Baada ya Kutuaminisha kuwa Hukumu ya Bernard Morrison ni leo, hatimaye mambo yawa Magumu kwa Yanga SC mpaka 14 Agosti, 2021

@Chige

On top of that, ni ule tu ubishi wa kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku kutaka kukomoana! What I mean, Yanga ishinde au isishinde, wala hawana mpango na huyo mchezaji!
 
Kuna Jambo naliona, Ngao ya Jamii Yanga Kucheza na Azam FC

Pasipo Shaka Tanzania inaenda kuandika historia yake katika Mchezo wa Mpira wa Miguu, Ni jambo ambalo wengi hawakutarajia kama linaweza kutokea, Kuna asilimia 80% Sasa kwa Klabu ya Simba kwenda kushuka daraja.

Wengi tulijaribu kutumia Elimu na Maarifa ambayo Mungu ametujaaliwa kutoa ushauri wakisheria na ushauri wakihekima kuwaomba wenye mamlaka ya soka Nchini kulitafutia ufumbuzi wa Kihekima juu ya tatizo la Bernad Morrison na Klabu yake halali ya Yanga lakini Bahati mbaya sana tulibezwa na watu kuchukulia mambo kishabiki zaidi. Bahati Mbaya sana mambo yameharibika hayawezi kutengenezeka tena. Bernad Morrison na Klabu ya Simba sasa wapo mdomoni mwa chatu, Chatu ambaye anavuta pumzi kulipa tumbo lake nafasi kwa ajili yakukiweka tumboni kile kilichopo mbele yake.

Logic reasoning

Kesi ya Msingi ambayo Yanga waliipeleka CAS ground yake ilikuwa madai ya YANGA "KUWA NA MKATABA HALALI NA BERNAD MORRISON"

Madai ya Pili ya Yanga

Yalikuwa, Klabu ya Simba kumrubuni Bernad Morrison kwa kumuahidi kumpa Dola Elfu kumi ambapo walimtangulizia Dola Elfu Tano ili aweze kukubali kusajiliwa na Klabu ya Simba ili hali alikuwa na mkataba na Klabu ya Yanga

Lakini pia Shauri B lilikuwa, Klabu ya Simba kumsajili Bernard Morrison akiwa ndani ya Mkataba na Klabu ya Yanga tena Shauri lake likiwa bado lipo katika kamati ya Sheria ya TFF.

Open fact

Kitendo cha CAS , kutoa Taharifa kuwa hukumu itatolewa tarehe 24/8/2021, Tafasiri yake nikwamba Bernad Morrison alikuwa na mkataba halali dhidi ya Klabu yake ya Yanga, Kama Shauri lakwanza la Yanga la madai kuwa Morrison Ana mkataba halali na Yanga lisingekuwa na ukweli, Basi kesi ingeishia hapa hapa kwenye hiki kipengele , CAS wasingekuwa na sababu yeyote ya kwenda kusikiliza tena vipengele B na C . Ambavyo Klabu ya Yanga inailalamikia Klabu ya Simba kumrubuni na kumsajili Bernad Morrison ili hali Ana Mkataba na Klabu ya Yanga

Bahati Mbaya sana Shauri hili wakati linajadiliwa kwenye kamati ya Sheria ya TFF , Chini ya Mwenyekiti Mwanjala walishindwa kujikita kwenye Determination of contract extension

Element kuu mbili za kisheria ambazo zimemuangusha Bernad Morrison katika Shauri hili ni

(a) Facts and (b) Defective on the case ground

Jkt Ruvu Kutoshuka Daraja

Kikanuni Klabu ikiwa imemchezesha mchezaji ambaye Ana mkataba na Klabu nyingine, Basi adhabu yake ni kunyang'anywa point katika mechi zote ambazo mchezaji husika ametumika kucheza.

