Baada ya kutoa mabandiko kuhusu hali ya Corona nchini, Kaimu Balozi wa Marekani aitwa Serikali kutoa ufafanuzi

Baada ya kutoa mabandiko kuhusu hali ya Corona nchini, Kaimu Balozi wa Marekani aitwa Serikali kutoa ufafanuzi

Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
Balozi huwa hawekwi ndani,kimahusiano ya kimataifa hiyo ishu bado sana ndogo,kinachofanyika hapo ni kutengeneza mazingira tu ya kuonekana kuwa Tanzania inapingana na kile kilichotolewa na ubalozi,hii hufanyika kwa nchi zote duniani.
 
Satire sio? OK!
Sasa mkuu kwenye nchi ambayo humuweka rumande wiki nzima raia wake eti kwa ''kucheka suti ya rais'' huoni ni ni nchi ya kipekee? Ile picha ya suti ya Magufuli enzi hizo Magufuli mwenyewe alitakiwa kuwa proud nayo. Awape vijana motivation kuwa ametoka mbali. Kusema ukweli ile picha ndiyo ilitakiwa iwe fahari yake ukitilia maanani waafrika wengi tunatokea kwenye maisha duni. Kile kweli ni kitu cha kumuweka mtu ndani?
 
Sasa mkuu kwenye nchi ambayo humuweka rumande wiki nzima raia wake eti kwa ''kucheka suti ya rais'' huoni ni ni nchi ya kipekee? Ile picha ya suti ya Magufuli enzi hizo Magufuli mwenyewe alitakiwa kuwa proud nayo. Awape vijana motivation kuwa ametoka mbali. Kusema ukweli ile picha ndiyo ilitakiwa iwe fahari yake ukitilia maanani waafrika wengi tunatokea kwenye maisha duni. Kile kweli ni kitu cha kumuweka mtu ndani?
Kwa maoni yangu, hapo ilibidi Idris atumie Confucianism Philosophy ya tenda kile ambacho hata yeye angependa utendewe. Mfano, anaweza akapost picha ya babaake huku anaidhihaki?
 
Serikali ya Tanzania imemuita na kumhoji balozi wa Marekani Tanzania juu ya kile kinachoitwa travel alert iliyotolewa na ubalozi huo.

Serikali imemtaka kuandika habari zilizothibitishwa na serikali ya Tanzania juu ya corona.

 
balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson akizungumza wakati alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Huyu beberu lazima serikali imshughulikie vilivyo kwa kuwatia hofu Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachokifahamu ni kua Marekani hua hawategemei hizi public available information ili kufanya maamuzi yao.

Na kwa nchi zetu hizi wala hawahitaji ridhaa ya serikali kutoa taarifa.

Tukumbuke prism project ya nsa na cia ya kukusanya taarifa zote Duniani na kusikiliza simu za watu wote.

Inawezekana kabisa hackers wa Marekani wameshaingilia mfumo wa mawasiliano wa serikali na wana taarifa zote za siri ambazo serikali haizisemi.
 
Km amekiuka sheria za diplomasia afukuzwe nchini.
 
USA imewaambia raia zake...Si ninyi serikali mnaficha data....Mtakula hizo data sasa. Mtapata watalii chini ya laki moja kwa mwaka. Serikali ya Magufuli ya ovyo, ovyo kweli imejaa washamba, malimbukeni na wauaji. Mtalipa hayo yote mnayoyafanya.
Hatutegemei hela za watalii,vyanzo vya mapato viko vingi hi nchi Ni tajiri.
 
Unafikiri sijui? Mbona nime-kejeli tu? Athibitishe nini wakati yeye anawapa raia wake hali halisi? Hujui nchi kama USA zinathamini sana sana usalama na uhai na raia wake na siyo kama hapa Bongo wanakoona uhai wa raia ni kama wa nzi tu?
Ukienda nje na ukakwama ndipo utakapojua namna TZ inavyowathamini raia wake. Waulize waTZ waliokuwa wamekwama India na Dubai. Nyie madogo msiojua namna dunia inavyokwenda mna shida sana, yaani mnavyoitukuza USA utadhani iko planet nyingine. The USA is rapidly losing global superpower status.
 
Balozi kakubali tu wito lkn hakuna cha kumfanya
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imemwita Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Imni Patterson ili kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.

Kaimu Balozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19.

Ubalozi wa Marekani wasisitiza maambukizi ya Corona jijini Dar yameshika kasi. Wadai Hospitali zimeelemewa! - JamiiForums

 
Huo ndiyo ukweli na Umy analijua hili kuwa USA siyo watu wa kuwa nawa nawa maana madhara yake yatakuwa makubwa
Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
 
Back
Top Bottom