Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,543
- 661
Kama kungekuwa na utawala wa sheria Afrika, basi sioni kwanini kungangania shirikisho badala ya kuunganisha nchi zote za maziwa makuu kuwa nchi moja. Lakini kwa kuwa watu wameshindwa kujiona kwanza wao kama Wanyaruanda, Wanganda Wakenya, wanajiona kuwa Watusi, Wabaganda, Wajuluo n.k, Inaonyesha hatuwezi kwenda mbele kwa kujiachia tu watu watembee kama Mijusi.
Tujenge utawala wa sheria unaoheshimu demokrasia na haki za binadamu, isiyokuwa na tabaka la watawala na watawaliwa, basi mengine tunaweza! Lakini hii tabia ya kusema kuwa nifanye hivi kumpiku yule ina matitizo makubwa. CCM imeshindwa tu kuwapa haki sawa CUF katika utawala wa nchi yao (Zanzibar) sasa huko tuendako? Tanganyika inaonekana inainyonya Zanzibar, huko tuendako?
Inabidi tufanye homework yetu kabla ya kuvamia haya mambo, wakati Mkapa anabinafsisha kila kitu hakuona haja ya kwenda kwa awamu na kufanya tathmini, sasa analalamika! tusije tukafikia huko, bado tuna nafasi. Tushirikishwe na tushiriki kikamilifu.