidiaje katika industry yake.

Najaribu kumtafutia appetizer ya kuirudisha mindset yake Bibleward.
 
Kuiamini biblia inabidi uwe na tatizo la akili kwanza
 
Mbona hivi ni vitu vidogo sana mkuu unataka kuvukuza sana.

Bible inakuba basic, forex ipo tangu enzi za Ibrahim. Yusuph Misri kacheza sana na concept za Bullish na Bearish.

Akili itafunguka zaidi ya hapo ulipojiwekea ukomo.
 
Kuiamini biblia inabidi uwe na tatizo la akili kwanza
Uko sahihi.
Inabidi akili ibadilike kwanza. Hii ndio wenye akili mbovu wanaona ni tatizo.
Maana inatakiwa uanze kuona mambo kwa Jicho la ndani sio hilo unalotumia kuchat jf. Hiyo process inataka kiwango cha juu sana cha humility.
Renewing your mind. Romans 12:1,2
 
Ni kweli hata vichaa kwenye ulimwengu wao wanaamini ukichaa ndio akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…