naomba hili tulichimbe, hatuwezi kuwa mgongo wa wakenya kusonga mbele wakati sisi tunalala tu. kama tusingelinda resources zetu tangu awali, leo hii tusingekuwa na madini nk.
Hivi, naomba tujiulize, kuna faida gani kuungana na hawa jamaa? najua faida ipo kama tutakuwa tunakubaliana kulingana na maslahi ya kila nchi. lakini, kwa proposals za wakenya kama hizi, kuna faida gani? kuna nini kinajificha ambacho wanataka ku take advantage of our country? kuna nini wanalilia hapa, kama resources tunazo, hata tukikalia ni zetu, tutakuja kuchuma baadaye.
Kilimanjaro wameiba hadi wamechoka, sasahivi wanaona aibu kwasababu dunia imejua kuwa iko tz. serengeti wameshindwa na kulegea vilevile. baadaye watakuja kusema hata ngorongoro na Bagamoyo iko kwao, hata zanzibar watasema iko kwao.
unayetoa mfano wa Congo, resources za congo zinaleta migogoro kwao, lakini that is not the case here in tz. hapa tz resources hazileti migogoro hata siku moja. may be if you people come with the proposal to buy some land from Tz or some part of victoria from tz, and we may sell you at more than five trillion dollars if you can ever have that money.
watz tujifunze kwa waganda, waliachia kisiwa cha migingo, sasahivi wakenya wamesema chao, hadi wanataka kupigana. sasa,kama kakisiwa kale tu wanataka kupigana vile, je, ziwa? ikiwezekana tuachane nao kabisa. siku zote ogopa mtu anayetaka kutake advantage of your being.