Wengi wetu wahenga tunaijua hii couple
Raqey ni mtu mwenye historia ya kusisimua katika kujitafuta kwake mpaka kujipata (zero to hero)
Sarah pia ni mwanamke mrembo na mpambanaji sana, kajipata kwenye biashara ya chakula
Kwa pamoja historia yao ya mapenzi mpaka ndoa ilikua ni nzuri sana, wamepitia mengi na wamesaidiana sana katika hustle zao mpaka kuwa wa juu... na pamoja wana watoto wanne vijana wawili na mabinti wawili
Mwaka 2023 kulikua na tetesi kwamba mume ni msaliti na picha zilivuja yupo na K mnato ya kiasia (mchina). Lakini wote wakaja front na kusema kwamba wameachana kwa amani na kila mtu ana mishe zake wanalea watoto kwa pamoja
Lakini currently tetesi zimevuja baba wa familia amegundulika na cancer anatakiwa kuanza matibabu na kubwa kuliko ANAMUOMBA MKEWE AMRUDIE
my take:
1. Binafsi nisingemrudia sababu iko wazi anahitaji tu msaada wa mtu wa kumuuguza na sio kwamba mapenzi yamerudi kwa mtalaka wake
2. Binadamu ni social beings, utu uzima huwa unakua mtamu kama ukiwa na mwenza mliyeshibana whether unaumwa au huumwi
Hivyo basi ukiwa unamtaliki mwenzio, hakikisha una mbadala wa kueleweka
Hii tabia ya kuzagaa halafu yakikukumbuka unarudi kwa mkeo anakupokea ilikua wanawake wa zamani, wa siku hizi wana roho ngumu kwelikweli