Fact reference ya hukumu

Klabu ya AS VITA inayoshiriki ligi kuu ya Kongo, msimu huu imenyang'anywa Point na Ubingwa baada yakumchezesha Mchezaji anayeitwa Zao Matutala ambaye kipindi wanamtumia alikuwa na kesi CAS kama hivi ilivyo kwa Bernad Morrison, Bahati Mzuri AS VITA mchezaji huyu walimtumia kwenye Mechi Tatu tu za Ligi, Ambapo AS VITA walinyang'anywa point 9 baada ya Zao Matutala kushindwa kesi, Kutokana na AS VITA kunyang'anywa point 9 TP MAZEMBE wakajikuta wanakuwa Mabingwa wa Ligi kuu ya Kongo kwa msimu wa 2021/2022

Kwanini hukumu haijatolewa leo?

Kuna kitu kinaitwa Documents compile
Hii ni stage yapili kutoka mwishoni kabla yakutoa Taarifa ya hukumu
Kwasasa CAS wanacompile documents ili waweze kutoa hukumu

Katika tukio hili lakihistoria JKT RUVU yenye Point 29 itasalimika kushuka Daraja, na Klabu yetu ya Simba itaungana na Gwambina Fc yenye Point 35, Ihefu yenye Point 35 na Mwadui yenye Point 19

Rage naye kaamka usingzini, anasema kesi hii ngumu

Siku zote tunajifunza kutokana na makosa, Ingawa funzo hili ni chungu lakini naamini litakuwa funzo kwenye tasnia ya Mpira wa miguu Nchini

Mwikwabi James
Legendary
0766074160
 
We waache wabakie na mambo ya kesi wasifanye usajili.

Afu waanze kusema simba inabebwa, TFF wote simba,mara sijui nini..

Nyie endeleeni na habari za morison
 
Hakuna Kitu kibaya duniani kama Mtu mzima wa Mfano wako Kuandika Maelezo marefu yenye 'Foolish References' kama haya kisha ukajiona Umeandika mambo ya maana wakati kumbe Kiuhalisia ulichoandika ni 'Absolute Rubbish' pekee.
 
Yanga ni taasisi, na sio mtu!

Na kama ni taasisi, kesi dhidi ya Morrison hawezi kukwamisha kusaka wachezaji wengine kwa sababu idara inayohusika na makesi ni tofauti na idara inayohusika na kusaka wachezaji wengine!!
Upande wao kule hii ni Idara moja. Tena ipo chini na Babura Gonzalenzi. Hahahah.
 
Siku ya kusikiliza na siku ya huku huwa ni tarehe tofauti mkuu. Huo ndo utaratibu wa mahakama
Kichwa chake kimejaa kamasi za manara. Atawezaje kulitambua hilo?
 
We waache wabakie na mambo ya kesi wasifanye usajili.

Afu waanze kusema simba inabebwa, TFF wote simba,mara sijui nini..

Nyie endeleeni na habari za morison
Yanga SC alimaliza Usajili kabla ya tarehe 3-8-2021.
 
Pole kwa ujinga wako. Suala la kusikiliza na kuhukumu ni la mahakama. Umeonyesha umbumbumbu wako maana hata Mzee Aden Rage aliwahi sema mashabiki wa Simba ni mbumbumbu. Wewe tuliza chupi kubwa kama ile ya Morrison usubiri hukumu. Useless.
😂
 
Subira huvuta kheri,juha atajulikana hivi karibuni

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 

Hivi akili zenu mmepeleka wapi Utopolo? Wanaume wazima mnatokwa mishipa ya shingo kusubiri ushindi wa Mezani? Mnadhani Simba ni wajinga wamchezeshe Benard hadi Fainal ya FA? Nendeni mkapambane uwanjani mpate ushindi wa kuvuja jasho na siyo kutuletea blah blah za ndoto zenu za mchana.Subirni CAS watoe hukumu safari hii mtakimbilia kushtaki UN kabisa,maana hata FIFA mtawaona ni Simba
 

Naona double back to back imewachanganya haswa! Mnatia huruma sana Utopolo
 
Naona double back to back imewachanganya haswa! Mnatia huruma sana Utopolo
Mara yule jamaa wenu wa MIA SABA aliwaaminisha kesi hamna, tulieni tusubiri hukumu agosti 24.

Halafu ile barua aliyo tuambia mzee wa MIA SABA kwamba ipo FIFA imeishia wapi?
 
Wewe naye, utoto mwingi hauna hata cha maana unachoandika, ni mipasho tuu ya kitoto ili mradi umeandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…